Usinunue vitu online kwa kutipia TIGO MASTERCARD!

Mkuu kama ulisubscribe kwenye App au service ni ngumu sana hata kwa card provider wengine kuissue reversal.
Changamoto nayoiona kwa Tigo na Airtel ni ujinga wao wakuchanganya card na wallet za Tigopesa au Airtel Money kwa hiyo mteja huna control ni kiasi gani kiwepo kwenye card.
 
Mkuu ni kweli unachokisema, kuna uwezekano ni kweli wengi hatujui hizi sheria lakini pia nafikiri aina ya miamala tunayopigwa haitupi motisha ya kutumia hela zaidi kwenye kuajili wanasheria na kutumia muda mahakamani.
Pia ukijaukasoma Terms and Conditions documents zao, zimekaa kwa design ya kuwafanya washinde hizi kesi
 
Shida ukilalamikia kwao kule wanasema fanya mawasiliano na mtandao wako ulioko huko Tanzania kwa kweli tunapigwa mpaka tunapigika sio sawa unapoteza hela nyingi na tigo wanafeli kuzichukua kwaajili yako, biashara za mtandao ni risk sana kwasisi watanzania hatuna sehemu ya kufanya tracking pesa ilipopotelea, na mitandao haisaidii kabisa
 
Mkuu pole sana kwa hii changamoto, na mimi nimekuja kujifunza kuwa hawa watu hawajali na mara nyingi hawataki kubeba jukumu la kumsaidia mteja wao hata kutosupport ya documents pia ni shida kwao.
Sheria zipo za kumlinda mteja lakini imekua ni kawaida kumuachia mteja ujipambanie ulichokipoteza huku unakuja kufeli maana huna njia nyingi za ku access ulichopoteza kama wao walio kuwa kwenye system
 
Hawa toka niliponunua simu moja ya duka lao na kuahidiwa ofa, lakini muda ukifika kupata hiyo ofa sasa mtihani.
Wahuni sana.
 
Pole mkuu, njoo mpesa Visa....MPESA VISA ndio mpango mzima yaani unaweka pesa kiwango unachotaka kulipia kwenye card ya Visa kwa hizo subscription au manunuzi, inatokea errors kukata haiendi kukata kwenye mpesa yako coz haingiliiani hata kidogo .wewe ndio mwenye permission ya kuweka fedha kwenye card au kutoa kwenye card.
 
Mkuu mimi nimefanya hizi electronic transaction kwa zaidiya miaka 15 sasa.Na nitakwambia kwamba kwa uzoefu wangu mifumo yote Tanzania ambayo inahusika na malipo kwa kupitia VISA na Master Card ni Majanga.Hii ni Kuanzia mifumo ya Mabenki,Mifumo ya virtual Card n.k.

Nimefanya miamala na benki kadhaa na mitandao yote ya VODA,TIGO na AIRTEL.

Kwanza kabisa inapokuja swala la technical au operational support wako chini kabisa yaani ni zero hawaelewi hata product yao wenyewe wala kuiamini.

Pili kunapokuwa na Transaction duplicates pesa haiweza kurudishwa kwenye akaunti yako.So mimi Huwa nahakikisha kwamba ninapotaka kufanya Muamala wa kulipa kwa kadi basi akaunti yangu inakuwa nakile kiasi tu ambacho kinatkiwa kulipwa BASI,Sizidishi hata thumni.

Pili huwa sipendi sana kutumia SAME bank account kwa ajili ya normal transaction kwenye hizi online transactions maana naelewa sana kwamba Kama Card number iko compromised basi utajikuta unapigwa na kitu kizito kabisa.

Ushauri wangu.

Kwanza Andika Barua nzito kwenda TIGO Kisha nenda TCRA ukafungue Malalamiko kwenye dawati la consumers protection kisha andaa kabisa mkakati wa kwenda Mahakamani.Ukwaletea Hizo mada hizo hakika watakupa pesa yako na Bakshishi Juu.
 
Niliwahi kulipia tkt ya ndege kwa kutumia hii Tigo Mastercard makato yalikuwa juu saana kupiga simu naambiwa charge ni percent kadhaa ya muamala. Voda wako vizuri zaidi kwenye virtual cards
 
Voda tunawasifia wako vizuri kwenye card kutofautisha na account ya mpesa ila kwenye customer care ukipata changamoto ni sifuri kabisa ..yaani hawaelewei kabisaaaaaa iwe kuongea hata Ile Voda chat utaambiwa utajibiwa after 24 hours. Ni vyema BOT ikaingilia kati kuliangalia hili..maana Kuna miss communication kubwa Sana baina mlipwaji na mtoa kadi..kila mtu anamtupia madai mteja.
Mfano supply anashindwa kupokea pesa anakwambia wasiliana na card provider ,ukienda Kwa card provide hajui hapo ni tatizo kubwa
 
Hii imenikuta mwezi wa 9, nililipia bidhaa aliexpress kupitia Tigo Mastercard. Hela ilikatwa lakini Aliexpress wakasema malipo hayajafika. Kuwasiliana na Tigo hawakuwa na majibu ya kueleweka. Nashauri ni bora zaidi manunuzi ya mtandaoni yafanyike kwa njia ya Visa au Mastercard zinazotolewa na Bank.
 
Na Mimi imenitokea juzi kupitia tigo master card, ni majizi sana. Ninashauri Mtanzania mwenzangu unaesikia hii kauli acha kabisa kutumia Master card za tigo, Kuna siku utanishukuru. Yani hawafai hata kulumangia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…