Usipowasamehe waliokukosea, unajipeleka mwenyewe katika moto wa milele!

Usipowasamehe waliokukosea, unajipeleka mwenyewe katika moto wa milele!

Binadamu tumeumbwa kwa sura na mfano wa mungu.

Kama mungu alishindwa kumsamehe shetani, wamewekeana bifu mpaka leo miaka maelfu, isitoshe na ugomvi wao akaona atuunganishe na sisi tusiohusika, mimi ni nani nisamehe?
 
kusamehe ni udhaifu, jino kwa jino
yaani mtu akuumize makusudi alafu umwache aishi kwa aman hapana lazima nae apitishwe kwenye tanuri la moto
 
Kesi ya Mungu na shetani ni tofauti kabisa. Shetani hakutaka kutubu wala kuonyesha moyo wa toba.

Pili, huyo unayekataa kumsamehe ni shetani au ni binadamu mwenzako?

Tafakari tena andiko hili:
"Na mkiwa na neno juu ya mtu, sameheni, kama Kristo alivyowasamehe ninyi.” (Wakolosai 3:13)
 
kusamehe ni udhaifu, jino kwa jino
yaani mtu akuumize makusudi alafu umwache aishi kwa aman hapana lazima nae apitishwe kwenye tanuri la moto
Sheria ya jino kwa jino ni ya Agano la Kale. Kwa sasa tuko chini ya Agano Jipya linalotutaka kusamehe hata saba mara sabini.
Mtu akikupiga shavu la kulia mgeuzie na shavu la kushoto(Mt 5:39)
 
Sawa, mkuu. Ila kuna wengine sijui wanafanya makusudi au sijui ni nini. Ukimsamehe kosa lake leo, kesho anakuja tena anakufanyia kosa lile lile. Inafika mahali unachoka kusamehe.
Msamaha haupaswi kuwa na kikomo.
Soma Mt 18:21-22
"Kisha Petro akamwendea, akamwambia, Bwana, ndugu yangu akinikosea mara ngapi nimsamehe? Hata mara saba? Yesu akamjibu: sikuambii hata mara saba; bali hata saba mara sabini"
 
Naongea na wewe uliyekataa kumsamehe ndugu yako, jirani yako, mke wako, mme wako, mzazi wako nk

Hapo ulipo huenda una kinyongo naye; umejaa chuki dhidi yake, hutaki hata kumuona au kumsalimia. Yamkini unapanga pia kulipiza kisasi.

Inawezekana huyo uliyekataa kumsamehe, yumo humu humu JF na umeamua kumuweka kwenye "ignore list"

Tafadhali sana nakusihi msamehe kuanzia leo. Msamaha sio chaguo la hiari; ni amri ya Mungu. Mtu anayekataa kuachilia dhambi za wengine, yeye pia hataachiliwa/hatasamehewa. Mtu huyo akifa na moyo huo usiosamehe, anakuwa amejipeleka mwenyewe katika moto wa milele.

Yesu anasema:
“Maana mkiwasamehe watu makosa yao, Baba yenu wa mbinguni atawasamehe nyinyi pia. Lakini msipowasamehe watu makosa yao, naye Baba yenu hatawasamehe nyinyi makosa yenu..” (Mathayo 6:14-15)

View: https://www.threads.com/@elius_ndabila/post/DNqKKCcp2DA?xmt=AQF0pTX_3RMGlMkb5aQZBi9v1Dg6xnzw4Lm3adfLTNlHgQ
 
Nilisoma somewhere kwenye andiko la kitaalamu kwamba mtu ambaye anatakiwa kusamehe ni yule ambaye amefuga hasira,jazba na kisasi dhidi ya mtu ambaye hakumkosea kwa dhamira au dhati yake.

