Usimchaji mtu pesa ndefu, kuwa mwaminifu hautalala njaa

Usimchaji mtu pesa ndefu, kuwa mwaminifu hautalala njaa

mathsjery

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2015
Posts
2,287
Reaction score
1,855
Nimekuwa nashangaa baadhi ya tabia za wafanya biashara akiona mtu amepigilia mavazi safi acha yale ya kupauka Pauka ya karume au lango lango basi anamchaji pesa ndefu ili amhudumie.

Watu wengine huwa hawapendi/hawajui kugalaliza akisha sikia bei ni kubwa huondoka na wewe mfanya bizinesi unajidanganya eti "hakuwa mnunuaji huyo" utasubiri na kukopa sana pesa ya kula kwa sababu ya tamaa zako.

Mfano,
Naenda dukani nakuta viatu vipya na imara vyenye bei tofauti tofauti 50000, 90000, 110000tshs n.k . Napita tena mtaani kuna kiatu cha aina hiyo eti bei ile ile na ukiangalia unaona kabisa kimetumika mh! Jamaa inakumbia bei ile ile, huwa mnafikiri watu wote ni akina MOOOOO. Aya komaeni.
 
Bro una hasira sana, umeambiwa bei kubwa ukatimka mbio[emoji16] mkuu usiende sehemu zenye bei kubwa huko tuachie sisi akina moo.
Wewe haujanielewa, nafanya comparison kati ya bidhaa mpya dukani na used mtaani iweje viwe na bei sawa yaani kitu nakikuta lango lango kimetumika uniuzie bei sawa na kile ambacho hakijatumika?

Hata MOOOOO hawezi nunua
 
kuna mwalimu wangu alikua akituambia "ukiona kitu bei kubwa jua wewe sio mlengwa wa hicho kitu"...ndo maana kuna wanaonunua embe supermarket na embe hizohizo wengne wana nunua buguruni
 
Huyu jamaa usikute ananisema mimi,kaomba kwa mkopo nimemgomea ndio tunakuja dhalilishana humu..
 
kuna mwalimu wangu alikua akituambia "ukiona kitu bei kubwa jua wewe sio mlengwa wa hicho kitu"...ndo maana kuna wanaonunua embe supermarket na embe hizohizo wengne wana nunua buguruni
Tatizo bei kuwa sawa embe la supermarket ni safi na mengine hufungashwa vizuri sasa wewe uniuzie embe ulilooshea maji ya kwenye kopo la kupewa na sahani wakati mfuko najitegemea kwa bei ile ile
 
Niliwahi kununua kiatu kilichouzwa elfu 60 kwa sh elfu 20.

Nikaja kugundua wanaanziaga bei kubwa ili akija kukushushia bado hapati hasara.
 
Kuna siku nilikuwa shinyanga, nilitembelea sehemu wanayouza makoti na masweta.. nilikua nahitaji moja tu la kishkaji niingie nalo porin..

Basi kuchagua pale, ishu ikaja kwenye bei jamaa anakaza kushuka sababu ya aina ya sendo nilizo vaa!

Nilishangaa sana yaani mtu anakuclassify kwa ulivo vaa...

Suluhu: ili kununua kitu bei ya chini, ni kuvaa rapurapu.
 
unaweza ukaambiwa jeans 50k, mwenzio ile ile akanunua kwa 10k tu.. negotiations muhimu
 
umemtaja mooo
of coz ana apeche alolo lakini hakuna watu wana BURGAIN duniani kama wadosi...
ila akienda kwa mdos mwenzie atanunua bei yoyote ila GOLO(mswaili)utashushwa bei hadi na boksa itakushuka.
ila wee GOLO nenda maduka ya wados kila kitu anakwambia junioni hii
 
unaweza ukaambiwa jeans 50k, mwenzio ile ile akanunua kwa 10k tu.. negotiations muhimu
Mfano mimi huwa siwezi kabisa kugalaliza sio kwamba nina pesa huwa naona ni kusumbuana tu kama bei simudu natembea mbele labda aanze yeye kunambia pungufu otherwise let's find money
 
Back
Top Bottom