Usiombe ukutane na mwanafunzi wa IT mwaka wa kwanza

Usiombe ukutane na mwanafunzi wa IT mwaka wa kwanza

We utakua sio mtanzania ,na kama ni mtanzania basi umewahi kuishi nje ya Tanzania, mawaza haya ni mageni kwa mtanzania
😁😁 hapana mkuu, Mimi mbongo Pure Ila nipo tu kwenye group linaloshindana na mifumo iliyopo "Challenging the existing norms" ,
shukrani kwa compliment brother 🙏🏽🙏🏽🙏🏽
 
Kuna habari fulani ilienea mitandaoni na kuonekana imewapa credit ya kitaalamu wanafunzi wa Chuo kikuu cha Tumaini Iringa kwa kudukua na kujilipia karo. Japo walichokifanya ni kosa la jinai na kinyume na maadili ya taaluma kwa upande mmoja lakini kwa upande mwingine kuibua hisia ya kuonyesha hao vijana wako vizuri katika nyanja ya tekinolojia ya habari IT!

Kabla ya kuendelea ebu tuangalie tofauti ya Hacker na Social engineer

(Hacker): Mdukuzi ni mtu aliyebobea katika teknolojia ya habari ambaye hutumia maarifa yake ya kiufundi kufikia lengo au kushinda kikwazo, ndani ya mfumo wa kompyuta kwa njia zisizo za kawaida.

(Social Engineering): (katika muktadha wa usalama wa habari) ni matumizi ya udanganyifu ili kuwashawishi watu binafsi kufichua maelezo ya siri au ya kibinafsi ambayo yanaweza kutumika kwa madhumuni ya ulaghai.

Kwa ufupi "hacker" hutumia tekinologia kupenya kwenye mfumo; wakati "social engineer" hutumia udhaifu wa kibinadamu kuingia kwenye mfumo.

Kwa mfano: kama utamvizia mfanyakazi akiwa kwenye kompyuta yake anaingiza majina ya waliolipa karo na kiwango alicholipa karo, ukamvizia labda kaenda chooni, au ikatokea ukapata nywila "password" kutokana na ukaribu wako na yeye kutokana na kuaminika kwako nayeye ukachukulia fursa ya udhaifu wake ukaingia na kuongeza au kubadili isivyo taarifa kwenye computer, hiyo tunaita "udukuzi (uhandisi) wa kijamii" kwa sababu uhandisi wa kijamii hutumia upotoshaji wa kisaikolojia na kutumia makosa au udhaifu wa kibinadamu badala ya udhaifu wa kiufundi au wa mfumo wa dijitali, wakati mwingine huitwa 'hacking ya kibinadamu. '

Hao vijana walifanya hayo katika mazingira ambayo wanamwingiliano wa moja kwa moja wa walimu na wafanyakazi na miundombinu ya tehama na walikuwa rahisi kupata credentials au kukutana moja kwa moja na miundombinu ya mtandao (network) au nyaraka za chuo na sio kutumia utaalam wa tekinolojia ya habari (IT).
Kama wanabisha ebu nenda mkadukue benki au jiongezee salio au hela kwenye mitandao ya simu!

Watanzania tusitumie uaminifu tunaoaminiwa na waliotuweka hapo kuiba na kujiona wajanja. Kama unajiona una maarifa anzisha taasisi yako kivyako na onyesha maujanja yako nakuhakikishia utatoboa!

Sio umeajiliwa unakwiba kwa mwajiri alafu unakuja mtaani na kujionyesha wewe ni mjanja! Au unasaini mikataba ya ulaghai kama wa DP WORLD unapewa mlungula alafu unatamba wewe mjanja na kuwaona waliomtaani mazuzu! Hii haijakaa sawa!
 
Aisee ikitokea umekutana na mwanafunzi wa IT mwaka wa kwanza wengi ni much know.
Niko na dogo hapa kamaliza mwaka wa kwanza anasoma masuala ya security yani yeye kila kitu anasema anaweza hack iwe gmail, wi-fi, mitandoa ya simu atumie net bure, anakwambia gmail haiko secure, instagram anaweza kuhack.
Basi mimi namchora tu na kumkubalia.
Kila anachoona kwenye computer anasema usitúmie hicho tumia hiki ananitajia softwares ambazo si maarufu ili mradi vurugu tu.
Hapa kaniambia nisitumie chatgpt haina performance nzuri nitumie sijui flick.

Huyo bado hana idea how real world works. Akisha rudi mtaani ataelewa real life halihitaji mbwembwe
 
Huyo dogo ni potential mwambie aihack dunia tuone yaliyomo.
 
Aisee ikitokea umekutana na mwanafunzi wa IT mwaka wa kwanza wengi ni much know.
Niko na dogo hapa kamaliza mwaka wa kwanza anasoma masuala ya security yani yeye kila kitu anasema anaweza hack iwe gmail, wi-fi, mitandoa ya simu atumie net bure, anakwambia gmail haiko secure, instagram anaweza kuhack.
Basi mimi namchora tu na kumkubalia.
Kila anachoona kwenye computer anasema usitúmie hicho tumia hiki ananitajia softwares ambazo si maarufu ili mradi vurugu tu.
Hapa kaniambia nisitumie chatgpt haina performance nzuri nitumie sijui flick.
Kuna huyo mmoja nilikutana naye mahali akaanza kujitia ujuaji, ilibidi niwe namkubalia kila anachosema na akujua kuwa anayemfundisha ni expert aliyemzidi experience ya zaidi miaka kumi.
 
Ngoja amalize theory chuo aje field mtaani ukweli utajulikana
 
Back
Top Bottom