Usilogwe ukaondoka nyumbani na kwenda usipopajua kwa kigezo cha kutafuta maisha

Usilogwe ukaondoka nyumbani na kwenda usipopajua kwa kigezo cha kutafuta maisha

We jamaa kweli humpendi jpm, yaani kila sehemu lazima umdiss tu hata Kama hahusiki na topic.....yule jamaa anakubalika kinoma hata kama amekufa, katika waliotumbuliwa na yule mzee naamini na wewe umo maana chuki yako imekita mizizi na hutamsahau hadi unakufa.
We unampenda shetani
 
Hii inawezekana ikawa ndio chanzo cha matatizo.

Kumbuka yule Mganga aliwapa dawa Room mate wote na kuna maneno aliyanuia ndio hayo yamesababisha hekaheka hizi. Ili awe salama inabidi arudi kule kwa yule Mganga akakiri kosa lake kisha akamuondolee hii laana inayomuandama.

Jamaa anaweza kuwa mtu wa mateso maisha yake yote.
kumbuka yupe bibi aliwambia yeye anajua kufunga tu kufungua hajui na akatoa siku tatu mwizi arudishe mali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Gereza ni Kama Kijiji fulani hivi chenye Sheria Kali. Mle Kuna matajiri wanyonge kila kitu. Wachawi ,waganga . Pia wambeya waongo bila kusahau humo kunavibaka pia. Walawiti wapo. Mkuu huko kunawafanyabiashara wa nyanya, dagaa, kalanga mboga za majani etc. Mkuu hicho ni Kijiji kamili kabisa
Wewe jela ulikuwa kwenye kundi lipi kati ya hao?

Nini kilikufanya uende jela?
 
SEHEMU YA KUMI NA SITA

Ilipoishia,,,,,,,,,,

Mara nikapigwa na kitu sjui ni nini, kuanzia hapo ndo sikujua nini kiliendea tena, nikawa nimefloot,

Endelea,,,,,,,,,,,,,,,

Nilikuja kupata fahamu nikajikuta nipo wodini, Nimelala kitandani nimetundikiwa drip, nimepigwa bandeji karibu kila mahali, Sa najiuliza nimefikaje fikaje pale ,Kumbu kumbu haziji kabisa, Naona tu manesi wanapita pita, watu wana pitapita,

Basi nesi mmoja akaja kwenye kitanda changu, akaangalia angalia ile drip, anataka kuondoka nikamuuliza, Nesi hapa ni wapi? Akasema pale ni Majengo hospital, Nimefikaje hapa? Akasema uliletwa hapa na polisi ukiwa na hali mbaya sana, basi akaondoka,

Sasa pale ndo kumbukumbu zikaanza kunijia, nikaanza kukumbuka matukio, Nikakumbuka wale vibaka, nikakumbuka nilivyokuwa napigwa, Daah machozi yakawa yananitoka, Nikakumbuka begi langu walichukua wale vibaka, mbaya zaidi lilikuwa na vyeti vyangu vyote kuanzia vya shule paka cheti cha kuzaliwa,

Ahhhah niliumia sana, nikasema sasa yote haya ni nini, kwanini yanitokee mimi, Basi nikamkumbuka Sity nikasema lait angekwepo angenisaidia, Nikakumbuka maneno ya Da J siku ile namwambia kwamba nataka kuondoka niende Arusha, alisema "Usiende huko Utakufa" Nikahisi Da J alifunuliwa yatakayokwenda kunikuta huko,

Basi nikakaa pale hospitali, kumbe polisi bado wananilinda, Wanakuja pale kitandani wananiangalia wanaondoka, Basi nikawa nasikia watu pale wodini wananong'onezana huku wananinyooshea kidole, Wanasema yule pale ni mwizi, Aliletwa hapa hafai ila saivi kapata nafuu, Moyoni nikawa naumia sana maana mi najua mi si mwizi, sema ndo hivyo nani ataniamini,

