Usimuahidi mwanamke kumuoa wakati huna malengo naye

Rajabmbisha

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2024
Posts
316
Reaction score
530
Heshima yenu wanajf, ipo hivi: Nipo kwenye mahusiano na huyu mwanamke kwa miezi minne sasa. Wakati namtongoza nilimuahidi kumuoa, na hapo ndipo nilikosea—nilimwambia nitamuoa ilhali sikuwa na malengo hayo.

Baada ya mwezi mmoja, usumbufu ukaanza; mara anauliza ni lini naenda kwao kujitambulisha.


Nikawa nampiga tarehe. Nilivyomuahirisha mara nyingi, ilibidi nihadi tena kwamba mwezi huu nitaenda kwao. Kiukweli nilimpa moyo tu, lakini sina nia ya kwenda kwao.

Sasa binti ameacha kazi na kurudi kwao kunisubiri. Najisikia vibaya sana. Natamani nimuambie ukweli kwamba sina malengo naye, lakini najua nikifanya hivyo nitamuumiza sana.

Ninajua ananipenda kupitiliza—hilo sina shaka nalo.

Mwanamke anayekupenda utamjua; mapenzi napewa muda ninaotaka, tena for free. Kosa dogo tu, anaomba msamaha bila kinyongo.

Kuna mengi siwezi kuyaandika yote hapa, lakini hata baada ya kumwonyesha ishara nyingi za kutomhitaji, bado hakati tamaa.

Ujumbe wangu kwa vijana:

Kama mpo kwenye mahusiano, waambieni wanawake wenu ukweli ili wachague wenyewe kuliko kuwadanganya. Na nyie wanawake, muwe mna jiongeza—muda mwingine mnaonyeshwa hamtakiwi, lakini bado mnaendelea kung’ang’ania.


Muwe na siku njema.
 
 
Ukirogaa unalalamikaa
 
Hujachelewa mwanetu ,Ukishamaliza kusoma post hii mwambie binti hutamuowa na omba Toba maana ushasema huna nia,ila bado unafanya vitendo vya kuonyesha una nia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…