Usilogwe ukaondoka nyumbani na kwenda usipopajua kwa kigezo cha kutafuta maisha

Usilogwe ukaondoka nyumbani na kwenda usipopajua kwa kigezo cha kutafuta maisha

SEHEMU YA KUMI NA MBILI

Ilipoishia,,,,,,,,,,,,,,

Daah haya majanga sasa, basi nikajikokota zangu kuelekea geto, ila shingo naiskia kama vile imefungiwa kamba alafu inavuta gari, Daah hawa jamaa si watu aisee, yan ukicheza unakufa hivi hivi,

Endelea,,,,,,,,,,,,,,,,

Nikajikokota taratibu paka geto, shingo inauma balaa, Basi nikamsimulia Da J yaliyotokea akanipa pole sana, Akachemsha maji akanikanda shingoni angalau ikaachia kidogo,

Basi Da J akanipa elf 20 kesho nikatafute simu, Kesho yake nikiwa najiandaa kwenda kutafuta simu Mara Sity naye akaingia, Akauliza simu imepatwa na nini toka jana haipatikani, basi nikamsimulia pale akasikitika sana, basi tukatoka kwenda kutafuta simu, Pia tukafanya mpango wa ku renew line,

Maisha yakazidi kuwa magumu maana simu ndo nilikiwa nategemea kutafutia kazi mtandaoni, maana Pc nilisha iuza ili kulipa kodi ya chumba, Basi nikawa sasa ni kusambaza cv ofisi kwa ofisi,

Basi nikatafuta panga langu nalichomeka kiunoni alafu napita ile njia ili nikutane na wale vibaka lakini sikufanikiwa, Basi maisha yakaenda hivyo, Mda mwingi naenda kushinda pale beting jioni narudi geto kulala hivyo yani,

Siku moja nikaondoka geto niende kule beting, geto nikaacha kumetuliaa maana hakukuwa na mtu nyumbani, Basi jioni niliporudi nikamkuta Da J anafua nje, Akaniuliza we chizi vitu umepeleka wapi, au umeenda kuhonga huko kwa malaya zako, sa mi sikumwelewa, kuingia geto nakuta geto jeupe kimebaki kitanda tu na chaga, yaani hadi godoro hakuna,

Nikashtula sana, Da J akaja, Nikamwambia Da J nimeibiwa vitu, Da J hakuamini, Akasema, mi nimekuja nikakuta mlango upo wazi, nikajua upo ndani, sa nakuita naona kimya, kuingia nashangaa hakuna vitu nikajua umeamua kuhama,

Daah ukisikia majanga ndo haya sasa, basi nikatoka nikaulizia kwa majirani nao wanaishia kushangaa tu, Daah haya maisha acheni tu, Nikampigia Sity akaja, akanikuta pale nimekaa kama bwege, yaan sijui hata nafanya nini, Sity akaniambia hivi wewe utakuwa umemkosea nini Mungu, yaani juzi tu hapa umekabwa ukaibiwa simu, hata mwezi haujaisha unavunjiwa unaibiwa vitu, hapana bwana ebu jichunguze umemkosea nini Mungu,

Sa mi nikifikiria sioni nlipokosea, au sababu siendi kanisani, lakini ni muda tu siendagi kanisani, tangu nianze chuo paka namaliza sijawahi kwenda kanisani, sasa iweje sasa hivi ndo yatokee haya, Basi tukakaa pale paka giza likaingia,

Sity akaomdoka, Mimi ikabidi nifungue tu kile kitanda nitafute mabox nitandike chini, maana nisingeweza kulala juu ya chaga bila godoro, Da J akanipa mashuka ndo nikatandika chini na mabox nikalala, Cha kushukuru ni kuwa nyuma ya mlango nlikuwa nimetundika begi langu ambapo kuna material tuliokuwa tunasoma na vyeti vyangu vipo huko, sa sijui hawakuliona, au waliona ni makaratasi tu na mavitabu hayana ishu, mi sijui ila Mungu saidia lilikwepo,

Basi usiku sikulala nikawa nawaza sana haya yote yanatokana na nini, nikakumbuka yale maneno ya Sity kwamba nijichunguze huenda kuna sehemu nimemkosea Mungu, Basi nikaamka nikapiga magoti nikasali ili kama kuna nilipokosea Mungu anisamehe,

Nikiwa bado nawaza nikaona kabisa kuwa siwezi kuendelea kukaa dar, Huu mji umenikataa nisilazimishe, swali sasa niondoke niende wapi, Kurudi nyumbani hapana yani akili ndo haitaki kabisa kusikia hicho kitu, Sasa nitaenda wapi,

