Usipande boda usiemjua usiku mwezenu yamenikuta

Polisi juzi walitoa tamko ukiona umelewa huwezi kwenda nyumbani wapigie wao watakufata na kukupeleka kwako
Unadhani ni bure... hapo lazima 50 au 60 ya mafuta ikutoke.
 
2
Polisi juzi walitoa tamko ukiona umelewa huwezi kwenda nyumbani wapigie wao watakufata na kukupeleka kwako
Wapi weweee...?. Polisi hawa hawa wetu?Na wewe ukawaamini?. Bora huyo alikutana na hao wakamseach tu hawakumlaza na ndani,wakamuachia aende zake,bila tena kutoa ya kutokea ndani
 
Mwanaume inakuje uwe na Bodaboda wako? Inafikirisha sana hii
 
Polisi juzi walitoa tamko ukiona umelewa huwezi kwenda nyumbani wapigie wao watakufata na kukupeleka kwako
Hii ilikuwepo botswana miaka ya 2000, sijui kama ipo miaka hii, ila kwa hawa polisi wetu ukienda umelewe ati upelekwe kwako nadhan litakukuta jambo.
 
Kuna sehemu bado watu wanaishi kizamani sana usela wa kizamani
Wakikuona foreigner lzm wakukabe...unajiuliza watu hawabadiliki

Ova
Wanakuona kama umewadharau kwenye mitaa yao,wanakaa wauni tu.
 
Hii ilikuwepo botswana miaka ya 2000, sijui kama ipo miaka hii, ila kwa hawa polisi wetu ukienda umelewe ati upelekwe kwako nadhan litakukuta jambo.
Hawa wa kwetu sio wa kuaminiwa
 
Juzi mida ya saa sita na mshkaj wangu tunapita chocho tukakutana na mlevi analia jamaa wamempiga na wamemuibia kila kitu sijui ndo wewe.
Sio kweli mkuu baada ya tukio sikupita Chocho yoyote nilinyosha barabara kubwa kutafuta boda mwingine ila kwa jinsi nilivyokuwa na midamu usoni wote walininawa wanaona hii kesi hii, ikabidi ninyooshe mpaka geto
 
Niliwahi panda bodaboda usiku, ilipofika sehemu anatakiwa kunisimamisha,akapitiliza, nilivyomwambia mbona unaenda tofauti jamaa hakusimama,baada ya hapo nilimwambia kitakachofuata nampiga kisu cha shingo,akageuza njia kurudi nilipotaka.
Ukweli hiyo siku huyo bodaboda nisingemuacha salama,kabla ya kufika kwa wahalifu wenzake,nilikuwa natanguliza kuzimu ili hata wezi wenzake wakija na mimi niwe nimefanya jambo.
 
Ahsante sana, hili la asali itabidi nijaribu
Ni kweli bodaboda waaminifu saa 3 mpaka 4 wanaenda kulala maana wanafamilia zao, ila hawa wa usiku kama sio kibaka basi jambazi nakubaliana na wewe unless wawe katika kituo kinachojulikana
 
Mtaa gani huo? Kwanini unaficha ficha mtaa wenye WAHALIFU? Bila shaka mlidhurumiana na VIBAKA wenzio wakakukata hayo mapanga
Hata nikitaja haisaidii, we jua kila mtaa usiku hao vibaka wapo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…