Basi badae nilikuja kufahamu kilichotokea siku ile, Kumbe wakati wanataka kunipiga kibiriti pale chini kumbe polisi wakatokea, Watu walivyoona polisi wakakimbia wakaniacha ndo ikawa ponea yangu, Kumbe kituo cha polisi cha majengo hakipo mbali na pale uwanjani kwaiyo polisi walipopata taarifa wakaja fasta, Basi nikatiwa kwenye gari yao wakanileta pale hospitali, kumbe hospitali yenyewe ilipo na pale uwanjani imetenganishwa na barabara tu,

Basi nilikaa sana pale hospitali, paka majeraha yakaanza kupona, polisi wapo tu na mimi hawaniachi, basi siku ya siku nikapewa ruhusa, basi polisi wakanichukua paka pale kituoni, Nikaandika maelezo pale badae wakanitia ndani kwenye kiselo chao pale kituoni , mzee baba maisha ya huko selo sitaki hata kuyasimulia,

Basi siku ya pili nikapandishwa mahakamani pale moshi mjini mahakama ya mwanzo, nikasomewa shitaka langu la kutaka kuiba kwa kutumia nguvu, Akaja askari mmoja wa kituo cha majengo kutoa ushahidi, akaelezea jinsi walivyopata taarifa, na jinsi walipofika pale wakanikuta napigwa, pia akasema dada ambaye nilitaka kumuibia pia walimpata na yeye akatoa maelezo yake,

Badae akaitwa dada aliyetaka kuibiwa na yeye atoe ushahidi, basi akapanda yule dada, akasema yeye alikuwa anakatiza pale uwanjani huku anaongea na simu, mara ghafla mimi nikatokea nikaanza kumkimbiza nataka kumnyang'anya simu, alipoona vile ndo ikabidi ajitetee kwa kukimbia na kupiga ukunga,

Basi na mimi nikaambiwa nijitetee na kama nina mashahidi pia nilete, Mi nikasema sina mashahidi nitajitetea mwenyewe, Basi nikaileza mahakama kila kitu, kuanzia nilipoenda pale shule, nilivyokimbizwa na wale vibaka, nilivyopigwa mpaka nilipojikuta hospitali,

Basi hakimu akasema kesi imeahirishwa mpaka kesho kwa ajili ya hukumu, kwa sasa nitaenda mahabusu ila milango ya dhamana ipo wazi, Nani sasa wa kuniwekea dhamana, ikabidi nipelekwe mahabusu gereza la Karanga lilopo pale moshi,

Mzee kwa mara ya kwanza natimba gerezani, wacha kabisa!! Siku hiyo sikulala kabisa, niliwaza mambo mengi sana, Nikakumbuka maneno ya Sity " Ebu jichunguze ni wapi ulipo mkosea Mungu", Nikakumbuka sana kijijini kwetu, Nikasema bora na mimi ningesepaga home kama Kidosho, Nikamkumbuka Happy na Mwanamgu Joyce, toka nimwone kwenye picha sijawahi kumwona tena, nikawaza saivi atakuwa mkubwa, sijui kama nitawaona tena,

Itaendelea
ILE LAPTOP...
 
Hadi sasa Nilichojifunza toka kwenye hii simulizi:
1. Ni kweli ukiingia kwenye Mji/ Nchi ya ugenini ni rahisi kuingia matatizoni hasa kama huna mwenyeji wa kukuongoza. Hii inatoa uhalisia hata wale wanaokwenda kutafuta maisha nje ya Nchi bila connection, nao wanapitia matatizo mengi.

2. Vijana wengi wasomi baada ya ajira kusitishwa na JPM, wamejikuta wanaishia kufanya kazi ambazo hawakuzisomea na kupelekea ndoto zao za mafanikio kufifia

3. Sio Wote wanaochomwa moto kwa kuhisiwa Vibaka kumbe wengine sio wezi, ni vibaka wanawageuzia kibao watu wema na kuwaingiza matatizoni. (Tujenge tabia ya kupata ukweli kabla ya kuhukumu mtu)

4. Sio wote wanaofungwa wanakuwa ni wakosaji, wengine wanafungwa wakiwa hawana hatia

5. Wanawake wanauwezo wa kujiegesha sehemu kwa lengo la kupata Mchumba/Mume wamtakae. Mfano tumeona jinsi Sity alivyojenga tabia ya kwenda kujisomea UDSM huku akiwa na mawindo yake. Alifanikiwa kumtega mtoa mada kwa kumtanulia mapaja ili amchungulie vizuri, kisha akajipeleka mwenyewe akakae na kupiga story na mtoa mada kisha akafanikiwa alichokitaka.

