Usimpe mtu connection ya kazi ni Bora uiuze kwa gharama

@GENTAMYCINE aliposema kua wakristo mna roho mbaya sikumuelewa vizuri ila sasa ndo inajidhihirisha waziwazi

Tizama Tz hii waloendelea na matajiri ni watu ambao wanapeana connection sasa ww endelea na roho yako iyo ya mkono wa birika
 
Wewe jamaaa una roho mbaya adi nimeipenda[emoji23][emoji23][emoji23]kwani wewe na mwigule Nchombi ni ndugu?
 
Bila connection hupati kazi mkuu
Kama upo serious na kutafuta huwezi kukosa connection. Me kazi za sales sizipendi sana na ndio ninabahati ya kuzipata.
Zinamfanya mtu atembee kutwa nzima, daah
 
Msaada unakanuni zake.
Sio kila mtu ni wakusaidiwa, kasome vizuri maandiko au visa vya wahenga.

Kuna watu ukiwasaidia amini amini nakuambia umejitia kitanzi mwenyewe.
Ni kumuomba Mungu macho akuonyeshe
Kwel kabisa mkuu yalishanikuta kunadogo alikuwa mkoan sasa mimi likuwa kwenye kampun frani ya bas dogo alinitinga sana nimtafutie kaz yoyote kwenye kampun hadi baba yake alikuwa ananitinga sana nikaona sio kes dogo nikamsogeza sasa kilichonikuta Mungu anajua
 
Ni kweli bora kuuza koneksheni maana kuna mwamba humu kapewa mchongo baada ya wiki tu anakuja kuomba ushauri jf namna ya kuacha kazi na kumwmbia mtu aliyemtafutia so unaona kabsa Watu hawapo siliazi na wanasahau kuwa ajira ni ngumu sawa hv ,
 
ila kweli kuna jamaa nilimtaftia kazi ya uhakika kila mwezi akawa analipwa 450,000/= lakin akaacha bila kuniambia nilivyokuja kumuuliza akasema mshahara mdogo
Amekaa mtaani siku moja anaomba nimtaftie kaz nyingine nikamkazia badae akaomba arudi kule kwenye laki 4 na 50 nikamzibia pia
 
Kaka hii inanihusu kabisa ... Nina ushuhuda kuna mtu yupo bongo alikuwa akinisumbua sana anatafuta kazi nikamtafutia mahali fulani hapo bongo ...huyo bosi ikabidi aniuzie hiyo nafasi kwa 1.5M japo hii jamaa aliyekuwa ananisumbua hakujua kuwa nimetoa ila nilifanya hivyo kwaajili ya family friend relation toka tuko watoto sana.. jamaa kafika huko Job miezi miwili mitatu anadai aongezewe pakee la sivyo anaacha kazi ...net pay yake kwa mwezi ilikuwa 1M ukiondoa makato ya PAYEE na Mifuko ya Jamii baada ya usumbufu wa muda wa wiki kadhaa Bosi wake akampa option mbili 1. kuendelea na kazi au 2. aandike barua ya kuacha kazi kwa hiari yake jamaa akachagua kuacha kazi kwa hiari yake kwa kuwa bosi kagoma kumuongeza mshahara .. yaani kwa aibu jamaa hajanipa taarifa mpaka huyo bosi wake alipokuja kunichana akaniambia kufanya kazi na watanzania inabidi uwe katili kidogo nijitahidi nisiwe soft sana ile kauli ilinikera sana ila nimejifunza... Tanzania sitakuja kumwamini kijana yoyote kwenye mambo ya connection.. 90% ya vijana shida wamezizoea wapambane tu na umaskini wao kichwani japo wana vyeti mikononi...
 
