Usimamizi ni kitendo cha kuweka watu pamoja ili kutimiza malengo na madhumuni yatakakinayo. Usimamizi unajumuisha Mipango, Maandalizi, Mahusiano, Majukumu n.k baina ya mtu mmoja au kikundi cha watu au zaidi.
Usimamizi bora ni uwezo wa kuyatenda Mambo yote haya katika Hali ya ubora. Mary Parker Follet (1868-1933) aliandika maandiko kadhaa juu ya usimamizi alifafanua Usimamizi kama Sanaa ya kufanya vitu vifanywe kupitia kwa watu, Pia alieleza usimamizi kama Falsafa.
Unapaswa kufanya bidii sana kuwa msimamizi bora, Kila mmoja wetu anayo nafasi ya kuwa msimamizi bora wa maisha yake pia maisha ya watu wengine, Hivyo ni muhimu elimu ya usimamizi bora kuwa kipaumbele katika jamii kwa nyakati zote. Vilevile usimamizi bora ni uwezo wa kutengeneza nafasi juu ya kila jambo kuwa katika katika hali ya ubora. Tazama ni usimamizi bora pekee katika maisha yote ya mwanadamu unaweza kumpa matokeo bora zaidi yanayohitajika katika jambo lolote.
Kinyume cha usimamizi bora ni usimamizi duni, Hivyo usimamizi duni ni hali ya kutokuwepo au kupungua kwa usimamizi bora, Usimamizi duni una matokeo ya maanguko katika mambo yote, Tazama usipokuwa msimamizi bora katika Afya yako utaipoteza, usipokuwa msimamizi bora kwenye Ndoa yako utaipoteza, usipokuwa msimamizi bora kwa Watoto wako utawapoteza, usipokuwa msimamizi bora wa Fedha zako zitaisha vilevile usipokuwa msimamizi bora katika mahusiano yako yatavunjika, Maisha yote ya mwanadamu yanategemea namna usimamizi unatendeka, Hauwezi kutawala kama wewe sio msimamizi bora wa rasilimali pia hauwezi kuwa kiongozi bora kama hauna elimu juu ya usimamizi bora wa watu na vitu.
Hivyo mapendekezo yangu ni kuwepo kwa mafundisho juu ya elimu ya usimamizi bora katika mitaala ya elimu kwa watoto wetu pia watu wazima waelimishwe kwa namna yao faida juu ya kuwa na elimu ya usimamizi bora kwasababu kama watu hawatakuwa wasimamizi bora wataendelea kupoteza kila wanachokipokea, Mtu ataweza kumiliki na kudumu na jambo analolisimamia katika ubora.
Ni vizuri kumthibitishia Mungu wako kuwa una uwezo wa kusimamia vyema jambo unalomuomba au kubarikiwa nalo, Hii ndiyo sababu Mungu anatoa na kutwaa kwa wakati wake. Taasisi za kifedha hazikupi fedha unazohitaji bali fedha iliyothibitika kuwa unaweza kuisimamia, Jamii haikupi heshima unayoihitaji bali inakupa heshima unayoweza kuisimamia.
Usimamizi bora ni kwa kila jambo kila wakati na kwa kila mtu mahali popote, Kiongozi anapaswa kuwa msimamizi bora wa watu wa Taifa lake na rasilimali zao, Baba anapaswa kuwa msimamizi bora wa nyumba yake, Kijana anapaswa kuwa msimamizi bora wa muda wake, Mtoto anapaswa kuwa msimamizi bora wa mwili wake vilevile wazee wanapaswa kuwa wasimamizi bora wa afya zao wakati wote.
Kila mmoja miongoni mwetu anapaswa kujielimisha kuwa msimamizi bora pasipo kujali nafasi au tofauti zozote baina yake na watu wengine, Kwakuwa msimamizi bora itakuwezesha kudumu na kitu chochote Mungu alichokubariki au juu ya yote umuombayo.
Matatizo mengi yanayowakumba watu katika bara la Afrika na Nchi zingine ulimwenguni ni matokeo ya uhaba wa elimu na maarifa juu ya namna gani mtu anapaswa kuwa msimamizi bora.
Mfano tazama machafuko katika mzunguko wa hewa ni matokeo ya kutosimamia vizuri mazingira yetu vilevile Njaa, Vita, Umasikini, Magonjwa n.k ni matokeo ya kutokuwepo usimamizi bora wa watu pamoja na rasilimali zingine.
Agizo la kwanza na la msingi kutoka kwa Mungu ni mwanadamu kuwa mtawala bora juu ya mambo yote yaliyomo ulimwenguni. Utawala unamaanisha uongozi vilevile uongozi unamaanisha usimamizi, Pia maandiko yanaonesha mwanadamu aliumbwa siku ya mwisho ya uumbaji ili kuwa msimamizi baada kuhitajika juu ya maendeleo ya ulimwenguni yalihitaji msimamizi bora.
Hivyo hata sasa maendeleo ya Taifa yanahitaji misingi imara ya usimamizi bora na hii itawezekana kama kila mmoja miongoni mwetu atajiibidisha kuwa na elimu ya usimamizi bora katika mambo yaliyo ya msingi juu ya maisha yake na juu ya maisha ya watu wengine.
Kiongozi bora atajijenga na kujenga Taifa lake, Atasimamia vizuri afya yake na afya ya watu wa taifa lake, Atasimamia vizuri mazingira yake na mazingira ya taifa lake vilevile atasimamia vizuri uchumi binafsi na uchumi wa taifa lake.
Taifa linalosimamiwa vizuri linakuwa taifa bora bali linalosimamiwa vibaya linakuwa taifa duni.
Ni wajibu wa kila mmoja wetu kuwa msimamizi bora wa majukumu yake pasipo kujali nafasi yake katika jamii, Hivyo ni muhimu kuwa viongozi wa taifa letu kuweka mikakati juu ya upatikanaji wa lazima wa elimu ya Usimamizi bora kwa watu wake na kwa vizazi vyote.
Watanzania wote waelimishwe na kujielimisha juu ya faida za usimamizi bora wa mambo yao binafsi kama vile muda, Fedha, Familia, Nafasi zao na mengine mengi kwa maslahi yao na maslahi ya taifa kwa ujumla.

Upvote
1