6. Sity huyohuyo ametuonyesha matendo ya wife material anavyotakiwa kuwa, kumsapoti mtu unayempenda hasa anapokuwa kwenye matatizo. Alijaribu kumpambania japo hakuwa na uwezo, na namna alivyokuwa anamuamsha usiku ili agegedwe. Hii kitu binafsi sijawahi kuiona kwa wanawake wengine niliowahi kuwaonja.

7. Sehemu tunazoishi tujifunze kuishi vizuri na majirani. Tumeona jinsi jirani Da J alivyokuwa anamsaidia mtoa mada kwenye hali ngumu na kimawazo.

8. Baadhi yetu hatuna utamaduni wa kwenda Msikitini wala Kanisani, hivyo hatuoni haja ya kumshirikisha Mungu matatizo yetu hata tunapookuwa kwenye matatizo.
Mniombee....ipo siku nitaleta haki ndani ya nchi hii
 
Hadi sasa Nilichojifunza toka kwenye hii simulizi:
1. Ni kweli ukiingia kwenye Mji/ Nchi ya ugenini ni rahisi kuingia matatizoni hasa kama huna mwenyeji wa kukuongoza. Hii inatoa uhalisia hata wale wanaokwenda kutafuta maisha nje ya Nchi bila connection, nao wanapitia matatizo mengi.

2. Vijana wengi wasomi baada ya ajira kusitishwa na JPM, wamejikuta wanaishia kufanya kazi ambazo hawakuzisomea na kupelekea ndoto zao za mafanikio kufifia

3. Sio Wote wanaochomwa moto kwa kuhisiwa Vibaka kumbe wengine sio wezi, ni vibaka wanawageuzia kibao watu wema na kuwaingiza matatizoni. (Tujenge tabia ya kupata ukweli kabla ya kuhukumu mtu)

4. Sio wote wanaofungwa wanakuwa ni wakosaji, wengine wanafungwa wakiwa hawana hatia

5. Wanawake wanauwezo wa kujiegesha sehemu kwa lengo la kupata Mchumba/Mume wamtakae. Mfano tumeona jinsi Sity alivyojenga tabia ya kwenda kujisomea UDSM huku akiwa na mawindo yake. Alifanikiwa kumtega mtoa mada kwa kumtanulia mapaja ili amchungulie vizuri, kisha akajipeleka mwenyewe akakae na kupiga story na mtoa mada kisha akafanikiwa alichokitaka.

6. Sity huyohuyo ametuonyesha matendo ya wife material anavyotakiwa kuwa, kumsapoti mtu unayempenda hasa anapokuwa kwenye matatizo. Alijaribu kumpambania japo hakuwa na uwezo, na namna alivyokuwa anamuamsha usiku ili agegedwe. Hii kitu binafsi sijawahi kuiona kwa wanawake wengine niliowahi kuwaonja.

7. Sehemu tunazoishi tujifunze kuishi vizuri na majirani. Tumeona jinsi jirani Da J alivyokuwa anamsaidia mtoa mada kwenye hali ngumu na kimawazo.

8. Baadhi yetu hatuna utamaduni wa kwenda Msikitini wala Kanisani, hivyo hatuoni haja ya kumshirikisha Mungu matatizo yetu hata tunapookuwa kwenye matatizo.
sio kipindi cha jpm tu hata saivi bado graduates tuna hustle
 
Nilizaliwa mwishoni mwa miaka ya themanini katika kijiji cha chabutwa wilaya ya Sikonge mkoa wa Tabora, nilifanikiwa kupata elimu yangu ya msingi hapo kijijini, shuleni nilikuwa vizuri sana, si walimu tu bali hata wanafunzi walinipenda. Familia yetu ilikuwa ya maisha ya kawaida sana kwani baba na mama wote ni wakulima wadogo wadogo tu, kwetu tulizaliwa wawili tu mimi na mdogo wangu wa kiume.

