Usipoteze tumaini, dunia ndivyo ilivyo

Usipoteze tumaini, dunia ndivyo ilivyo

Kalaga Baho Nongwa

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2020
Posts
9,953
Reaction score
23,150
Ni imani yangu sote tu wazima, nina kila sababu leo kuongea na vijana wenzangu.

Sote tunafahama hali ya maisha, vita ya kulipigania tumbo ni vita ngumu zaidi kuliko ile ya kusaka utajiri. Ni kama ile vita ya kupigania uhai, unapambana ii uendelee kuitwa kiumve hai.

Kwa mara kadhaa nimekuwa nikiandika mada zenye mfululizo wa kufichua mazingira yenye bidhaa nafuu ili aliyekwama kuanza biashara kwa sabab hiyo aanze. Bado napata ukakasi yA kwamba bado tuna idadi kubwa ya vijana ambao hata kufikiria kufanya biashara hawajawahi pamoja na uhalisi uliopo.

Katika perspective hii, sababu za kushindwa walau kufikiria kwamba kuna siku wataanza biashara ni pamoja na kukosa mitaji, shinikizo la kuajiriwa kuwa na faida nyingi kuliko hasara nk. Biashara bado inalipa, pamoja na ugumu uliopo katika kulipambania tumbo na kujitegemea

Safari bado ni ngum, mwanzo unakatisha tamaa na mwisho unaoonekana wakati wa kuanza unaogofya sana. Never lose hope.

Screenshot_20241116_173630_WhatsAppBusiness.jpg
 
Maisha yapo hivo wanaanzia kwenye mifuko
Wanakomaa, wanajifunza, wanakuja kubadilisha maisha Yao
Kikubwa kupambana
Kupambana hakuepukiki, ila kadiri miaka inavyosonga naona hali tight sana. Mpaka leo sijajua tatizo hasa linaanzia wapi ni population au n nn mbona fursa imekua kitendawili.
 
Hiyo hali ipo nchi nyingi Africa
Tunaamini katika kusota ndo ufanikiwe
Kikubwa afya ipo
That's can not be tentative answer. Leo hii tungekuwa na sababu za msingi kujadili pengine mjadala huu ungetufaa mbeleni. Afya hii haiwez kuwepo sababu watu wanashinda na njaa na kufanya kazi ngum pamoja na njaa waliyonayo.

Tunaanzaje kutafuta suluhu walau miaka kadhaa mbele mambo yasiwe tight zaidi. Mm nina hakika kuna kazi watu wamezikataa miaka kadhaa nyuma leo hij kuzipata mtihani. Katika hali isio ya kawaida modernization inavunja kabisa ukaribu wa ndugu, miaka ya sasa hata ndugu yako haguswi kabisa na changamoto zako
 
Back
Top Bottom