Usiombe uumwe USA

Usiombe uumwe USA

kila nikiwaza kwenda wanakokuita ulaya au marekani kutafuta maisha naona ni uzushi mtupu.....
unakuta mtu ametoka bongo 10yrs ago lakini maisha anayoishi huko ya kubahatisha hata bahati mbaya akifa anazikwa na serikali....
Nadhani maisha yako wewe Natalia yanasomeka! hao wanachangisha wapate kuishi waambie waje tukalime mihogo na matikiti maji kimanzichana mashamba bwerereeeeeeeeeeee
 
Natalia umefulia tu rudi bongo uje kulima viazi mabwepande!!! Mbona watu tunawajua wapo huko manhanhe bruklin uptown bmg londoni wanakimba mbaya kama stoper rhymes wa faya atown.
 
huku dawa zinatembezwa madumu kwa madumu zinatibu magonjwa 800 raha tupu

huyo mtoa mada si mwelevu wa maisha ya DUNIAN na utakuta mtu anae Ongea ivyo yy.KAPELEKWA NA DADA NA SHEMEJI ZAKE WAPO HAPO KALIBU..NDIO MAAANA ANAMUONA HUYO MKENYA KAMA NI MJINGA FULANI kuugua nikitu cha kawaida duniani kote hata hapa BONGO watu huenda kwa Waganga au kula MWAOLUBAINI ni ukosefu wa kipato sio wanapenda hapa wengi wanategemeana HUKO SIO IVYO nakusii MTOA MADA OGOPA KAULI YAKO
 
........Tazama daraja la kigamboni tulivyotapeliwa. Huwezi kujenga daraja kama hili ili yapishane magari mawili. hapo ni lazima yawe yanapisha magari manne. Halafu daraja hili ni jembamba sana haliwezi kukidhi haja ya wingi wa magari tanzania. hapa New York city, kuna daraja la brocklyn linalounganisha manhatan na broklyn. lilijengwa mwaka 1958 likiruhusu magari nane kupisha. Yaani maane upande mmoja na manne upande mwenginewe. Halijawahi kuwa kero tangia mwaka 1958. sasa wewe angalia hilo la kigamboni.

Limeanza kuwa kero kabla ya hata kumalizika. halafu sijaona njia za wapita kwa miguu zikiwa pana au pengine hazipo. unaona hatari yetu sisi wabongo. Upo tayari kuiba pesa bila kujali madhara yatakayotokana na wizi wako. Hapo magari yakigongana basi abilia wote watazama kirahisi kwa wembamba wa barabara.


Kuhusu daraja la Kigamboni nakataa, lile uliloliona ni temporary tu,daraja lenyewe litakuwa na uwezo wa kupitisha magari manne kama sikosei, njia ya waenda kwa miguu, baiskeli. Kuhusi hilo ondoa mashaka hata wao wenyewe walisema msije kusema hili ndiyo dalaja lenyewe.
 
......huku kama umejikata, kutoa jino, operation ndogo, kukamuliwa jipu, kuna dawa za pain killer, ambazo unapewa kufuta maumivu. Utamu wa dawa hizo na raha yake, ni mara tano ya kulala na msichana. Je bongo dawa hizo zipo kweli ?

Tok nizaliwe sijawahi kisikia dawa kama hiyo ambayo ukimeza utamu wake ni mara tano ya kupiga bao!!!
 
Kuna mdada mmoja mkenya aliumwa 2 weeks saa hizi nyumba hajalipa gari umeme na maji an simu .na kazi Hana Leo kuna kikao cha kumchangia.maisha gani hayo siheri Arudi Kenya tu .unaumwa week 2 tu unakutwa na drama lote hilo.kuishi paycheck to paycheck no heri urudi bongo

Ule mpango wa Obama wa Health insurance hauwahusu wageni? kama ni hivo warudi tu!
 
Wapi unaweza kuomba kuumwa?

Wengine wanaweza kukwambia bora huko USA kuna habari ya mtu asiye na bima ya afya kuweza kuhudumiwa na hata ukikosa kazi kuna welfare system na ma unemployment benefit kibao, zaidi ya hapo huwezi kukosa kubangaiza hata ku deliver magazeti.

Hapa naona kuna habari ya aina ya kazi hajasemwa vilivyo. Kama mtu huna makaratasi hata mwajiri hawezi kuzingatia sheria zinazoruhusu mtu kuumwa bila kufukuzwa kazi.