Basi baada ya kumaliza shule ya msingi nilichaguliwa kujiunga na shule ya skondari Chabutwa iliyopo pale katani. Kwa vile nilikuwa John kisomo basi maisha ya shule hayakuwa mabaya ki ufaulu, Paka namaliza form four nilikuwa naongoza pale shuleni, Baba yangu alipenda kunihusia kuwa nisipende kujionesha kwa watu kuwa nina akili maana si wote wanapenda kuona watoto wao hawafanyi vizuri alafu watoto wa wengine wanafanya vizuri

Basi nilijitahidi sana kufata ushauri wa mzee ingawa kama unavyojua haya mambo hayafichiki, Kata nzima ilikuwa inanifahamu, kwenye vikao vya shule ndo usiseme maana niligeuzwa sample space (Sehemu ya wengine kujifunzia).

Basi nikamaliza four pale na Mungu si Athumani nikafaulu vizuri na kuchaguliwa kujiunga na shule ya Pugu Secondary kwa ajili ya five na six. Mzee wangu alifurahi sana si kwa sababu ya kufaulu tu bali nilichaguliwa shule ya mbali na pale nyumbani maana mzee alikuwa hana amani kabisa na majirani wa pale katani

Basi bana, siku ya siku nikatimba shule ya baba wa taifa, Askwambie mtu nilikutana na life la kibabe sjawahi kuona
Picha linaanza shule haina maji, Maji utajua pa kuyapata, kama utaenda mtaani kununua utajua mwenyewe, Ukitaka uzame pondi ( Huko bondeni kuna visima wanatumia wanakijiji ila maji yake yana magadi na fangasi wa kutosha)

Kufupisha story sitaelezea sana life la Pugu, ila kiukweli lilikuwa la kiume, Miongoni mwa vitu sitavisahau ni bweni letu la Mapinduzi 3 ambalo ndo lilikuwa linaaminika bweni la watu wakorofi shule nzima, pia nikiwa bado mgeni nilikaribishwa kwa kupigwa nguo zangu zote nikabaki na nliizokuwa nimevaa tu, yaani siku hiyo nimetoka pondi nimefua nguo zangu nikaanika kwenye ukoka, nikaondoka kwenda kutembea majohe, kurudi jioni nakuta ukoka unanikodolea tu hakuna nguo yaani Hadi boxer walichukua wahuni wale.

Kingine sitasahau ni tukiwa karibu kumaliza six, tumebakiza paper ya practical ya chemistry, siku hiyo ilikuwa jioni ki giza ndo kinaingia, nimetoka kupiga zangu nguna maharage, najisogeza taratibu naelekea kwenye kipindi cha dini, Mara ghafla naona watu wanakuja wengi wanakimbilia eneo la shule, Wa baba, wa mama wengine wana watoto, nikajiuliza kimoyomoyo haya maandamano ya nini tena, nikiwa bado nashangaa ghafla nikaona kitu hicho ndo kilifanya nione hii issue ni serious, nikamwona teacher wetu wa darasa nae anakuja mbio, tena mbaya zaidi ana kitambi sasa akikimbia balaa, na alikuwa na spidi maana ilikuwa kawaida yake kila asubuhi anatukimbiza ambao hatuendi assemble.

Duuh, nlipoona hivyo na mimi nikaliunga tukaanza kukimbia, kuna sehemu wanafunzi wanapenda kuangalia tv nikakuta nao wamesepa wameacha tv pale, Daaah sasa wote tunakimbia halafu hatujui tunakimbia nini, Sasa wakati naendelea kukimbia nikakutana na mlemavu mmoja yupo kwenye kiti chake cha matairi ( Maana ile shule ina wanafunzi walemavu pia),. Sasa hana mtu wa kumsukuma na kile kiti chake, kila mtu anaokoa nafsi yake, basi huruma ikaniiingia nikaanza kunsukuma huku tunakimbia, ebwanaeeh tumekimbia mwisho nikaona hapa nafeli, maana watu wanazidi kukimbia kuelekea bondeni huko alafu kelele zimekuwa nyingi, nikaona usintanie nikamwacha yule mlemavu nikaanza kukimbia mwenyewe.