Basi wazo likanijia kule Arusha naskia kuna kiwanda cha nguo, alafu kuna jamaa zangu kama watatu tumemaliza nao chuo naskia wamepata kazi huko,Namba zao nlikuwa nazo sema ndo zikasepa na ile simu iliyoibiwa, ila sio case,Ni bora niende huko huko ntawatafuta tu huko, Ni bora niende tu na mimi nikajaribu maisha, Ila sasa nikifika ntafikia kwa nani, Daah maswali yakawa mengi ila majibu machache, ila moyo ukawa umeshakufa ganzi lazima lazima niondoke huu mji,

Basi kesho yake Sity akaja, nikamshirikisha wazo langu, akakubali kishingo upande ila na yeye maswali yakawa yaleyale niliyojiuliza usiku, Ila nikamtoa hofu kwamba mimi ni mwanaume lazima nipigane nisikae kizembe tu, na maisha ni popote, Basi akakubali ,shida ikaja ni nauli napata wapi, Basi nikasema nitafute mteja wa kile kitanda ndo nipate nauli,

Kweli nikatangaza kwa wadau mbalimbali mmoja tu ndo akasema atanipa elf 50, nikasema fine, Basi nikaanza maamdalizi ya kuamsha zangu Arusha, Da J alipokuja jioni nikamwelezea, akasema bana usiende , nikamwambia sa nikibaki hapa ntakaaje , sina chochote, lazima niondoke, akasema usiende huko utakufa, nikamwambia mwanaume haogopi kufa,

Basi yule jamaa akaja akachukua kile kitanda akanipa hela, Mda huo Sity alikuwa kaondoka akasema atakuja badae alale huku ili kesho anisindikize stand, Basi kweli badae badae hivi Sity akaja, Tukaongea pale, Akanipa elf 30 akasema ameenda kutafuta ndo kapata hiyo, Basi nikawa na elf 80 tayari, Usiku ukaingia tukatandika mabox tukalala, Nikala zangu mzigo wa mwisho mwisho huku nnasikitika huu mzigo ndo nauacha hivyo daah,

Basi saa 11 Sity akanishtua nijiandae, nikaoga pale fresh, nikawa najiandaa andaa pale, wakati najiandaa nikimwangalia Sity usoni machozi yanatiririka tu, Basi nikakaa nianze kum bembeleza, nikamwambia we ndo mke wangu, ngoja nikatafute ntakuja kukuchukua niamini mimi, basi akatulia,

Basi Sity akabeba begi tukatoka, Nikamgongea Da J , nikamuaga pale, Daah alihuzunika sana, Basi akanipa elf 10 akasema utakula njiani, Basi nikampa ufunguo wa geto aje ampe mwenye nyumba, ingawa kitasa kilikuwa kimevunjwa na wezi, Basi tukaaga pale tukasepa,

Tukafika ubungo, nikapata gari la saibaba, lilikuwa bado halija jaa basi tuka kaa na Sity siti moja tukaongea mengi tu, ila Sity alikuwa anajizuia lakini machozi bado yanatoka, Ilipofika saa moja gari ikataka kuanza kuondoka, Sity akashuka tukawa tunapungiana kwa chini, Basi chuma ikaamsha taratibu, Sity akawa analikimbiza gari paka likatoka nje ya kituo, Basi gari ikakamata morogoro road, Sity tukamuacha kasimama tu pale kaduwaa gari inaondoka, Basi chuma ikaamsha Arusha moja hiyo

Itaendelea
Hiki kipande kimenigusa sana.
 
aah mwamba shusha nondo...ila me sitosahau siku kumi na mbili ndani ya mgodi..nilikula hadi nguo..pia wale jamaa walokaa siku 42 ndani ya duara huku wakila mende,nywele zao kucha na maji wanayo kojolea na haja kubwa huku pembeni kuna mwenzao marehemu daah..R.I.P uncle
 
Basi utakuwa mdogo Sana .Yalianza mabomu ya Mbagala ndo yakafuata ya Gongo la mboto wakati huo Hussein Mwinyi alikuwa waziri wa ulinzi(2009-2010)
Mabomu yalianza ya goms kwenye miaka ya 2003 kwa mara ya pili ndo hayo anayasimulia OP mwaka 2011 kisha yakafuata ya mbagala(sikumbuki mwaka). Naishi Gongo la Mboto ndomana nimekumbuka miaka.
 
