Hii app ya Whatsapp sioni faida yake kabisaaa imegeuka kausha damu kwangu, imagine nina group tano za michango ya harusi na zote zinadai 50K kwenda juu. Na bado sijui kama kutakucha bila kuongezwa kwenye group jingine.
Yaani kila siku unaungwa kwenye magroup mpya za harusi, watu hata huwajui unaambiwa ni kaka yake Fulani, au ni ndugu wa Fulani then mkeka unawekwa uanze michango, sms usiku na mchana ni michango tu.
Hivi watu hawawezi oa bila kuchangiwa? Uoe wewe tukuchangie sisi? Au ndoa zinakuja kwa kushitukiza? Ka mshahara kenyewe 500K na ndugu wananitazama duh!
HAPANA.