Nikakimbia hatimae nikafika pondi, pale kidogo nikakuta watu wamerundikana kidogo,wanaulizana ni nini ila hakuna anaejua, ila juu angani anga limegeuka rangi, limekuwa jekunduuu kama vile jua lataka kushuka, alafu kelele kama vile watu wanapiga mabati huko angani au kama vile msitu unaungua sasa zile kelele za miti, daah hapo nikajua ndo mwisho wa dunia huu, wakati nageuka huku na kule mara namwona yule mlemavu ila saivi hayupo kwenye kiti bali anatambaa chini, nikajiuliza huyu kakimbia au kabebwa? Nikabaki nimestaajabu ila nikajichanganya asije kuniona akasema huyu broo ana roho mbaya, maana jinsi anga lilivyo jekundu yaani Hadi watu mna onana kabisa

Basi bana kelele zikazidi, watu woga ukaongezeka basi mbio zikaanza , tukapanda juu tukatokea Barbara kubwa ya pugu kajiungeni, Barabara imejaa watu wanakimbia, magari ndo usiseme, basi tukawa tunakimbia kelele zikizidi ukitazama juu unaona kama kimondo cha moto kinakuja hivyo unalala chini, kikipita unaamka tena unaaza mbio, Basi tukafika njia panda ya kisarawe na chanika, tukala kulia kuelekea kisarawe, mbio mbio unafika mahali unakutana na mdada anakimbia kanga inaanguka anabaki na chupi lakini hana muda wa kuokota kanga,ni kukimbia tu, mi pia sikuwa hata na hamu ya kutazama hayo mambo, maana unakimbia ukilala chini unasali ili likimondo lipite, basi ni kukimbia na kusali tu

Basi mara tukafika shule ya secondary Minaki , kulikuwa na wanafunzi pale nao wakaungana na sisi kukimbia, tukakimbia mara tukatoboa kisarawe,hapo ni usiku hata siijui saa ngapi, Basi pale kisarawe tukakuta watu wengi kinyama, yaanii pale ndo ikawa kama makutanio, watu wanaulizana ni nini,lakani hakuna anaejua dhahiri ni kitu gani kimetokea, Basi wakati tunashangaa pale mara ule mwanga na yale makelele yakawa takekaribia tena, watu wakaanza kuondoka kuendelea mbele,

Daah kwa jinsi nlivyokimbia na miguu ilivyokuwa inauma nikasema mi skimbii tena, kama kufa nife tu, basi nikaona cruzer moja imejaza watu nyuma inaondoka, nikaikimbilia nikaidaka, nikadandia yenyewe ikachanganya, sasa wakati natafuta sehemu ya kuweka mguu nikakosa, mikono ikachoka kubembea nikarudisha miguu kwenye lami, acha niburuzwe, nikaskia watu wanasema umeuaaaa, gari ikasepa nikaamka kujiangalia, nilikuwa nimevaa jinsi lakini ililiwa na lami paka ikakutwa Ngozi, nilichubuka vibaya, damu zinatoka balaa vidole vinatoa damu, ndala Sina maana zulikatika toka huko nikiwa nakimbia

Basi, mara nikaona cruiser moja imechorwa msalaba mwekundu, watu wanaikimbilia, na mimi nikazama, sasa wakati nazama kuna mama mmoja alikuwa mbele yangu, nikamvuta nyuma mi nikazama ndani, kumbe ni mke wa yule dereva anae endesha lile gari


Itaendelea

SEHEMU YA PILI

SEHEMU YA TATU

SEHEMU YA NNE

SEHEMU YA TANO

SEHEMU YA SITA

SEHEMU YA SABA
Kwanza story ni ya uongo,miaka ya 80 Sikonge yote ilikuwa haina sekondari hata moja
 
Kwanza story ni ya uongo,miaka ya 80 Sikonge yote ilikuwa haina sekondari hata moja
Sikonge,Tutuo,Ipole,Chabutwa ,Mibono,Usunga one,kulikuwa hakuna Shule ya sekondari hata moja,hadi ilipofika 1995 ndiyo ikaanziahwa Ngulu sekondari.

Mtunzi ni wa mchongo.
 
Back
Top Bottom