Shusha nondo, halafu nakusifu hata huwajibu wanoko wa chai kabisaaa. Endelea hivyo hivyo
umeona eeh.yule mpwaungusijui anakaa kujibu mwisho anafyum anazira. dawa ni kutojibu


wewe jamaa uliiba lapptop bib alisema wakifunga hawafungui umesahau kwa nin mishe zako zinabuma.
ukiibiwa sio na wewe uibe sio sawa.tulia mungu atakulipia.sis tushadhulumiw sana ila huwez kudhulum na ewewe.weee unashagaa kuuza mabesen sis tumeaplly zoom kufika pale tunabiwa kaz yenu nyie ni kwenda ma shopping mall ukiona mtu kapendeza ana muonekano wa hela unamvaa unampa promo ya holiday tour akielewa somo unampa business card anaenda kuambiwa namna vacation offer yeye na familia yake.kwa hio unalipwa kwa commision ya wataofanikiwa kuwapa vacation package. nauli buku nane kwa siku hicho ndio kiliniweka mama m bongo mpaka aende vacation wakat maisha yake tayar yashavaa soks mpaka uson
 
Daah..mawanang..umenikumbushaa mbaal..na mie nlishawah ona tangazo Kama uliloliona aww..cemaa m wahusikaa walikua sinzaa..@nlienda nmechomekeaa kinomaa cku iyo..kufikaa palee..nlichokaa. washenz wale et.nitembezeee mabakuli@daah..kugonga nyumba za watu kwa kwel hapanaa !boraa kuchomaa mahind!thanks God now nko pazur Kia's!it was 2014
Wale wajinga , hawaishii kumtaka mtu tu ila mpaka elimu huziitaji pia

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
 
SEHEMU YA TATU

Ilipoishia,,,,,,,,,,,

Basi kwa vile jamaa yangu Frank yeye ana account na ndio mtu nnaemuamini na ni mtumishi mzuri basi nikamkabidhi kibunda aniwekee kwenye account yake mpaka nitakapopata account, Kweli umdhaniaye siye kumbe ndiye

Endelea

Basi nikahama pale kwa Frank nikahamia chuo campus, Nikafanikiwa kufungua account CRDB maana wao tuliambiwa boom linawahi CRDB kabla ya benki nyingine, Akilini napangia bajeti kile kibunda, nikasema nijibane nitumie nusu, halafu nusu niweke nikipata boom lingine niongezee ninunue PC (Laptop), maana story zilikuwa kwamba engineering bila PC hutoboi.

Basi baada ya kupata account nikasema nimcheki Frank ili anipe kibunda yangu niweke kwenye account, mzee pale ndo niliamini hela haina pastor wala mchungaji, nikaanza kupigwa sound, mara nipo mbali nikitoka nitaenda benki, Mara leo nimeenda benk ATM hazina hela, sound nyingi, siku nyingine namwambia sina hela hata ya kula basi ananipa elfu10 halafu anasema kesho nikija chuo tunaenda kwenye ATM, kesho ukimtafuta anakupiga chenga, mara hapokei simu, nikasema mzee hii balaa sasa.

Basi bana, akanizungusha wee, mwishoni ikabidi anichane ukweli, daah nilihuzunika sana, akaniambia kuwa alichukua hela yangu akachanganya na yake na mshikaji mwingine wakanunua pikipiki, wamempa mtu kila siku analeta elfu saba, Sasa nikamuuliza mi nitaishije, akasema usijali mi ntakuwa nakupa hela ya kula, pia ntakulipa kidogokidogo mpaka iishe, Nikasema daah hii mbona balaa tena.

Kiukwelii maisha yangu pale chuoni yakawa magumu sana, ikafika steji sina hela hata kumi, njaa inauma, Frank hapatikani kwenye simu, kwenda geto kwao kumefungwa hawapo, yaani hapo ndo maji unaita mma,

Pale hall two kuna matank ya maji ya kufulia na kuoga, huwezi amini yale yakageuka maji yangu ya kunywa, home naogopa hata kuomba hela maana hali halisi naijua, tena ingetakiwa mimi ndo niwatumie hela. Basi maisha yakaenda hivyo, siku nyingine Frank ananiipa elf 20, mara elf 10 mara asinipe, hivyo yaani.

Shule ikaanza, masomo kibao, mchana kutwa naranda randa kule Coet na drawing board langu, maana room ni mbali balaa , floor ya 11 na lift haifanyi kazi hivyo ni bora usubiri vipindi hukuhuku Coet.

