Usipokuwa makini utajikuta unachangia harusi 5 hadi 6 kwa mwezi

Usipokuwa makini utajikuta unachangia harusi 5 hadi 6 kwa mwezi

Hii app ya Whatsapp sioni faida yake kabisaaa imegeuka kausha damu kwangu, imagine nina group tano za michango ya harusi na zote zinadai 50K kwenda juu. Na bado sijui kama kutakucha bila kuongezwa kwenye group jingine.

Yaani kila siku unaungwa kwenye magroup mpya za harusi, watu hata huwajui unaambiwa ni kaka yake Fulani, au ni ndugu wa Fulani then mkeka unawekwa uanze michango, sms usiku na mchana ni michango tu.

Hivi watu hawawezi oa bila kuchangiwa? Uoe wewe tukuchangie sisi? Au ndoa zinakuja kwa kushitukiza? Ka mshahara kenyewe 500K na ndugu wananitazama duh!

HAPANA.
Nauhakika ndoa nyingi hizo ni za KIKRISTO na mazishi yao ndio wamefanya anasa
Huwezi Kuta huu UPUMBAVU kwa watu waliostaarabika kama mabudha,wahindu na waislam
 
Mimi hua sihangaiki.

Nkikuta wameniweka, naleft chap chap alaf namtumia text mlengwa kua hali yangu mbaya ntamtumia chochote kitu ndani ya wiki 2 au mwezi depending na deadline yao.

Baas hakuna mapresha tena. Namuwekea li thate kama ni ule usela wa kuunga na jojo, kama ni close ones anakula li fifte.

Nliwahi kuungwa li grupu lina ma injinia na madokta wa kutosha, aisee jamaa wa chini kabisa nkaona ana pledge laki mbili.

Nkapiga hesabu hapa watakuja kuniacha uchi sokoni, chqp chede nkasepa na mia, myakimyaki nkadere mwanangu nkampa li fifte nkamwambie kateseke kivyako
Huu mwandiko utakuwa wa Arusha
 
Ni kutoa tuu
20241003_152546.jpg
 
Hizi mambo nishaona ni ujinga tu kuchangiana ...kuna bestfrnd wangu ana jambo lake next WK...aliwachangia jamaa flan iv last year..150k Cha ajabu aliwataarifu kuwa ana jambo lake....moja kqmtumia 10k na mwngine hakujibu hatq msg....hapa nmeapa sitomchqngia mtu yyte tena...yeye anataka akuvune afu kwako qnajikausha
Ukipewa usisahau, ukitoa toa bila kukumbuka.

Ukiisha kwa matarajio kutoka kw wanadamu utakua dissappointed kila siku.
 
Kama walikuchangia kipindi cha harusi yako na wewe wachangie kipindi cha harusi zao .

Kama hawakukuchangia katika harusi yako na wewe usichange harusi zao...........

Mwisho kabisa katika maisha jifunze kuwa na msimamo sio leo hii unawakataa watu wa karibu alafu kesho kutwa unawahitaji kipindi una jambo lako
Mkuu ukiishi na mentality hii itakutesa, utakuwa mfungwa wa maisha yako mwenyewe.

Yaani uko radhi ujiumize ili tu mambo yao yaende ukiwa na matarajio siku ukikwama watakusaidia. Hii sio sawa.

Kama unatenda jambo litende kutoka moyoni sio kwa sababu Juma atasema hivi, Stella ataninunia. Ukisharuhusu wanadamu wawe na effect kwenye maisha yako hutakuwa na maamuzi.

Nikiwa na hela nakutolea. Sina, sina. Mchango hauna mantiki, sitoi.

Kama siku ikitokea naumwa taabani na hutaki kunichangia kwa kuwa sikuchangia harusi yako basi ni juu yako wewe na Mungu wako ukamueleze huko msikitini na kanisani huwa unaenda kusali kitu gani.
 
Haya ni matokeo ya sherehe kufanywa biashara, MC alipwe, Ukumbi, Caterer, videographer, mziki, sijui nini nini..

Kuna tatizo gani kwa sherehe za nyumbani? Wanafamilia, nani atashindwa kulisha familia yake?

On the other hand kiuchumi, tumieni pesa ili izunguke 😜
Cha ajabu unaweza ukawaambia ndugu zako mi nataka sherehe yangu iwe simpo tu lakini utapingwa na watashupali michango ichangishwe utafikiri wanaoa wao.
 
