Usinunue vitu online kwa kutipia TIGO MASTERCARD!

Usinunue vitu online kwa kutipia TIGO MASTERCARD!

siku hiyo nilishangaa msg inaingia kua nimeshafanya malipo na tigo pesa mastercard ,muamala ambao sijaufanya ,duu ilikula kwangu tigo hawana sapot kabisa mpaka badae kufatilia sana nikagundua ni malipo ya application za simu

Kiufupi ukilipia kitu online kwa kutumia tigo pesa mastercard automatically card inaweza kufanya malipo mengine bila wewe kua na taarifa utashtukia tu unapokea msg kua muamala umekwishafanyika ,poor service ni wizi mtupu.kwa sasa nimeacha kuweka hela huko kuepusha hili.
Mkuu kama ulisubscribe kwenye App au service ni ngumu sana hata kwa card provider wengine kuissue reversal.
Changamoto nayoiona kwa Tigo na Airtel ni ujinga wao wakuchanganya card na wallet za Tigopesa au Airtel Money kwa hiyo mteja huna control ni kiasi gani kiwepo kwenye card.
 
Sheria zipo na wanasheria wapo
Watanzania kuwa wagumu kuwaburuza Hawa wapuuzi mahakamani ndiyo sababu za wao kuburuza wananchi na kuwaibia hovyo
Lakini kama tungezingatia sheria kwa kila makosa wanayofanya huduma ingekuwa nzuri

Siyo wananchi wa kawaida wala wanasheria wa nchi hii wanaojielewa
Mambo ya kijinga ni mengi na ni fursa za kupiga pesa kirahisi tu lakini watu wamekaa tu

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
Mkuu ni kweli unachokisema, kuna uwezekano ni kweli wengi hatujui hizi sheria lakini pia nafikiri aina ya miamala tunayopigwa haitupi motisha ya kutumia hela zaidi kwenye kuajili wanasheria na kutumia muda mahakamani.
Pia ukijaukasoma Terms and Conditions documents zao, zimekaa kwa design ya kuwafanya washinde hizi kesi
 
Means huna pakushika mzee duuuuh... Bongo noma, hivi Hakuna namna yeyote Ile ambayo inafanywa na mamlaka kwaajili ya kukomesha hizi tabia maana ww sio wa kwanza na wanao fanya hivyo big company sio kwamba ni genge tuuy la wahuni kwamba itachukua muda mrefu kupatikana kwao au ikoje iyo mambo apo.
Shida ukilalamikia kwao kule wanasema fanya mawasiliano na mtandao wako ulioko huko Tanzania kwa kweli tunapigwa mpaka tunapigika sio sawa unapoteza hela nyingi na tigo wanafeli kuzichukua kwaajili yako, biashara za mtandao ni risk sana kwasisi watanzania hatuna sehemu ya kufanya tracking pesa ilipopotelea, na mitandao haisaidii kabisa
 
Mkuu pole sana kwa hii changamoto, na mimi nimekuja kujifunza kuwa hawa watu hawajali na mara nyingi hawataki kubeba jukumu la kumsaidia mteja wao hata kutosupport ya documents pia ni shida kwao.
Sheria zipo za kumlinda mteja lakini imekua ni kawaida kumuachia mteja ujipambanie ulichokipoteza huku unakuja kufeli maana huna njia nyingi za ku access ulichopoteza kama wao walio kuwa kwenye system
 
Hawa toka niliponunua simu moja ya duka lao na kuahidiwa ofa, lakini muda ukifika kupata hiyo ofa sasa mtihani.
Wahuni sana.
 
Pole mkuu, njoo mpesa Visa....MPESA VISA ndio mpango mzima yaani unaweka pesa kiwango unachotaka kulipia kwenye card ya Visa kwa hizo subscription au manunuzi, inatokea errors kukata haiendi kukata kwenye mpesa yako coz haingiliiani hata kidogo .wewe ndio mwenye permission ya kuweka fedha kwenye card au kutoa kwenye card.
 
Mkuu mimi nimefanya hizi electronic transaction kwa zaidiya miaka 15 sasa.Na nitakwambia kwamba kwa uzoefu wangu mifumo yote Tanzania ambayo inahusika na malipo kwa kupitia VISA na Master Card ni Majanga.Hii ni Kuanzia mifumo ya Mabenki,Mifumo ya virtual Card n.k.

Nimefanya miamala na benki kadhaa na mitandao yote ya VODA,TIGO na AIRTEL.

Kwanza kabisa inapokuja swala la technical au operational support wako chini kabisa yaani ni zero hawaelewi hata product yao wenyewe wala kuiamini.

Pili kunapokuwa na Transaction duplicates pesa haiweza kurudishwa kwenye akaunti yako.So mimi Huwa nahakikisha kwamba ninapotaka kufanya Muamala wa kulipa kwa kadi basi akaunti yangu inakuwa nakile kiasi tu ambacho kinatkiwa kulipwa BASI,Sizidishi hata thumni.