Basi bana ikafika karibu na UE, PC nagongea kwa washkaji tu, siku moja nipo na PC ya mshikaji room napiga msuli mezani, Sasa inabidi nisome nimalize chapter zote kabla mwenyewe hajaja kuchkua PC yake, kwahiyo hata nikichoka vipi nasoma tu maana kesho yake kuna paper, Ilipofika saa tisa usiku nikawa nimetepeta balaa ,nimechoka balaa, usingizi huu hapa, nikasema cha kujifia ni nini nikaacha PC pale mezani nikasema nilale saa 11 nishtuke nimalizie, nikalala.

Kuja kushtuka saa 12, kucheki mezani PC hamna, umebaki waya wa adapter tu unaelea maana niliupitisha chini ya shuka kuelekea mezani nikawa nimeulalia, Basi nikajua jamaa watakuwa waliamka wakaizima maana niliacha inapiga mziki laini kwa mbalii, nikawashutua jamaa niwaulize aliyechukua PC mezani, wote wakasema hawajachukua, Duuh nikapata wazo au mwenyewe alikuja akaichukua, nikapanda floor ya juu nikamuulize, nikakuta bado kalala nikamwamsha nikamuuliza akajibu kwa kushtuka, hapana sjachkua, vipi imeibiwa??

Nikamwambia subiri, nikarudi room nikakuta jamaa bado wanadiscus kila mmoja anatoa mawazo yake, mwingine anasema alishtuka saa 11 akaikuta mezani, Daah sasa nani kachukua, mara mwenye PC akaja aliposikia jamaa wanavo discuss akajua PC yake imeibiwa, acha aanze kulia, tena kwa nguvu, PC yake Toshiba kanunua laki saba anaskia imeibiwa.

Basi bana, jioni ikafika, usiku ukaingia asubuhi kukakucha ndo hivyo tena PC imeenda, jamaa anataka hela au PC yake daah nikajiona sijui nna gundu, Basi ikabidi hela ya field ilipoingia takribani laki sita nimpe yote jamaa, Alafu mimi ntajua ntaishije, nitaendaje huko field na pia ntarudi vipi nyumbani, mzee usiombe yakukute.


Itaendelea
Sio usiombe yakukute, wewe ulikuwa ni lofa. Na nina mashaka mpaka now bado ni lofa!
 
SEHEMU YA KUMI NA TATU

Ilipoishia,,,,,,,,,,,,,

Basi chuma ikaamsha taratibu, Sity akawa analikimbiza gari paka likatoka nje ya kituo, Basi gari ikakamata morogoro road, Sity tukamuacha kasimama tu pale kaduwaa gari inaondoka, Basi chuma ikaamsha Arusha moja hiyo

Endelea,,,,,,,,,,,,,,,,

Chuma ikawa inatambaa balaa, safari imeshika kasi, watu naona wana mzuka kinoma na safari, naona kama wana enjoy, tofauti kabisa na mimi, sina raha, mawazo kibao, pembeni nimekaa na mtoto mzuri wa kichaga lakini sina hata time nae ( Nilijua ni mchaga baada ya kusikia akiongea na simu kichaga),

Nipo zangu kimya sina story na mtu mara simu ikaita, kucheki nikakuta ni Sity anapiga, nikapokea, Akauliza tumefika wapi, Nikamwambia tupo mbali sana, maana hata maeneo mi siyajui huko njiani, Basi akasema yeye kalala anahisi kama anaumwa vile, nikamwambia aende basi akachek maleria, akasema wala si maleria , ni mawazo tu anawaza ataishi vipi bila mimi, Ana feel upweke hadi anaumwa, Nikamwambia tuombe Mungu tu mambo yakikaa fresh tutaonana soon, basi tukaingia porini porini huko hakuna network simu ikakata,

Basi safari ikaendelea, mara nikapitiwa na usingizi nikalala sana, Kuja kushtuka nakuta gari imesimama watu wanashuka, nikamuuliza yule dada wa kichaga, dada hapa wapi, Akasema Mombo watu wanashuka kwenda kula, kucheki saa ni saa saba, kwenye simu kuna miscall za Sity kama zote, Nikampigia, Akasema mmefika wapi, nikamwambia ndo tupo mombo sehemu ya kula panaitwa Liverpool, Akauliza, we umekula, nikamwambia mi hata hamu ya kula sina, akanibembeleza na kunisihi sana, kwamba nikienda kula hata yeye atapata faraja,

Basi nikaona isiwe shida, nisije nikamuudhi mtoto mzuri bure, nikashuka nikaenda toilet, nikatoka nikaenda kununua sambusa mbili za nyama na soda nikarudi kwenye gari nikatulia,

