Ni rahisi sana. Iko hivi, kama hujawahi kuomba mtu mchango, hakuna mtu anayestahili mchango wako. Hauna deni.
Maana yake mtu anapokuomba mchango, unaweza kumjibu direct kwamba 'samahani sitaweza' na yeye hawezi kuku press kwasababu hakudai - hujawahi kumchangisha.
Ukiwa na msimamo thabiti watu wataliona hili na wataacha kukusumbua. Binafsi kwa mwaka nachangia harusi za mtu mmoja au wawili - ambao ni ndugu nimekuwa nao na tumeshibana.
Sichangii sherehe ya ndugu wa ndugu, rafiki wa ndugu, ndugu wa rafiki na third parties nyingine kama hizi. Hata ndugu ambaye simfahamu (ndugu wa kuambiwa tu - sijawahi kuonana naye) sichangii.
Nimekuwa na msimamo katika hili kiasi cha kwamba siombwi michango wala siaddiwi kwenye magroup.
Ukisema 'hapana' za kutosha, watu wataacha kuomba