SEHEMU YA KUMI NA TATU
Ilipoishia,,,,,,,,,,,,,
Basi chuma ikaamsha taratibu, Sity akawa analikimbiza gari paka likatoka nje ya kituo, Basi gari ikakamata morogoro road, Sity tukamuacha kasimama tu pale kaduwaa gari inaondoka, Basi chuma ikaamsha Arusha moja hiyo
Endelea,,,,,,,,,,,,,,,,
Chuma ikawa inatambaa balaa, safari imeshika kasi, watu naona wana mzuka kinoma na safari, naona kama wana enjoy, tofauti kabisa na mimi, sina raha, mawazo kibao, pembeni nimekaa na mtoto mzuri wa kichaga lakini sina hata time nae ( Nilijua ni mchaga baada ya kusikia akiongea na simu kichaga),
Nipo zangu kimya sina story na mtu mara simu ikaita, kucheki nikakuta ni Sity anapiga, nikapokea, Akauliza tumefika wapi, Nikamwambia tupo mbali sana, maana hata maeneo mi siyajui huko njiani, Basi akasema yeye kalala anahisi kama anaumwa vile, nikamwambia aende basi akachek maleria, akasema wala si maleria , ni mawazo tu anawaza ataishi vipi bila mimi, Ana feel upweke hadi anaumwa, Nikamwambia tuombe Mungu tu mambo yakikaa fresh tutaonana soon, basi tukaingia porini porini huko hakuna network simu ikakata,
Basi safari ikaendelea, mara nikapitiwa na usingizi nikalala sana, Kuja kushtuka nakuta gari imesimama watu wanashuka, nikamuuliza yule dada wa kichaga, dada hapa wapi, Akasema Mombo watu wanashuka kwenda kula, kucheki saa ni saa saba, kwenye simu kuna miscall za Sity kama zote, Nikampigia, Akasema mmefika wapi, nikamwambia ndo tupo mombo sehemu ya kula panaitwa Liverpool, Akauliza, we umekula, nikamwambia mi hata hamu ya kula sina, akanibembeleza na kunisihi sana, kwamba nikienda kula hata yeye atapata faraja,
Basi nikaona isiwe shida, nisije nikamuudhi mtoto mzuri bure, nikashuka nikaenda toilet, nikatoka nikaenda kununua sambusa mbili za nyama na soda nikarudi kwenye gari nikatulia,
Basi watu wakarudi gari ikaamsha, tukafika moshi mjini kama saa kumi hivi, Basi likaingia stendi, wenye kushukia moshi wakashuka, Wakapanda wengine wanaoenda Arusha, Basi likakaa pale kama nusu saa hivi hatimae likaondoka, safari ya kuelekea Arusha ikaanza,
Tukafika Arusha kama saa moja hivi usiku, Nikashuka pale kama mtu anaejua anapoenda vile, ili machalii ya r yasije niona wakuja yakanidandia maana stori zao nnazo,
Basi nikazunguka zunguka pale stand mwisho nikaamua nikae kwenye vile vibanda vya abiria, Pembeni kuna mama mmoja kaweka vitu vyake pale anauza chakula, Nikamsalimia yule mama, nikamuuliza eti kiwanda cha nguo kipo maeneo gani, akasema kipo kisongo kinaitwa a to z, nikamuuliza ni mbali kutoka hapa, akasema ndio, ni nje ya mji, unapanda kihiace ( daladala) nauli mia tano, Nikamuuliza hivyo vihiace vipo hapa, akasema inabidi uende standi ndogo inaitwa kilombero, huko ndo kuna vihiace vinavyoenda nje ya mji, basi akanielekeza ilipo hiyo stand, ila nikaona hata nikienda saivi ni usiku ntapata shida tu huko, ni bora nitulie tu pale stand paka kesho asubuhi ndo nianze hizo mishe,
Basi nikatoa simu nikampigia Sity nimjulishe nimefika salama, tukapiga stori pale kidogo basi tukamaliza,
Pale stand abiria wanaolala pale ni wengi tu, wanaotoka maeneo ya mbali ambao wanasubiri magari ya alfajiri sana, basi nikawa sina wasiwasi,
Muda ulivyoenda nikaweka begi langu kama mto, nikatia mbonji pale kwenye benchi, ila nikawa nalala kwa machale, kila saa nashtuka shtuka wasije machalii ya r wakapita na mimi,
Basi asubuhi ikafika, nikaenda kwenye kamgahawa flani hivi nikaomba maji nikanawa uso, nikapiga chai pale fresh, Nikatoka nikashika njia kuelekea stand ya kilombero huku naulizia maana ni mbali kidogo,
Kufika pale daladala kama zote, basi nikaskia kisongo kiwandani!!, Kisongo kiwandani!!, Basi nikajua ndo hii na hicho kiwanda itakiwa ndo hicho cha nguo, basi nikazama ndani, badae kikajaa hicho kikaamsha,
Basi tukatembea weeee tukatoka nje ya mji kabisa, tukafika sehemu tukakata kushoto tukatembea kiasi hivi mara nikaskia wale wa kiwandani!!, wale wa kiwandani!!, basi tukashuka, abiria wengine wakabaki gari hiyo ikageuza tulipotoka,
Basi pale ndo kiwandani, kuna geti kubwa na walinzi hapo nje, sema geti ni la nondo kwaiyo ndani unapaona, ila ndani tena kuna geti jingine huko ndo huwezi kuona maana geti si la nondo,
Basi pale nje kuna maduka na vibanda vingi tu, Nikajivuta kwenye kibanda kimoja nikanunua soda nikakaa nakunywa huku nasoma mazingira, nikajaribu kumuulizia jamaa pale kuhusu chance za kazi pale kiwandani, akasema pale kila ijumaa wnakujaga hapo getini wanachukua watu, nikapiga hesabu siku hiyo ilikuwa jumatano,kwaiyo inabidi nisubiri paka ijumaa ndo nije,
Basi nikajaribu kumuulizia kuhusu wale jamaa zangu kama anawafahamu lakini wapi, basi nikakaa sana pale paka jioni wafanyakazi wakaanza kutoka, aisee!! ni wengi kichizi, basi nikawa nawaulizia kama wanawajua wale jamaa zangu ila hakuna hata mmoja anaewajua, Nikasema sasa hapa kazi ipo.,
Basi kigiza kikaanza kuingia, hapa sasa nitafute pa kulala, mfukoni nna kama elf 60 hivi na machenji, nikaulizia gest maeneo yale nikaambiwa gest paka kisongo,
Basi nikachkua boda pale buku paka kisongo, nikaulizia gest pale nikaelekezwa gest moja maeneo yale, nikafika nikaulizia chumba nikaambiwa single elf 5 nikasema fresh, basi nikapewa chumba nikaeka begi langu nikaenda kuoga, nikatoka nikaenda kucheki msosi huko road,nikala nikarudi zangu room, nikajilaza kitandani nikampigia Sity tukaanza kupiga story,
Itaendelea