Hapo akikutana na mimi ambaye naangalia tu bila kuelewa kitu basi ananifanya kama sehemu yake ya kutolea mafunzo. "Usione hivi, nikiwa serious na JavaScript, Python na Hii JQuery kwa huu mwaka nakuhakikishia mwakani napiga project hata mbili tu kila moja 1.5M hapo navuta 3.0M fasta" hii kauli inasemwa kwa nguvu.
"Sasa unajifunzaje?" ukimuuliza hivi anajibu " Ni rahisi tu, kuna website inaitwa w3school, kuna muda unakopi codes alafu unazibadilisha kidogo tu kitu himo. Alafu nimekumbuka ngoja nitumie Sublime naona hii VS Code inaanza kuganda, code nilizoweka nzito sana [emoji23][emoji23][emoji23]".
Unaweza kupasuka hata mbavu ila kutokana na ukaribu wenu na ushkaji unajikuta unakausha tu na kujipa moyo kwamba utachekea nje [emoji23][emoji23][emoji23]