Usinunue vitu online kwa kutipia TIGO MASTERCARD!

 
Master card tigo niwizi mtupu nimerudishiwa pesa zimepotelea hewani ,
 
ahsante kwa taarifa, nimekuwa nikitumia vodacoma master card sikuwahi kupata changamoto nilijua tigo wapo vizuri
 
Wakuu tujifunze kutumia mamlaka zinazosimamia, kwa mfano hapo ni kuandika email nzuri ya malalamiko yenye ushahidi ns kutuma TCRA na BOT utaona wenyewe watakutafuta na pesa wafakurudishia

Sent from my SM-A037F using JamiiForums mobile app
 
Kwa Tz cross border payment iwe withdrawal issues au deposit issue hawatoi msaada

Kuna ela niliipwa from asia voda na Tigo wote hawakunpa ushirikiano na hawaelew tuu hAta watoa huduma wao.
 
Habari mkuu, nmepitia huu uzi, na mimi ni muhanga wa ili jambo aise! Nina siku ya nne tigo wananizungusha toka nifanye malipo ya Tigopesa master card kwenda High commission of canada, pesa yangu imekatawa kwenye tigo laki tatu na tisini elfu, uku nakolipia huduma sijapata malipo wanasema hawakupokea, yalikua declined. Yaan nina hasira sijui ata pa kuanza kudai ela yang, nmeenda mpaka tigo makumbusho wananipa hadithi za kua ela zmepokelewa wakat kiuhalisia hapana hazikupokelewa.
 
Tigo ukiripoti matatizo hawashughulikii kwa haraka,nilishatoa Tigo kwenda Voda mpk leo haijafika,ukiwapigia wanakuambia kuna shida subiri masaa 24,yanapita tena,unawauliza vip,unaambiwa subiri tena

Mpk leo haijafika nimeamua kupotezea
 
Kwa Tz cross border payment iwe withdrawal issues au deposit issue hawatoi msaada

Kuna ela niliipwa from asia voda na Tigo wote hawakunpa ushirikiano na hawaelew tuu hAta watoa huduma wao.
Wanakuambia subiri masaa 24 ,inapita wiki

Wako nyuma na teknolojia
 
Mimi nashauri wahanga ambao tuna matatizo kama haya hususani kwa Tigopesa mastercard, tujioin kwa pamoja tupeleke malalamiko TCRA hata kwa njia ya email tu as tukusanye kesi zote za vielelezo pamoja then tutume TCRA kama email moja ili tupate way forward.

Nasema haya sababu nilijua mimi ni muhanga peke yangu na nilikausha baada ya kukosa msaada mwaka jana, lakini kumbe inatokea kwa watu wengi na tunabaki kugugumia tu kwa hela zetu wenyewe tulizipata kwa tabu sana, hata kama ni pesa kidogo bado ni Jukumu la Tigo kuwajibika kwa sisi customers wao.

Mwaka jana nilifanya malipo kwenye Apple store kiasi cha 250,000 ambayo ilikatwa vizuri kabisa bila shida, next day ikakatwa tena 250,000 kwa mara ya pili kwenda apple, nilicheki apple nikakuta kweli kuna invoice imelipiwa mara mbili. Nilicommunicate na apple (as ujuavyo wenzetu wazungu hawana ushamba wa kiafrica wa urasimu wa kipuuzi), walinijibu ndani ya 24hrs kuwa pesa zangu zitarudishwa kwenye card niliyolipia.

After a day wakanitumia email ya proof kuwa wamerudisha hela kwangu ikiwa na details zote kama zilivyotumika wakati nalipia. Nikawasiliana na Tigo na kuwaelezea wakasema mchakato huo huwa unachukua muda hadi hela isome Kwenye account yangu.

Aisee nilisubiri for two months kimya, kuwatafuta Tigo tena wakasema bado niendelee kusubiri pesa kama hiyo inapitia channels nyingi sana hadi kufika kwao, Wazee muda huo huo ukumbuke kadi zao sio permanent ni za siku 90 then inaexpire alafu niko zaidi ya two month wanasema nisubiri. Ikafika muda card ikaexpire na sikuona shida sababu wallet na Tigopesa ziko linked direct (sio kama voda).

After six months baada ya kufuatilia tena Tigo, wakaniambia mbona nimechelewa sana kutoa taarifa ishapita miezi mingi, uzuri wakati natoa taarifa ya kwanza nilihifadhi reference number ambayo nilikua kila ninapofuatilia nawatajia, nilipowatajia kipindi hiki wakasema kesi ya zamani sana na reference number haiwezi kuwepo kwa system.

Ilifika mahali nikachoka sana usumbufu wa kila siku na unaenda kutia huruma kama unaomba msaada vile while pesa ni zangu, uende kunyenyeke watu ukatie tie huruma ofisi zao ndo warespond hii haikuwa sawa kwangu, nilipiga chini na nikaacha kufuatilia lile swala mpaka leo.

Kitendo cha kuona hili swala kumbe linawakumba watu wengi, naona si vyema kuacha liende hivhivi aisee, itabidi tufanye namna.
 
Pole sana, customer service centre hawawezi kukusaidia, labda kama wanachokitengo kinachohusika na tigo pesa direct, mm nadhani wanashindwa kukusaidia kwakuwa hawana ushahidi wa moja kwa moja unaoonyesha pesa kuingia kwenye mifumo yao na kwamba ipo huko ina ning'inia hewani, kituo kikuu cha watoa huduma wa tigo ndio wanaweza kukusaidia ishu ya refund

Kingine ni uvivu wa watoa huduma wengi linapokuja jambo kama hilo la pesa kutoka kimakosa kisha ihitajike kurudishwa, labda kwakuwa process zake kuna muda ni complicated sana...

Kama Microsoft hawajapata hiyo miamala mingine, basi tigo pesa wawajibike kukurudishia pesa yako...

Lakini huenda ikarudi baada ya muda fulani kwenye akaunti yako kama itaonyesha hazikufanikiwa

M pesa wao huwa zinarudi kama muamala haujafanikiwa
 
Achana na hao wanaokaa ftont Desk hapo tafuta mtu wa kitengo ashughulikie suala lako .. ingia mlango wowote hapo mpaka wakupe pesa yako.
Acha uwoga
 
Achana na hao wanaokaa ftont Desk hapo tafuta mtu wa kitengo ashughulikie suala lako .. ingia mlango wowote hapo mpaka wakupe pesa yako.
Acha uwoga
Ya kwangu ilikatwa Airtel. Kiasi cha laki nne na ushee. Nilienda straight kwa Manager pale makao makuu. Sio issue za vibandani au dirishani hizi. Na imeisharudishwa
 
Pole mkuu. Apo unacho Takiwa kufanya, ni kuifanya account yako ya benk like nmb, NBC,crdb etc kuwa na uwezo wa kufanya manunuzi online.

Unaifanya account yako ya benk ina kuwa wallet.
Mfano nmb Visa,rcdb master card, NBC Master card.

Alafu SS unakuja Ku Link na PayPal account yako.

Hii itatusaidia kufanya manunuzi duniani bila kurudishiwa pesa Zako.

Coz hizi wallet ,tigo Visa, MPESA master card etc hizi šŸ‘ˆhazitambuliki kwenye dunia ya Kwanza, Ndio maana pesa zenu zinarudishwa.

Tumieni PayPal account alafu Una Link na account wallet zenu za benk,hii itatusaidia kufanya miamala mpaka wa 100,000 USD dollars Kwa mkupuo mmoja
 
Hiyo ninpolice case hapo motandao haihusiki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…