Wakuu hizi mambo za kijinga sana mimi nilioa bila kuchangisha niliandaa budget yangu ya watu 50 tu. Na matukio ya hapa na pale ila cha ajabu kuna wale niliwaalika na wengine sikualika ila mtu anatuma kuomba mchango ukisema huna anakasirika why?

Umeandika vizuri sana hapo chini Ndoa ni mipango sio emergency. Ila kuna wadau kwao bora usichange msiba ila harusi na sendoff watakutoa damu yaani lawama kibao.

Sasa hivi nimelimit kabisa ishu za kuwa added kwenye group za WhatsApp bila kuniomba na ukiomba kuniadd nakataa nasema tu nitakuchangia nikiwa fresh, so nikipata sawa nikikosa basi ila stress za magroup sitaki.
 
Namshukuru Mungu sipo kabisa katika mawazo ya watu kwenye kuchangia harusi.
Nina miaka 4 sijahudhuria harusi/kitchen party/send off wala kuvaa sare ya sherehe yoyote.

Kabla ya hiyo mitano nilikaa tena karibu miaka 6 nyuma, nikahudhuria hiyo
moja 2020.

Nimejitafutia a very beautiful way ya kuungana na jamii inayonihusu
1. Ukiumwa nitakuja kukuona aidha hospitali au nyumbani kwako
2. Ukifiwa/ukifariki nipo pale kukuona unapata hifadhi au mpendwa wako anahifadhika vizuri tu
3. Ukipata tatizo serious nitakushauri, kukusaidia wa fedha labda iwapo niko kwenye nafsi ya kufanya hivyo ili utatue.
4. Ukipata mafanikio/kupata mtoto/kupanda cheo/ kuoa/kuolewa nitakupongeza kwa uwazi kabisa hata post nitakuandikia
5. Nitakupigia simu au kukutumia ujumbe kukujulia hali nipatapo nafasi, mimi si aina ya watu natafuta wengine ninapokuwa na shida tu. Hapana! I check on people randomly tu.

KWANINI?
Mimi siwezi kabisa michanganyiko ya watu wengi.
Sichukii watu, bali sipendi kusanyiko la watu kwa wakati mmoja.
So msibani sina choice lazima niwepo, ila bado si sehemu ninakuwa sawa.
Nakosa energy kabisa ya kuoperate akili wala mwili kwenye watu wengi.

Si wala issue ya confidence, its just mahali pekee ninajihisi salama na nina furaha ni nyumbani kwangu!
Nikiwa na wale tu niliowazoea, watu wengi kwa mara moja ni kama nimevamiwa.

Harusi si mahala kwangu kabiiiiiisa physically, ninazifurahia tu nikiziona kwa Gara B. Baaas!
So
-Bajeti ya michango ya harusi huwa haipo kabisa kwenye kipato changu.
-Sare sijui za wadada sijui marafiki mimi sipo
-Make up sijui nywele sijui nn kwa ajili ya sherehe sipo

Sijioni nikibadilika, am gud this way!
 
Harusi yangu sikuchangiwa na umma kwenye familia tuna utaratibu wa kuchangiana, Hivyo hata niungwe kwenye hizo grou huwaga sichangii na mtu hawezi kunilaumu au kunishtumu
Nko vzr sana
 
Nauhakika ndoa nyingi hizo ni za KIKRISTO na mazishi yao ndio wamefanya anasa
Huwezi Kuta huu UPUMBAVU kwa watu waliostaarabika kama mabudha,wahindu na waislam
Kimsingi ni mzgo mzto sana
 
Wacha kabisaaa... Mimi lipo moja mpaka sasa mwenye kiwango cha chini ni 250k yaani hadi jasho....
Ndio wewe uliyejifanya una jeuri ya kunipa mimi 200k kumbe kimshahara chako chenyewe hakikutoshi mpaka kuchangia mambo ya kijamii tu unalia lia namna hii!?
Screenshot_20241003_165945_Samsung Internet.jpg
 
Nina fungu maalumu kwa ajili ya mayatima, wajane, maskini na wasiojiweza, hyo 200k inatoka katka fungu hilo maana hujiwezi.
Pole sana kijana,acha kujitutumia kulikonuwezo wako , tutashindwa kukusaidia shauri zako., bado una safar ndefu sana kuyafikia mafanikio. Na huna ujanja huo unaojifanya unao kama hata kigari tu unatembelea screpa kama hizi πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡
Screenshot_20241003_170744_Samsung Internet.jpg
 
Back
Top Bottom