Dah mkuu vijana waaminifu tupo usiseme ivo mkuu watu wenye shida wapo we kma una connection nipe hutojuta ila iwe ya halali tuu
 
Kama upo serious na kutafuta huwezi kukosa connection. Me kazi za sales sizipendi sana na ndio ninabahati ya kuzipata.
Zinamfanya mtu atembee kutwa nzima, daah
Kazi Sales zinakupa experience nzuri sana na Zina pesa
 
Kama upo serious na kutafuta huwezi kukosa connection. Me kazi za sales sizipendi sana na ndio ninabahati ya kuzipata.
Zinamfanya mtu atembee kutwa nzima, daah

Jiongeze

Nimepatia maisha kwenye Sales, Kaa hapo hapo usubiri kuchumia kivulini
 
Mkuu huwa unasema ukweli mchungu na ni ukweli ulio wazi naunga mkono hoja

Nje na mada kidogo mkuu Taikon wa fasihi Kuna kundi limeibuka kutoka kaskazini mwa Tanzania hapa JF hasa Arusha wakidai kuhujumiwa na serikali kwamba pesa zinazo patikana mkoa wa Arusha ndo zinajenga Dar,Dodoma nk mbaya zaidi wanafikia hatua ya kusema wanahitaji kujitenga na kutengeneza taifa la United State of Arusha kwa kuiunganisha Arusha na Moshi sababu ya wewe mkuu umekuwa unatoa elimu nzuri Sana kupitia uwezo wako katika fasihi na ujunzi wa lugha sanifu ya kiswahili naomba ukipata muda andika jambo kuhusu hili maana mbegu isha anza kumea ya ukanda.
 

Kwema Mkuu.
Sawa haina shida Mkuu ngoja tutafanya hivyo.
Wanaosema hivyo wengi wao sio watu wenye kufikiri vizuri.
Ila hatuwezi kuwanyima haki Yao ya kutoa maoni vile wanavyoona Kwa akili Yao.
 
Acheni mambo yenu. Wewe mwenyewe umesaidiwa sana hadi kufikia hapo.
Kuna mtu nilimsaidia dili kubwa sana na hadi Leo amebadilisha maisha yake.
Sasa nikayumba sana financially nikawa najisemea huyu jamaa anajua hali yangu mbona hata hastuki au hata kuulizia naendeleaje?

Kumbe na yeye anafikiria kitu kikubwa Cha kunifanyia ili kunisaidia.
Aisee out of nowhere napokea simu yake kuwa nikaonane na bosi fulani kwa ajili ya kazi.

So, tufanye wema. Kuna wenye kukumbuka fadhira pia kuna wapumbavu. Fuata moyo wako.
 
Moja Nini Faida / Kazi ya Pesa ?, Pili Tenda wema uende zako..., Tatu unaweza ukamsadia mtu derseving kitu fulani bure ila down the line akakulipa maradufu kuliko angekupa vipesa kadhaa na kuondoka kwa shingo upande kwamba wewe ni dalali / fisadi...

Pili ukimuuzia mtu kitu una obligation ya kuhakikisha kwamba ulichokiuza kina value, sasa akienda kule kumbe kazi ni ndivyo sivyo unakuwa kama umeshiriki kwenye ulaghai....

Binafsi mtu yoyote deserving mwenye uwezo wa kitu fulani tampa ufahamu wangu wote bure sababu ninajua ata-fit sehemu fulani na kule ninakompeleka kama ni kwa wadau wangu ninajua ataongeza tija; na sio kuwapelekea jamaa zangu misfits sababu tu ya njaa yangu / ulafi wa pesa...
 
Aah post hii mkuu ungeipost ata wiki ijayo nikiwa nishapata Kazi Man, niko na mdhamini wangu alafu naona huyu jamaa pia ni member humu, akiuona huu uzi mambo yanaweza kuwa tofauti. Punguza ukuda Kaka mtaani pagumu ndugu yangu.

Bless brother bandiko ni zuri mno lakini ungepost wiki ijayo🙂
 
Daah huyo jamaa alichezea sana bahati lakini mkuu kama bado unayo nafasi usisite kutusaidia maana vijana waaminifu bado tupo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…