Kwa mfano, unaendesha gari kwa mwendo wa stara kabisa akaja mtoto kwa speed akitokea huko alipotokea akajipigiza kwenye gari na kuvunjika kiungo, then mzazi wake akuwekee kisasi. Huyo anatakiwa kusamehe kwasababu kwanza hakujui na humjui so haukuwa na dhamira yoyote na mtu usiyemjua kabla ya tukio. Pili mazingira ya tukio haukuyapanga na haikuwa sehemu ya mpango wako ugonge mtoto wa mtu. Huyu anapaswa akusamehe baada ya wewe kumuomba msamaha na asipokusamehe MUNGU atamuadhibu kwasababu MUNGU atanunua hiyo kesi na kumtetea yule asiye na hatia dhidi ya huyu anayebeba kisasi butu.

Ila ikatokea mfano mtu kwa kiburi akakufanyia kitendo ambacho madhara yake hayatibiki mfano ni waziri au askari akaamuru ndugu yako afungwe au ateswe kwa kosa ambalo kisheria ni la kulipishwa faini ila yeye akaifanya ni issue personal akampiga na kumdhuru mfano yule mzee Ali kibao. Hapo hutakiwi kusamehe, unatakiwa ulipize kisasa na hata MUNGU atakusaidia kumnyoosha. Ukisamehe hapa maana yake ulitaka yule nduguyo adhurike na kuumia.

Mfano katika mahusiano, ulikuwa unampenda sana mwanamke,kwa bahati mbaya wazazi wake ambao hawakupenda muwe pamoja wakaamua kuwatenganisha na binti alifanya kila mbinu kukurejea ikashindikana,huyu mkikutana baadae akiwa na watoto wa mwanaume mwingine pengine katelekezwa hautakiwi kuwa na kinyongo nae. Unatakiwa umsamehe na hata ikibidi umsaidie.

Ila imetokea unampenda binti una maisha ya kawaida kwa tamaa tu akalala na mtu mwingine na kukutamkia wazi kuwa amechagua kuwa na mtu mwingine aidha kwasababu kakuzidi pesa au ana mvuto au sababu yoyote ambayo sio ya msingi na haina utu ndani yake ,au akaamua tu kukupotezea kimya na kukughost kwa miaka mingi. Siku ukikutana nae akakuomba msamaha akitamani mrudiane, mkubalie halafu omba mkutane sehemu private,mzee tafuta fimbo za mpera mbili, funga mlango,tandika bakora hiyo Takataka piga kipigo cha mbwa mwizi. Tandika hadi nafsi yako iseme inatosha. Hakikisha hakuna mtu wa kuamulia hicho kipigo. Halafu muage na umwambie popote utakapokutana nae ni utaliamsha tena kwa mitama na makofi. Akae mbali na wewe kabisa asikuzoe. Trust me utajiskia vizuri.
 
Ubarikiwe sana Mshana Jr
kwa ku-share video hii... Injili inahubiriwa kwa kila njia ili asiwepo atakayetoa udhuru siku ya mwisho kwamba hakusikia...
Nabii Elisha: Je m'appelle Elisha, je parle Francais!...
Dada, are you married? Huyo mkoje nae?
Dada mpiga picha: Ni baba yangu

Hahaa, kama ni baba yake, Mungu ajua...
Kama ni mchepuko, Injili imepenya
 
Nilisoma somewhere kwenye andiko la kitaalamu kwamba mtu ambaye anatakiwa kusamehe ni yule ambaye amefuga hasira,jazba na kisasi dhidi ya mtu ambaye hakumkosea kwa dhamira au dhati yake.

Kwa mfano, unaendesha gari kwa mwendo wa stara kabisa akaja mtoto kwa speed akitokea huko alipotokea akajipigiza kwenye gari na kuvunjika kiungo, then mzazi wake akuwekee kisasi. Huyo anatakiwa kusamehe kwasababu kwanza hakujui na humjui so haukuwa na dhamira yoyote na mtu usiyemjua kabla ya tukio. Pili mazingira ya tukio haukuyapanga na haikuwa sehemu ya mpango wako ugonge mtoto wa mtu. Huyu anapaswa akusamehe baada ya wewe kumuomba msamaha na asipokusamehe MUNGU atamuadhibu kwasababu MUNGU atanunua hiyo kesi na kumtetea yule asiye na hatia dhidi ya huyu anayebeba kisasi butu.