Sasa labda tuongelee kufanya kazi bila makaratasi zaidi kuliko kuumwa per se.
 
Marekani na Ulaya uwnde kimpangilio, ni bora zaidi kuliko kuishi bongo! msijiliwaze huo ndio ukweli
 
Tumeshazoea dawa za wamasai na Loliondo njooni huku tuko Paradiso
 
karibuni huku kama una ka kitambi flani unajifanya afisa usalama na kabastola chako feki unapiga hela za kutosha, jioni twanga pepeta pale mango gdn na unaitwa pendeshee, karibuni home:glasses-nerdy:

Hahhahahhaaaa
Umeshanipa trick
 
Usipoteze diesel nyingi tango kujieleza,maisha popote tu.hata ukirudi bongo bado lazima ufanye kazi ufanye kazi upate hela,iwe biashara au kuajiriwa.we unafikiri marekani kungekuwa hovyo vasco da gama na mafisadi wenzake wangekuwa wanachezea kodi kwenda huko kila siku?

Leo hii usa wakitangaza kwenda usa huihitaji viza,nafikiri tz itabaki tupu.





nDIO MAANA mAREKANI NI nCHI TAJIRI KUPITA ZOTE DUNIANI. nA sISI NI MASIKINI KUPITA NCHI ZOTE ZILIZOFUATA UKOMUNISTI. Kulipa nyumba na bili za simu, maji, umeme ni lazima kwa kila mpangaji. Tena hakuna excuse. Ila ukiwa na matatizo ya kuachishwa kazi na unakabiliwa na matatizo mengi kimaisha , kuna mahali kwingi sana sana kwenda kupata misaada. Hapa New York city,, kuna sehemu inaitwa workforce, hapo unapewa food stamp na kucollect unemployment wages kwa siku kadhaa. Hakuna shida kabisaa wala Njaa hapa marekani. labda huyo dada alikuwa kazini wiki moja tuu na hakumaliza three months probabation.

wewe usiombe kuishi marekani. Mwarabu wa saudi, Iraq, Bahrain, UAE na Libya, anafanya bahati nasibu ya Gree card masaa 24 ili aje aishi marekani ingawa nchi zao huzalisha pesa utafikiria wanatungua na makota mtini.

Hakuna mtu asiyependa kurudi tanzania. Ila upatikanaji wa kazi ni finyu na madawa ya kujitibu ni fake sana, je hili linavutia kweli kuja tanzania?huku kama umejikata, kutoa jino, operation ndogo, kukamuliwa jipu, kuna dawa za pain killer, ambazo unapewa kufuta maumivu. Utamu wa dawa hizo na raha yake, ni mara tano ya kulala na msichana. Je bongo dawa hizo zipo kweli ? na kama zipo si zitakuwa fake. mimi nemishi dar, sasa nataka nikirudi, nikaishi Sumbawanga au katavi, je ni raisi kupata kazi huko au ndo nilazimike kuja ishi dar tena?
 
Jamani jamani tusidanganyane bongo maisha bado duni sana yaani sana zaidi ya tunavyofikiria, wanaotetea kuwa bongo ni bora kuliko Europe/USA basi hawana exposure ya kutosha, tembeeni duniani muone jinsi TZ ilivyo duni. Nilikuja bongo mwanzoni mwa mwaka huu kidogo nilie machozi, watu woote utadhani wagonjwa au mateja flani kwa kuzubaa na kupauka. Wamepoteza matumaini wanaishi bora liende. Kuna wachache ambao wameiba iba serikalini au wanafanya biashara haramu (hawalipi kodi au wanauza madawa) ndio walau wanaishi life standard ya maskini wa europe. Kuna mshkaji nilisoma nae nilipokeja bongo nilimkuta na utajiri wa kutisha wakati yeye ni afisa wa kawaida serikalini, hivi niongeapo ana kesi ya kujibu kwani halmashauri aliyokuwa anafanyia kazi , zaidi a billion 2 hazijulikani zilipo na yeye ndo muhusika mkuu this means anaweza kufungwa, kazi kesha fukuzwa, ni maisha gani haya ya kugeuka jambazi ili utoke? Europe maisha raha mustarehe, no stress za kesho nakula nini, huibi ili ujenge nyumba, una save from your clean money sio magendo, kuna life security nk.

