M bwa mwitu na binadamu ni marafiki sana,nakumbuka miaka ya 90 tulienda na mjomba wangu polini kulina asali,tukiwa kambini aliingia Simba ghafula akaja akakaa miguuni kwa mjomba,sisi na wwnzangu tukiwa wasoho lakini tulikuwa tumaliza darasa la 7 tukataka kukimbia,mjomba akasema msikimbilie nje pandeni vitandani kwenu maana vitanfa tulikuwa tumetengeneza vya juu tulifunga kwa kamba kwaabanzi ya mbao, akatuambia huyu Simba atakuwa amekimbizwa na mbwa mwitu,kwa hiyo msiogope Simba hawezi kutudhulu maana hapa Simba anaona ndiyo sehemu salama ya kunusulu maisha yake,sababu mbwa mwitu anamuogopa binadamu sana,
Tulifanya hivyo aiai tukiwa juu ya vitanfa vyetu tukawa tuna mwangalia mjomba akiwa na Simba,baada ya muda mjomba akatuambia anzeni kutelwmka mmoja moja ukitoka nje tafuteni miti mpande juu kila mtu apanse mti wake,kweli tulifanya hivyo,hatimae mjomba nae alifanikiwa kujinasua mikononi mwa simba naye akatoka nje akapanfa juu ya kambi /kibanda maana juu tulikuwa tumekieseka kwa magome ya miti na tukajaza udongo kwa juu,
Tukiwa juu ya miti na mjomba akiwa juu ya kambi tuliwaona mnwa mwitu wakiizingika kambi lakini walikuwa wanaogopa kuingia ndani wakijua ndani ya kambi kinawatu wamebakia, ilikuwa saa sana mchana,tuliendelea kukaa juu ya miti hadi saa moja na nusu jioni giza likiwa limeingia ndipo kwa mbali tulimuona mjomba akikoka Moto wa mahogo nje,akatuambia telemkeni Simba amesha enda maana hata Simba anajua giza likianza mbwa mwitu lazima aende kulala huwa hawindi usiku anapumzika,kweli tilitelemka na tukaingia kambini
Mbwa mwitu Hana mashala kwa binadamu anamuogopa Sana.