Usipuuzie ulaji wa matunda. Ina faida kubwa sana kiafya

Poa yanaongeza sana nguvu za kiune Kwa wanaume,me ni shahidi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tende zisikose kwenye list yako.
 
Kwenye hiyo list yako ongezea na Apple [emoji519][emoji520]
Ndiyo, Apple na Tende. Huwa nazitumia pia, hasa tende, ni kawaida kuzikuta kwangu sema si mara nyingi napata fursa ya kuzila. Ndizi na chungwa zimekaba nafasi.

Ila apple nazo ni nzuri. Wanasema ONE APPLE A DAY KEEPS A DOCTOR AWAY
Hata hivyo, wanasema ndizi ina virutibisho vingi zaidi kuzidi apple.

Lakini ni tunda zuri na ninalipenda.

Asante kwa ushauri. Umepokelewa kwa mikono miwili.
 
Mkuu,

Huu n ujumbe mzuri,mm pia n mdau wa matunda japo siku hiz nmeacha kuyapa uzito kama mlo unaojitegemea .ilkua dinner n matunda

Ila nina hoja hapa ,

Wataalamu wa afya wanasema matunda yaliwe kwa akili na kwa uangalifu mkubwa kwan mwili hauna mfumo tofaut wa kuchakata sukar ya matunda (natural) na sukar artificial (ambazo tunaambiwa ndio mbaya kwa afya kama soda,juyce,nk) yaan mwili unachakata sukar kama sukar

Hvyo matunda yenye sukar nying kama tikit,ndiz,machungwa,nanasi yakiliwa kwa kais kingi yana athari sawa na alyekunywa soda/pombe/juyce za viwandan naamnukuu Dr.boaz mkumbo

Bado sjamnukuu dr Janabi [emoji28]

Science ya lishe imenishinda kabisa

Ila nafkiri kila chakula kitumike kwa kias kidogo hasa wanga,sukar na mafuta..tutakua kwenye nafasi ya kupata matokeo mazur ya kiafya.
 
Wa Nashukuru mkuu, ila wakati mwingine ni kama vile wataalamu wanatuchanganya.
 
Matunda ni chakula bora kuliko vyote duniani sema mindset zetu ndo zinatucost. Hebu fikiria KWANINI MUNGU ALIWAWEKA BINADAMU WA KAWANZA KATIKA BUSTANI YA EDENI ILIYOSHEHENI MATUNDA YA KILA AINA?
Unadhani hakuna nyama kipindi kile?
La hasha!
Alijua matunda ni bora kuliko chochote,,,TULE MATUNDA KWA AFYA ZETU.
 
Mimi nilipo matunda hadimu sana ila kuna tikiti na tango tu na samaki wapo wakimwaga na kuku wa kienyeji na maziwa ya kienyeji na majani ya maboga mikunde kisamvu mchicha dona sana na bakuli la majani ya maboga na samaki mchemsho
 
Mimi nilipo matunda hadimu sana ila kuna tikiti na tango tu na samaki wapo wakimwaga na kuku wa kienyeji na maziwa ya kienyeji na majani ya maboga mikunde kisamvu mchicha dona sana na bakuli la majani ya maboga na samaki mchemsho
Kuku wa kienyeji!
Samaki mchemsho
Matikiti na matango!
Kisamvu, majani ya maboga, mikunde...n.k.

Mpaka na maziwa!

Hongera kwa kufaidi mema ya nchi!!!
 
.
 
Uliyaona hayo kila aina ya matunda?
 
Life is temporary,ukifa na ngozi nzuri inakusaidia huko kaburini.mi nakula chakula ninachojisikia,nakua tunda nikiwa na hamu nalo,nakula nyama,nakula samaki,napiga supu ya ulimi,mkia,kongoro,nakunywa bia castle lite baridi,kitimoto roast na ndizi saafi ,sijawahi kuumwa huu mwaka zaidi ya wakumi,napiga shoo kwa mama yeyoo kama kawa.kuishi kwa uoga kwa kuogopa kufa ni ujinga.enjoy
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…