Usimuamini Mwanasiasa hata siku moja: Hili kuongeza mshahara lipo kisiasa sana

Usimuamini Mwanasiasa hata siku moja: Hili kuongeza mshahara lipo kisiasa sana

AbuuMaryam

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2015
Posts
2,577
Reaction score
4,637
Mwanasiasa akiingia ndani na akakwambia nje mvua inanyesha toka kahakikishe...

Mwanasiasa akisema anakupenda... Geuza kwa upande wake kinyume...

Akisema amekufanyia hivi au vile... Chunguza vizuri.. Kuna nini baadae...

Mkikaa baadae mkatulia kwenye akili zenu mtajua tumepigwa changa la macho...

Nakumbuka ilitangazwa faini za bodaboda zimepungua kutoka 30,000 mpaka 10,000...watu walishangilia kisiasa...

Walipokaa wakatulia wakafikiri upande wa pili... Wakakumbuka. HUWEZI KOSEA KILA SIKU UKAKAMATWA UTOE FAINI... ILA MAFUTA UTAHITAJI KILA SIKU ILI CHOMBO KITEMBEE. HUKO NDIO MMEPIGWA NA KITU KIZITO...

SIIPENDI SIASA. SIWAPENDI WANASIASA. NA SIWAAMINI WANASIASA.

WANASIASA WANIACHE NA MAISHA YANGU NA MOLA WANGU. WAO WAJILIE TU DUNIA YAO. ILA WAKUMBUKE KUWA. HIZO PESA WANAZODHULUMU WATU ZITAWAACHA AU WAO WATAZIACHA HIZO PESA.

KUNA MTU ALIKUFA HATA MSHAHARA WAKE HAKUUTUMIA...
 
Kujitenga na siasa ni ngumu aisee labda utengeneze maisha yako binafsi huko msituni🤣🤣🤣

Wasomi wengi wa kale(enzi hizo) walifia maporini kisa siasa za nchi zao
 
Wasiongeza mishahara!! Wangekuwa wana uchumi!?

Ni muda muafaka watumishi kupata nyongeza, miaka mingi wamesota bila nyongeza!
 
Haupendi siasa?Inabidi ukaishi kwenye pango la mbuyu huko porini.Siasa haikimbiwi.
HALAFU:
Tusubiri kwa kutulia ili tuone kama ni kweli watumishi wamepata nyongeza.
 
Back
Top Bottom