SEHEMU YA KUMI NA SABA
Ilipoishia,,,,,,,,,,,,,
Mzee kwa mara ya kwanza natimba gerezani, wacha kabisa!! Siku hiyo sikulala kabisa, niliwaza mambo mengi sana, Nikakumbuka maneno ya Sity " Ebu jichunguze ni wapi ulipo mkosea Mungu", Nikakumbuka sana kijijini kwetu, Nikasema bora na mimi ningesepaga home kama Kidosho, Nikamkumbuka Happy na Mwanamgu Joyce, toka nimwone kwenye picha sijawahi kumwona tena, nikawaza saivi atakuwa mkubwa, sijui kama nitawaona tena
Endelea,,,,,,,,,,,,,,
Siku ile ni kama sikulala kabisa, nawaza mambo kibao, nawaza sijui hukumu itakuwaje, Upande mmoja naona kama ntaachiwa huru,upande mwingine naona kama nitafungwa, Najiuliza hivi nikifungwa itakuwaje,
Kesho yake asubuhi wale ambao tuna kesi mahakamani tukapandishwa kwenye karandinga la magereza tukaelekea mahakamani, Tulipofika mahakamani tukafungiwa kwenye chumba kimoja pale mahakamani, hakina dirisha, mlango ni wa grili kwaiyo mnajazana mlangoni mnachungulia uone kama utaotea mtu unae mjua, basi wengine wakipiga makelele pale mlangoni wakiwasemesha watu wanaopita karibu mi nimetulia zangu kwenye kona naskilizia,
Muda wa kesi yangu kutajwa ukafika, nikaitwa jina pale, mlango ukafunguliwa nikatoka kuelekea kizimbani, Mwendesha mashtaka akaisoma kesi pale, akasema mahakama ipo tayari kwa ajili ya kutoa hukumu,
Wote tukawa kimya tunamsubiri hakimu aseme, basi hakimu akasema kutokana na ushahidi uliotolewa na kwa jinsi mtuhumiwa alivyojitetea, mahakama imememkuta mtuhumiwa na hatia, Kabla ya kutoa hukumu akawapa nafasi wale wazee wa mahakama nao watoe maoni yao,
Mzee mmoja akasimama akasema kutokana na vitendo vya wizi kuongezeka katika manispaa ya moshi,anaiomba mahakama itoe adhabu kali ili iwe funzo kwa wengine, Nikaona kama mwili umeisha nguvu, kama kizunguzungu vile,
Hakimu akaendelea, akasoma vipengele vyake vya sheria, mwisho akasema nimehukumiwa kifungo cha miezi sita gerezani,
Nikatolewa pale nikarudishwa kwenye kile chumba nisubiri muda wa kurudishwa magereza, Sasa nawaza nivipi nitaanza maisha mapya ya gerezani, zile stori zote za gerezani nilizokuwa nazisikia sasa naenda kukutana nazo, Yaani sasa nikajua watu ni wabaya aiseeh!,
Muda ukafika tukapandishwa karandinga haoo gerezani, Kufika pale nikapelekwa kwa mkuu wa gereza, nikapewa maelezo ya jinsi ya kuishi mule gerezani, Nikapewa jezi zangu za orange zimeandikwa magereza tanzania, fulu suti kuanzia kofia paka chini, askari mmoja akaniletea maviatu flani hivi kama mabuti mabaya mabaya maana nilikuwa sina hata ndala,
Maisha ya jela yakaanza,
Mule ndani nikakutana na jamaa mmoja hivi ni mtu wa dini sana, yani yeye kuswali muda wote, ana bonge la singda usoni, Jamaa alinisaidia sana kunijenga kisaikolojia, akaniambia miezi sita si mingi, tena akapiga hesabu zake akasema hapa ni miezi minne tu unakaa, kwaiyo usiwaze, Wenzio hapa tuna namba ndefu, we unatoka kesho tu hapa, kwanza shukuru huyo hakimu kakuhurumia,kwa kesi yako ulitakiwa kula kuanzia mvua tatu,
Mi nikamwambia sawa,shida yangu ni kuwa mi sijafanya hilo kosa, akasema hiyo kawaida mbona, Akanionesha mzee mmoja, akaniambia unamwona yule, kala maisha na kosa hajafanya, akanionesha mwingine unamwona yule kala 30 na kosa hajafanya ,kwaiyo wala usiwaze, ila nikusihi tu ukitaka kuishi vizuri humu ndani we fata sheria,usiwe mkorofi, usipende makundi, usipende vitu vya watu, Basi tukapiga stori sana na jamaa paka usiku sana tukalala,
Mule ndani si kubaya kama nilivyokuwa nasikiaga, hakuna tofauti na shule, Kuna TV kubwa tu tunakula muvi,news, kuna draft, kuna uwanja wa mpira,yaani pako poa tu,
Maisha ya jela ndo hivyo yakaendelea,mwanzoni ni magumu sana, ugali maharage saa nane ndo imetoka hiyo, Kulima ndo usiseme, gereza lina shamba kubwa hilo, tunalima mahindi, maharage, kahawa ndo usiseme, mboga mboga, kuna mabwawa ya kufuga samaki, ng'ombe utachunga, kuna kiwanda cha mabuti ya jeshi, kuna kiwanda cha mikate ila huko ni wafungwa wanawake ndo wanapelekwa,
Sehemu nzuri za kula bata ni huko viwandani ila huku kwingine ni tabu tupu, yaani unasimamiwa na nyapara kulima unachapwa kama mtoto, Siku nyingine tunabebwa na karandinga tunapelekwa mbali huko kuna mashamba makubwa mzee unalima trekta likasome,
Basi mi nikafata yale jamaa aliyonihusia,nikawa sina time na mtu, nikiambiwa na afande fanya hivi chap kwa haraka nafanya, vitu vya watu sina time navyo, rafiki yangu ni yule jamaa tu,
Basi hakuna kazi nilikuwa siipendi kama kulima, nilikuwa natamani sana nipangiwe huko kiwandani, Basi siku moja tumeenda huko kiungi kulima, askari aliyekuwa anatusimamia nikamsikia anaongea na mwenzake kuwa kesho yeye atakuwa kiwandani, basi nikasema chance ndo hii, badae nikamfta yule afande, Nikamwomba anifanyie mpango na mimi nifanye huko kiwandani, Akasema basi kesho ukiniona nakuja kuchukua wafungwa na wewe uje,nikasema sawa,
Kweli kesho nikamwona kaja kuchukua wafungwa,na mimi nikajipeleka basi akanihesabu, tukaingia huko kiwandani, huko kweli ni bata, hakuna cha nyapara wala nini, ni nyinyi tu na maafande, hakuna kufatiliana, ni kugonga kazi tu, Kwanza mnafanya kazi mme rilax, mmekaa kwenye viti mnapiga stori,muda ukifika mnagonga chai, saa ngapi ngapi mnagonga maziwa yaani fresh, nikasema maisha ndo haya sasa, sio kule kuchapana mafimbo kama ng'ombe,
Basi nikawa nna nidhamu kweli,yule askari akanipenda sana, siku nyingine kama hatuingii kiwandani basi ananipangia kazi ambazo haziumizi, basi maisha yakawa yanaenda,
Kumbe bana mule ndani si wote wanafurahia wakiona mambo yako yakiwa yanaenda fresh, kumbe si huku mtaani tu hadi jela watu wenye roho za husda wapo,
Itaendelea
,