Pili huwa sipendi sana kutumia SAME bank account kwa ajili ya normal transaction kwenye hizi online transactions maana naelewa sana kwamba Kama Card number iko compromised basi utajikuta unapigwa na kitu kizito kabisa.

Ushauri wangu.

Kwanza Andika Barua nzito kwenda TIGO Kisha nenda TCRA ukafungue Malalamiko kwenye dawati la consumers protection kisha andaa kabisa mkakati wa kwenda Mahakamani.Ukwaletea Hizo mada hizo hakika watakupa pesa yako na Bakshishi Juu.
 
Niliwahi kulipia tkt ya ndege kwa kutumia hii Tigo Mastercard makato yalikuwa juu saana kupiga simu naambiwa charge ni percent kadhaa ya muamala. Voda wako vizuri zaidi kwenye virtual cards
 
Voda tunawasifia wako vizuri kwenye card kutofautisha na account ya mpesa ila kwenye customer care ukipata changamoto ni sifuri kabisa ..yaani hawaelewei kabisaaaaaa iwe kuongea hata Ile Voda chat utaambiwa utajibiwa after 24 hours. Ni vyema BOT ikaingilia kati kuliangalia hili..maana Kuna miss communication kubwa Sana baina mlipwaji na mtoa kadi..kila mtu anamtupia madai mteja.
Mfano supply anashindwa kupokea pesa anakwambia wasiliana na card provider ,ukienda Kwa card provide hajui hapo ni tatizo kubwa
 
NItakupa sababu mbili muhimu kwanini usitumie kadi yako ya TIGO mastercard kununua vitu online.

1. Hii kadi wameunganisha mojamoja na akaunti ya Tigopesa, hamna control ambayo mteja unakua nayo kudhibiti kiwango cha juu ya muamala pale ambapo akaunti yako inakiasi cha kutosha kufanya muamala zaidi ya mmoja.

2. Accountability, support ya Tigopesa ipo very poor, haijibu kwa wakati na haitaki kubeba majukumu ya kutatua matatizo pale yatakapotokea. Ili uwezekuelewa vizuri ngoja nikupe mapito yangu ya hivi karibuni.

Kisa: Mwezi uliyopita nilinunua application kupita MICROSOFT Store kwa kiasi cha $15, inaonekana kulikua na tatizo kwenye mfumo wa malipo na kupelekea muamala ya $15 kufanyika mara nne, tena ingewezekana kufanyika mara nyingi zaidi kama nisingewahi kuizuia kadi.

Sasa Microsoft wanasema kati ya miamala minne ni mmoja tu ambao umewafikia, nawakashauri ni wasiliane na benki yangu kuhusu miamala mitatu ambayo haikufanikiwa na wakanipa reference namba 3.

Sasa nimewasiliana na hawa ndugu zangu Tigo kwa njia ya simu kisa kwenda kwenye moja ya duka lao, wanakazana kuwa miamala yote minne ilienda ("Posted"), wamegoma kusoma barua pepe niliyotumiwa kutoka Microsoft, wamegoma mimi kuwaunganisha ("CC") katika barua pepe ambayo nimetumiwa na Microsoft. Pia wamenipa printout ya hizo transaction lakini wamegoma kutumia makaratasi ambayo yapo branded, yani kwa lugha nyepesi wameprint tables kwenye makaratasi ya kawaida ambapo hamna details ambazo zinasema kilichoprintiwa kimetoka wapi. Sasa wanategemea mimi nishare haya makaratasi na hawa wajamaa, dah.

Kwa ufupi hili ni funzo nimelipata, na imani na wewe utakua umejifunza kitu kipya.

N.B: Kunamdau anaweza sema ningeamisha hela kwenda namba kabla sijafanya huo muamala.
1. Hii sio practical kwa sababu itahitaji niwe na namba zaidi ya moja, pia kila unapoamisha kuna makato yasiyo na kichwa wala mguu.
2. Baada ya kuamisha unaweza kupokea muamala kutoka kwa mtu na kuifanya accounti yako kuwa na hela za ziada.
3. Kama ni subscription, huu ujinga unaweza kufanyika usiku wakati umelala, na kujikuta unaamka asubuhi message za Tigo pesa zinaongozana.




Asante
Hii imenikuta mwezi wa 9, nililipia bidhaa aliexpress kupitia Tigo Mastercard. Hela ilikatwa lakini Aliexpress wakasema malipo hayajafika. Kuwasiliana na Tigo hawakuwa na majibu ya kueleweka. Nashauri ni bora zaidi manunuzi ya mtandaoni yafanyike kwa njia ya Visa au Mastercard zinazotolewa na Bank.
 
Na Mimi imenitokea juzi kupitia tigo master card, ni majizi sana. Ninashauri Mtanzania mwenzangu unaesikia hii kauli acha kabisa kutumia Master card za tigo, Kuna siku utanishukuru. Yani hawafai hata kulumangia.
 
Back
Top Bottom