Usipokuwa makini utajikuta unachangia harusi 5 hadi 6 kwa mwezi

Usipokuwa makini utajikuta unachangia harusi 5 hadi 6 kwa mwezi

Witch hunter

JF-Expert Member
Joined
Nov 21, 2018
Posts
2,106
Reaction score
5,806
Hii app ya Whatsapp sioni faida yake kabisaaa imegeuka kausha damu kwangu, imagine nina group tano za michango ya harusi na zote zinadai 50K kwenda juu. Na bado sijui kama kutakucha bila kuongezwa kwenye group jingine.

Yaani kila siku unaungwa kwenye magroup mpya za harusi, watu hata huwajui unaambiwa ni kaka yake Fulani, au ni ndugu wa Fulani then mkeka unawekwa uanze michango, sms usiku na mchana ni michango tu.

Hivi watu hawawezi oa bila kuchangiwa? Uoe wewe tukuchangie sisi? Au ndoa zinakuja kwa kushitukiza? Ka mshahara kenyewe 500K na ndugu wananitazama duh!

HAPANA.
 
Mimi hua sihangaiki.

Nkikuta wameniweka, naleft chap chap alaf namtumia text mlengwa kua hali yangu mbaya ntamtumia chochote kitu ndani ya wiki 2 au mwezi depending na deadline yao.

Baas hakuna mapresha tena. Namuwekea li thate kama ni ule usela wa kuunga na jojo, kama ni close ones anakula li fifte.

Nliwahi kuungwa li grupu lina ma injinia na madokta wa kutosha, aisee jamaa wa chini kabisa nkaona ana pledge laki mbili.

Nkapiga hesabu hapa watakuja kuniacha uchi sokoni, chqp chede nkasepa na mia, myakimyaki nkadere mwanangu nkampa li fifte nkamwambie kateseke kivyako
 
Hii app ya Whatsapp sioni faida yake kabisaaa imegeuka kausha damu kwangu, imagine nina group tano za michango ya harusi na zote zinadai 50K kwenda juu. Na bado sijui kama kutakucha bila kuongezwa kwenye group jingine...​
Shida tuna ubinafsi sana, mtu akiwa sherehe au harusi yake anafurahia kupokea michango kutoka kwa wengine. Ila wengine wakiomba achangie harusi ndo habari kama hizi zinaibuka.

Kama hutaki kuchangia na wewe usiombe michango kwa watu na usikubali wengine wakuchangie . Hakuna cha bure ukila na ukubali kuliwa.
 
Hii app ya Whatsapp sioni faida yake kabisaaa imegeuka kausha damu kwangu, imagine nina group tano za michango ya harusi na zote zinadai 50K kwenda juu. Na bado sijui kama kutakucha bila kuongezwa kwenye group jingine...​
Ukishaingia kwenye mzunguko wa michango ya harusi kutoka ni vigumu. Ukitafuta mchango wa harusi yako au mtu wako wa karibu ukachangisha watu 50, basi ujuwe itabidi na wewe uchange mara 50x2. Njia ya kukwepa mchango ni kutoomba mchango na mtu akitaka umchangie mwambie kwa macho makavu kuwa huchangii harusi bali unachangia misiba na magonjwa.
 
Mchango wa harusi mara nyingi hutegemea ukaribu wako na mhusika, siyo lazima uchangie kila harusi.
 
Mwanaume unakosaje msimamo? Unashindwa kusema direct tu kuwa sina hela full stop.

Unamuogopa nani sasa?

Binafsi sijawahi changia harusi wala kushiriki harusi yoyote ile hata ya ndugu zangu sipendi sherehe sherehe kabisa huwa sipendi mirundikano ya watu.

Uzuri ni kwamba sina wazo la kuoa maishani mwangu.
 
Ukishaingia kwenye mzunguko wa michango ya harusi kutoka ni vigumu. Ukitafuta mchango wa harusi yako au mtu wako wa karibu ukachangisha watu 50, basi ujuwe itabidi na wewe uchange mara 50x2. Njia ya kukwepa mchango ni kutoomba mchango na mtu akitaka umchangie mwambie kwa macho makavu kuwa huchangii harusi bali unachangia misiba na magonjwa.
Tuko Tanzania mkuu... Haya maneno ni makali mno... Tutauwawa
 
Back
Top Bottom