Bonge la Uzi....Vijana inabidi tuwe na fikra za namna hii.
Mleta mada hajasema watu waibe au wafanye uharifu, amesema tafuta hela kwa udi na uvumba na usiogope ku-take risk.
Kuvuka border, kuvuka maji au kuzamia pits za migodini sio uharifu...huo ni ushujaa wazee.
Uharifu ni kuiba mali za umma ukiwa kiongozi, matumizi mabaya ya madaraka, tozo za ajabu ajabu, kuiba kura nk.
Vijana tukaze pamoja na changamoto nyingi lakini as long as tunapumua, tuna nafasi ya kutoboa....watu wanasema miaka 40 ni ya kuanza bata, utafutaji na muda wa kutoboa hatulingani mazee...Mi ntatafuta hadi siku nakata pumzi...maana wapo waliotoboa na miaka 40, 50, 60 mpaka 90 huko.
Vijana wanaogopa kuacha familia na kwenda hata mikoa ya mbali kutafuta hela. Sio lazima kwenda mbali ila pale inapobidi usisite kuliamsha.
Heshima kwa vijana wote tunao-hustle daily na tunaamini tutatoboa..Mwenyezi Mungu atusimamie.