Usipande boda usiemjua usiku mwezenu yamenikuta

Usipande boda usiemjua usiku mwezenu yamenikuta

Kwanza pole saana kwa yaliyokusibu.Shehe pilau hailiwi usiku pilau yaliwa mchana !
Pili umeuliza kuhusu kundoa alama ya mabaka ya majeraha usoni/mwilini.Tumia kupaka asali sehemu iliyoathitika au nenda pharmacy yoyote kubwa kaulize dawa ya kutoa alama za majeraha utapata.
Mwisho nimalizie tu kuwapa story ya kuwa siku moja kiasi cha saa kumi usiku niliamua kuacha gari mitaa ya sinza kwa kuwa haikuwa na mafuta ya kutosha baada ya kuipaki gari nikasogea barabarani maeneo ya sinza uzuri uwanja wa TO darajani nikisubiri bodaboda ikaja ya kwanza ikapita ikaja ya pili ikasimama kidogo kwa mbele kama unaelekea sinza kijiweni nikaenda nikamwambia nataka kwenda Mwenge kwa kuwa nilitaka nikapande daladala za kwenda Bunju.Jamaa akanipakia lakini akanambia ye meneja wa baa mojawapo karibu ya mlimani city anaelekea kazini na amenichukua kwa sababu amenihurumia ningeweza kudhurika akaniusia kuwa nisijaribu tena kufanya hivo siku ingine yaani kusimamisha bodaboda usiku njiani kwa sababu wengi wao ni vibaka na majambazi naweza kujikuta napata madhara makubwa akanishauri niwe nasogea mpaka sehemu amabapo kuna staendi ya bodaboda wakiwa wengi! Basi alinipeleka hadi Mwenge pale Shall/PUMA ambapo pale unapata magari ya Tegeta /Bunju masaa 24 na watu muda wote wa usiku wapo wa kutosha na ni salama.
Hivo nami nawausia usipande bodaboda za kusimamisha niani usiku nenda hadi katika kituo ambacho utakuta zipo nyingi unachagua mojawapo kwani katika kituo si rahisi kukuta vibaka au majambazi wa dizaini.
 
[emoji23][emoji23]
Screenshot_20241227_160316_Gallery.jpg
 
Hilo ndo la kumshkuru Mungu maana nilikuja kupata story the same date vibaka walimchoma kisu Cha tumbo mwanachuo chuo Fulani huku huku hakuomba hata maji,
Ni Mungu tu
Mtaa gani huo? Kwanini unaficha ficha mtaa wenye WAHALIFU? Bila shaka mlidhurumiana na VIBAKA wenzio wakakukata hayo mapanga
 
Wakuu heri ya Christmas, japo kkwangu ilikuwa mbaya.

Huwa Sina tabia ya kutoka usiku sikukuu yoyote ila saa 3 usiku nikapata mwaliko wa pilau mahali Fulani, nkaenda nkala safi, vikaanza vinywaji mdogo kuja kushtuka saa6 na madakika kumpigia boda wangu hapokei mwingine akapokea ila kashalala.

Nikasema no sweat nitatafuta barabarani yoyote yule kweli nikampata nlikuwa nipo na mshikaji wangu tukapanda mshikaki.

Kufika kichochoro chenye mwanga hafifu bodaboda akayumba kidogo tukajikuta Chali tushadodondoka, kuhangaika kujiinua nakutana na panga la uso, mara nasikia kauli "wachukulieni kila kitu" ndo akili ikaja hapa tushaingia 18 za vibaka, nafosi kunyanyuka Tena nikachezea Tena la uso, nikaona hapa niwe mpole akazama mfukoni akasomba kila kitu mpaka bablish zangu.

Alivyoniachia nikatoka nduki la kilevi mixer kupepesuka hata yule mwanangu sikumkumbuka kumbe naye anachezea maparu tulikuja kuona home tunaugumia wote majeraha.

Akili kukaa sawa nikatambua yule boda na wale wahuni wako pamoja maana ye hakuguswa, na hata Ile kuanguka ilikuwa ishapangwa nao, kwamba akifika sehemu nzuri ya kutushughulikia ajiangushe makusufi muda huo wahuni wanatufata kwa nyuma kimyakimya, sema kutokana na hali ya ulevi hata hatukuwashtukia si unajua pombe Ina tabia ya kupuuza.

Wakuu nawaonya usipande boda usiku kama humjui, minishayavagaa, wameniharibu reception yangu ninaomba msaada kwa anayejua dawa ya kuondoa makovu usoni hapa bado nauguza majeraha ila najua ya kipona hizo kovu zitakuwa za kufungia mwaka.

Natanguliza shukrani
...Pole Sana, Mkuu [emoji120]
 
Panga la uso na hospitalini hujaenda?
 
Yaani hii dar na viunga vyake nikabwe 😄
linapokuja suala la kujilinda,kutembea kuishi kimachale basi hapa ndipo penyewe

Ova
🤣🤣 Hongera bhana,sema nini ...huwa yatokea tu popote
 
🤣🤣 Hongera bhana,sema nini ...huwa yatokea tu popote
Kuna sehemu bado watu wanaishi kizamani sana usela wa kizamani
Wakikuona foreigner lzm wakukabe...unajiuliza watu hawabadiliki

Ova
 
  • Kicheko
Reactions: M45
Back
Top Bottom