One thing which makes TZ special to me and huwa na miss sana huku huwezi pata ni...NYAMA CHOMA, otherwise bongo life msoto saana, tusidanganyane :becky:
 
Kuishi uropa siyo kuukata hasa kwa wale waliokwenda kule bila mipangilio ya uhakika. Heri warejee makwao wakapige nguna maana hakuna kitu kinachouma kuona watu wanavyodhalilika hasa akifa mmojawapo kwa kuchangishana.

Kwani USA ni uropa aka Europe!
 
wanang'ang'ania kuona maghorofa....majumbani wakisimulia BT yupo marekani full ujiko

Maghorofa hata Dar yamejaa tena yanachipuka kama uyoga kila siku japokuwa wakati wa masika tunalia na mafuriko ya mitaro!
Hizo sifa za kijinga za 'binti yupo marekani' ndio huwa sizielewi kabisaaaaaaa! Kuna mama aliishia kuuza assets ili kutumia vijana pesa za matumizi majuu! Watu wakubwa wazima kusoma hawasomi kazi za maana hawana wamemfilisi mama yao kwa woga wa kurudi bongo!
 
Kama husomi na huna kazi ya maana unang'ang'ania nje kwa sababu Bongo kama huna elimu na huna kazi nzuri maana yake unasukuma mkokoteni Tabata Dampo... bora kulea wazee mbele huko

Kuliko nikashike shike vizee nje bora nikakaange samaki ferry!
 
Tanzania kuna matibabu gani ya maana? Tanzania watu hawaishi kwa mashaka na kubahatisha? Ikija kwenye huduma za afya Tanzania iko nyuma vibaya mno. Watanzania wangapi wanakufa vifo kwa ajili ya magonjwa yanayoweza kuepukika? Ni wengi mno! Healthcare system ya Tanzania ni janga.

Katika hilo la health system ya Tanzania wala sikubishii sana mkuu. Suala hapa ni je, kuna haja gani ya kung'ang'ania kuishi marekani au ulaya kama ukiumwa 2 weeks tu basi inalazimu marafiki wakuchangie ili uweze kulipa kodi na bills nyingine za kawaida? Huko marekani na ulaya kwenu mie nafurahia kuja muda mfupi na kurudi zangu bongo. Pamoja na shida tulizonazo bongo, kwa ujumla kuna chembechembe za raha!
 
Katika hilo la health system ya Tanzania wala sikubishii sana mkuu. Suala hapa ni je, kuna haja gani ya kung'ang'ania kuishi marekani au ulaya kama ukiumwa 2 weeks tu basi inalazimu marafiki wakuchangie ili uweze kulipa kodi na bills nyingine za kawaida? Huko marekani na ulaya kwenu mie nafurahia kuja muda mfupi na kurudi zangu bongo. Pamoja na shida tulizonazo bongo, kwa ujumla kuna chembechembe za raha!

Hahaa wewe Mwajei wewe! Wangapi bongo wanakufa kwa kushindwa kumudu gharama za matibabu bana? Watu hao utawaambia nini sasa? Msitake kuipamba bongo ionekane kama vile ina unafuu wa maisha wakati hali ni ngumu beyond belief! Bongo hakuna unafuu wowote ule katika sekta yoyote ile.
 
Mlioenda wote huko usa kwa nia ya kutafuta kazi ni wavivu wa kufikiri. mbona watu hapo bongo wanatengeneza pesa za kufa mtu. Fikiria mtu ananunua dagaa wa mwanza sh. 2000 kg. Anakaanga na kuweka viungo na kupack kwenye vitray kwa kila robo kg. sh2000 na anauza mpaka nje. Ok ni mashamba mangap mumeyaachaa eti mnaenda kuwa mayaya, wakat huku watu wako pori wananunua mazao na kusafirisha nje na majumba ya kufa mtu.njoon mtembee huku muone waliojitoa kufanya kazi nzito kama mnazofanya nyinyi huKo walivotoka kimaisha. Nyie kaeni mtazeeka mayaya shauri yenu
 
Kuliko nikashike shike vizee nje bora nikakaange samaki ferry!

Kazi ni kazi tu ili mradi inakupatia riziki yako kiuhalali. Kuanza kuponda ajira za wengine ni dalili inayo reveal mapungufu ya nafsi. Sasa sijui kuna ubaya gani kuwa na kazi ya kuwahudumia wazee hadi wewe uonyeshe dharau juu yake!
 
Back
Top Bottom