Basi watu wakarudi gari ikaamsha, tukafika moshi mjini kama saa kumi hivi, Basi likaingia stendi, wenye kushukia moshi wakashuka, Wakapanda wengine wanaoenda Arusha, Basi likakaa pale kama nusu saa hivi hatimae likaondoka, safari ya kuelekea Arusha ikaanza,

Tukafika Arusha kama saa moja hivi usiku, Nikashuka pale kama mtu anaejua anapoenda vile, ili machalii ya r yasije niona wakuja yakanidandia maana stori zao nnazo,

Basi nikazunguka zunguka pale stand mwisho nikaamua nikae kwenye vile vibanda vya abiria, Pembeni kuna mama mmoja kaweka vitu vyake pale anauza chakula, Nikamsalimia yule mama, nikamuuliza eti kiwanda cha nguo kipo maeneo gani, akasema kipo kisongo kinaitwa a to z, nikamuuliza ni mbali kutoka hapa, akasema ndio, ni nje ya mji, unapanda kihiace ( daladala) nauli mia tano, Nikamuuliza hivyo vihiace vipo hapa, akasema inabidi uende standi ndogo inaitwa kilombero, huko ndo kuna vihiace vinavyoenda nje ya mji, basi akanielekeza ilipo hiyo stand, ila nikaona hata nikienda saivi ni usiku ntapata shida tu huko, ni bora nitulie tu pale stand paka kesho asubuhi ndo nianze hizo mishe,

Basi nikatoa simu nikampigia Sity nimjulishe nimefika salama, tukapiga stori pale kidogo basi tukamaliza,

Pale stand abiria wanaolala pale ni wengi tu, wanaotoka maeneo ya mbali ambao wanasubiri magari ya alfajiri sana, basi nikawa sina wasiwasi,

Muda ulivyoenda nikaweka begi langu kama mto, nikatia mbonji pale kwenye benchi, ila nikawa nalala kwa machale, kila saa nashtuka shtuka wasije machalii ya r wakapita na mimi,

Basi asubuhi ikafika, nikaenda kwenye kamgahawa flani hivi nikaomba maji nikanawa uso, nikapiga chai pale fresh, Nikatoka nikashika njia kuelekea stand ya kilombero huku naulizia maana ni mbali kidogo,

Kufika pale daladala kama zote, basi nikaskia kisongo kiwandani!!, Kisongo kiwandani!!, Basi nikajua ndo hii na hicho kiwanda itakiwa ndo hicho cha nguo, basi nikazama ndani, badae kikajaa hicho kikaamsha,

Basi tukatembea weeee tukatoka nje ya mji kabisa, tukafika sehemu tukakata kushoto tukatembea kiasi hivi mara nikaskia wale wa kiwandani!!, wale wa kiwandani!!, basi tukashuka, abiria wengine wakabaki gari hiyo ikageuza tulipotoka,

Basi pale ndo kiwandani, kuna geti kubwa na walinzi hapo nje, sema geti ni la nondo kwaiyo ndani unapaona, ila ndani tena kuna geti jingine huko ndo huwezi kuona maana geti si la nondo,

Basi pale nje kuna maduka na vibanda vingi tu, Nikajivuta kwenye kibanda kimoja nikanunua soda nikakaa nakunywa huku nasoma mazingira, nikajaribu kumuulizia jamaa pale kuhusu chance za kazi pale kiwandani, akasema pale kila ijumaa wnakujaga hapo getini wanachukua watu, nikapiga hesabu siku hiyo ilikuwa jumatano,kwaiyo inabidi nisubiri paka ijumaa ndo nije,

Basi nikajaribu kumuulizia kuhusu wale jamaa zangu kama anawafahamu lakini wapi, basi nikakaa sana pale paka jioni wafanyakazi wakaanza kutoka, aisee!! ni wengi kichizi, basi nikawa nawaulizia kama wanawajua wale jamaa zangu ila hakuna hata mmoja anaewajua, Nikasema sasa hapa kazi ipo.,

Basi kigiza kikaanza kuingia, hapa sasa nitafute pa kulala, mfukoni nna kama elf 60 hivi na machenji, nikaulizia gest maeneo yale nikaambiwa gest paka kisongo,

Basi nikachkua boda pale buku paka kisongo, nikaulizia gest pale nikaelekezwa gest moja maeneo yale, nikafika nikaulizia chumba nikaambiwa single elf 5 nikasema fresh, basi nikapewa chumba nikaeka begi langu nikaenda kuoga, nikatoka nikaenda kucheki msosi huko road,nikala nikarudi zangu room, nikajilaza kitandani nikampigia Sity tukaanza kupiga story,

Itaendelea
 
Back
Top Bottom