Ila ikatokea mfano mtu kwa kiburi akakufanyia kitendo ambacho madhara yake hayatibiki mfano ni waziri au askari akaamuru ndugu yako afungwe au ateswe kwa kosa ambalo kisheria ni la kulipishwa faini ila yeye akaifanya ni issue personal akampiga na kumdhuru mfano yule mzee Ali kibao. Hapo hutakiwifunzei kusamehe, unatakiwa ulipize kisasa na hata MUNGU atakusaidia kumnyoosha. Ukisamehe hapa maana yake ulitaka yule nduguyo adhurike na kuumia.

Mfano katika mahusiano, ulikuwa unampenda sana mwanamke,kwa bahati mbaya wazazi wake ambao hawakupenda muwe pamoja wakaamua kuwatenganisha na binti alifanya kila mbinu kukurejea ikashindikana,huyu mkikutana baadae akiwa na watoto wa mwanaume mwingine pengine katelekezwa hautakiwi kuwa na kinyongo nae. Unatakiwa umsamehe na hata ikibidi umsaidie.

Ila imetokea unampenda binti una maisha ya kawaida kwa tamaa tu akalala na mtu mwingine na kukutamkia wazi kuwa amechagua kuwa na mtu mwingine aidha kwasababu kakuzidi pesa au ana mvuto au sababu yoyote ambayo sio ya msingi na haina utu ndani yake ,au akaamua tu kukupotezea kimya na kukughost kwa miaka mingi. Siku ukikutana nae akakuomba msamaha akitamani mrudiane, mkubalie halafu omba mkutane sehemu private,mzee tafuta fimbo za mpera mbili, funga mlango,tandika bakora hiyo Takataka piga kipigo cha mbwa mwizi. Tandika hadi nafsi yako iseme inatosha. Hakikisha hakuna mtu wa kuamulia hicho kipigo. Halafu muage na umwambie popote utakapokutana nae ni utaliamsha tena kwa mitama na makofi. Akae mbali na wewe kabisa asikuzoe. Trust me utajiskia vizuri.
Daah, fimbo mbili za mpera! Kweli njia ya mbinguni ni nyembamba, nao waionao ni wachache..
Jifunze kwa Yesu. Alivishwa taji ya miba, akasulibiwa msalabani, akachomwa mkuki.. Lakini bado aliwaombea msamaha waliomfanyia huo uovu
 
Mimi nilijaribu kusamehe watu ambao sikuwakosea jambo ila hata wao wanakiri walinikosea kwa kusudi ila wameomba msamaha.

Hakuna nafuu unapata zaidi ya majuto na kukosa amani kila ukimuona tena maana anakufanya mjinga mara mbili. Kwanza alikukosea kwa dhamira na ni bahati tu hakukumaliza kabisa ila pili amekuja kukuomba msamaha sio kwasababu yako ni kwasababu yake ili ajiskie vizuri na ukikaa vibaya atakufanyia tena ubaya mwingine.

Kuna kisa cha dada m'moja huko majuu, Martha McKay kuuwawa na kijana ambaye miaka 23 nyuma alimuua mama yake mzazi.

Huyo kijana (16 years) alimuua mama wa huyu dada kipindi akiwa bwana mdogo, then alitumikia adhabu yake na baada ya kutoka binti alimpa kazi na kuishi nae kwa imani ya samehe saba mara sabini na mpende adui yako zaidi ya rafiki yako. Kilichomkuta ni kukatishwa uhai na mtu yule yule aliyemdhurumu uhai.

Angemuwekea kisasi na kuhakikisha akitoka anamalizana nae kibabe si ajabu leo angekuwa hai.

Kisasi hakitakiwi kwa mtu ambaye amekukosea bahati mbaya ila kisasi ni tiba ya akili na muhimu kukifanya kwa mtu ambaye alikutazama usoni wewe ukilia machozi yeye bila huruma akifurahia kukuona unaumia na unateseka huku yeye akiwa ana nafasi ya kukuokoa au kuacha mara moja ili usiumie zaidi ila yeye anandelea kupuuza maumivu yako anafurahia kukuona ukiumia.

Huyu usimuachie, ukipata nafasi ya kumkomesha itumie vema sana na hakikisha anaumia hadi anakumbuka ile siku alikukosea. Trust me utajisikia vema moyoni na hakuna dhambi utaandikiwa.

Kuna kisa pale uarabuni sikumbuki kama ni Iran au iraq. Kuna dada alikuwa mzuri tu. Sasa kuna mtu alikuwa anataka kumla ila binti hakuwa tayari kuwa nae sababu alijua jamaa anatamaa tu za kingono.

Jamaa akavizia binti yule akamwagia tindi kali. Akapata damage isitofutika usoni kwa 90% . Ukimuona huwezi mjua kama ni mwanadamu. Jamaa alikamatwa. Baada ya kukiri kosa na kuomba msamaha familia ikasamehe,ila system ya waarabu ni unachagua adhabu. Akasema anataka jamaa nae achezee acid. So jamaa akapewa adhabu ya kumwagiwa acid ili aone matokeo ya alichofanya kwa yule binti.

So nasisitiz tena. Akikukosea kwa bahati mbaya,msamehe kwa huruma sababu hakukuwa na dhamira ya kukudhuru. Na ndio maana nasisitiza kuwa ni vema kusikiliza maelezo ya aliyekukosea kabla haujatoa hukumu. Pengine kuna kitu haujakijua so usikurupuke kutoa adhabu au kisasi.

Ila ukishajiridhisha na muhusika kuwa alikuwa na dhamira sio kwa wewe kutaka tu kumkomesha au kumtolea hasira, kama umejiridhisha 100% bila doubt kuwa alikukosea kwa makusudi kabisa then wala hakuna alama yoyote ya bahati mbaya, then hiyo ni wewe tu sasa, chagua kuishi na maumivu au kumalizana nae vibaya.

Mimi ukinikosea na tukaketi na kuweka maelezo mezani na ikadhihirika bila utata kuwa kuna maeneo ya kukosea kibinadamu then hapo mimi bila shida nitarudisha moyo nyuma tuanze ukurasa mpya kwa amani.

Ila kama tulitazamana usoni wakati ukinikosea na nilikwambia kuwa unaniumiza au unanidhuru ukasema "kwahiyo sasa unatakaje" au " ndio ukome na bado ntakunyoosha". Then jua tu siku utakayokuja kuniomba msamaha mimi nitakuwa napanga kisasi changu. Na nitakunyosha mbwa wewe hadi ujue kuwa binadamu hatuna nguvu juu ya binadamu wengine.

Shenzi kabisa.
 
Daah, fimbo mbili za mpera! Kweli njia ya mbinguni ni nyembamba, nao waionao ni wachache..
Jifunze kwa Yesu. Alivishwa taji ya miba, akasulibiwa msalabani, akachomwa mkuki.. Lakini bado aliwaombea msamaha waliomfanyia huo uovu
Si umesikia lakini kuwa atarudi kuja kugawa kichapo kwa watenda dhambi?😂😂 Kisasi kipo kwa wanaofanya kusudi.

Yaani uniumize moyo wangu kabisa kwa makusudi naona halafu nikuache nikipata fursa ya kisasi aisee utaandika barua ya msamaha kwa machozi na damu. Sinaga huruma na wasaliti.
 
Sawa, mkuu. Ila kuna wengine sijui wanafanya makusudi au sijui ni nini. Ukimsamehe kosa lake leo, kesho anakuja tena anakufanyia kosa lile lile. Inafika mahali unachoka kusamehe.
Na ni matokeo ya kuambiwa kuwa ukikosea omba msamaha. So wanajua kuwa akitia huruma atasamehewa.
 
Back
Top Bottom