Usiri watanda ajali ya Naibu Waziri Tamisemi

saigilomagema

JF-Expert Member
Joined
Jun 5, 2015
Posts
4,683
Reaction score
7,222
Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais (Tamisemi), Dk Festo Dugange amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Benjamin Mkapa mjini Dodoma akipatiwa matibabu baada ya kupata ajali ya gari

Habari za uhakika ambazo Mwananchi limezipata, zinaeleza Dk Dugange alipata ajali hiyo usiku wa kuamkia Aprili 26, 2023. Hata hivyo, mpaka sasa si Jeshi la Polisi wala viongozi wa wizara yake waliokuwa tayari kuthibitisha kuhusua ajali ya kiongozi huyo.

Licha ya jitihada za Mwananchi kuwatafuta Waziri wa Tamisemi, Angellah Kairuki na Naibu wake, Deo Ndejembi pamoja na Msemaji wa Serikali, Gerson Msigwa lakini, hakuna aliyekuwa tayari kuzungumzia taarifa hizo.

Hata hivyo, akihutubia wananchi wa Wilaya ya Chamwino, Dodoma kwenye uzinduzi wa majengo ya Jeshi la Zimamoto Aprili 26, 2023, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliwaambia mbunge wao Ndejembi hakuhudhuria hafla hiyo kwa sababu alipewa jukumu la kumuuguza naibu waziri mwenzake aliyepata ajali.

"Ndugu wananchi, naleta salamu nyingi kutoka kwa mbunge wenu Ndejembi (Deo) alitamani kuwa nanyi hapa, lakini tumempa jukumu la kuangalia matibabu ya naibu waziri mwenzake alipata ajali Jana," alisema Majaliwa bila kumtaja naibu waziri huyo aliyepata ajali.

Taarifa za uhakika ambazo Mwananchi limezipata kutoka hospitalini hapo, zinaeleza Dk Dugange ambaye ni mbunge wa Wanging’ombe, mkoani Njombe alifikishwa hospitalini akiwa mahututi na kwa sasa hali yake inaendelea vizuri.

"Ni kweli majeruhi tuliyenaye ni Dk Dugange, alifikishwa hapa akiwa kwenye hali mbaya lakini tunamshukuru Mungu kwa sasa anaendelea vema," kilisema chanzo chetu.

Source: Mwananchi
My Take:
Waziri mkuu anashiriki ktk upuuzi km huu? Bila wamwondoe mtu wao kimya kimya anaeenda kuhudumiwa na waziri mwingine?. Mtu aliyefanya jambo la aibu km lile? Nimechoka na viongozi wa nchi hii.
Tuna viongozi kweli nchi hii, halafu bila haya wanaongelea maadili, nimemdharau huyu waziri mkuu mpaka basi. Wanahabari fichueni ujinga huu usikike kimataifa tuhakikishe huu kijana asiye na maadili harudi kwenye uongozi wa nchi yetu.
 
Hii nchi inachekesha, sasa huyu ndiye waziri anayesimamia watumishi wa local government, huyu mchepukaji ndio anasimamia uhamisho wa watumishi🤣 no wonder tukiandika sababu ya uhamisho ni kumfata mwenzi wa ndoa wanasema ndoa sio sababu ya uhamisho....imagine mume Kagera, mke Mtwara.....ndo maana wahenga walisema aliyeshiba hamjui mwenye njaa....wao hawana upwiru, hawaheshimu ndoa, wanajichepukia hadharani ...so ukisema unaomba uhamisho kumfata mwenza wanakushangaa.

Wakitoka kuziniana huko wanasimama majukwaani sijui maaadili, maadili....unafiki mtupu....Mama kipenzi tafadhali tuondolee huyu mtu, hafai kukaa hapo wizarani.
 
Umeongea kwa uchungu kweli,naona hata wao wenyewe wanaona kinyaa kutangaza kuwa Mhe, alipata ajali alipokuwa anatoka kuchepuka. Wengi wa waheshimiwa wana michekupo huko hatari kabisa, ndio maana kuzungumzia hii mambo kwao inakuwa kama kujiexpose.
 
Kuchepuka kwa mawanaume siyo kashfa kihivyo kwa tamaduni za ngozi nyeusi, kashfa hapo ni kutumia gari ya umma ndivyo sivyo, huenda ni katika utaratibu wa mabaharia kulindana huwezi jua.
 
Gari ya waziri
 
Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais (Tamisemi), Dk Festo Dugange amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Benjamin Mkapa mjini Dodoma akipatiwa matibabu baada ya kupata ajali ya gari

Habari za uhakika ambazo Mwananchi limezipata, zinaeleza Dk Dugange alipata ajali hiyo usiku wa kuamkia Aprili 26, 2023. Hata hivyo, mpaka sasa si Jeshi la Polisi wala viongozi wa wizara yake waliokuwa tayari kuthibitisha kuhusua ajali ya kiongozi huyo.

Licha ya jitihada za Mwananchi kuwatafuta Waziri wa Tamisemi, Angellah Kairuki na Naibu wake, Deo Ndejembi pamoja na Msemaji wa Serikali, Gerson Msigwa lakini, hakuna aliyekuwa tayari kuzungumzia taarifa hizo.

Hata hivyo, akihutubia wananchi wa Wilaya ya Chamwino, Dodoma kwenye uzinduzi wa majengo ya Jeshi la Zimamoto Aprili 26, 2023, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliwaambia mbunge wao Ndejembi hakuhudhuria hafla hiyo kwa sababu alipewa jukumu la kumuuguza naibu waziri mwenzake aliyepata ajali.

"Ndugu wananchi, naleta salamu nyingi kutoka kwa mbunge wenu Ndejembi (Deo) alitamani kuwa nanyi hapa, lakini tumempa jukumu la kuangalia matibabu ya naibu waziri mwenzake alipata ajali Jana," alisema Majaliwa bila kumtaja naibu waziri huyo aliyepata ajali.

Taarifa za uhakika ambazo Mwananchi limezipata kutoka hospitalini hapo, zinaeleza Dk Dugange ambaye ni mbunge wa Wanging’ombe, mkoani Njombe alifikishwa hospitalini akiwa mahututi na kwa sasa hali yake inaendelea vizuri.

"Ni kweli majeruhi tuliyenaye ni Dk Dugange, alifikishwa hapa akiwa kwenye hali mbaya lakini tunamshukuru Mungu kwa sasa anaendelea vema," kilisema chanzo chetu.

Source: Mwananchi
My Take:
Waziri mkuu anashiriki ktk upuuzi km huu? Bila wamwondoe mtu wao kimya kimya anaeenda kuhudumiwa na waziri mwingine?. Mtu aliyefanya jambo la aibu km lile? Nimechoka na viongozi wa nchi hii.
Tuna viongozi kweli nchi hii, halafu bila haya wanaongelea maadili, nimemdharau huyu waziri mkuu mpaka basi. Wanahabari fichueni ujinga huu usikike kimataifa tuhakikishe huu kijana asiye na maadili harudi kwenye uongozi wa nchi yetu.
Hili hata wafiche vipi litajulikana tu. Hii inadhihirisha utaratibu wa kupata viongozi Tanzania una shida mahali.
 
Kama ni kweli basi anangojewa apone tu kisha wanakula kichwa. Mama ni muungwana hawezi kumtumbua mgonjwa.

Ingekuwa enzi za mzalendo Ngosha basi unaliwa kichwa ukiwa na mabandeji yako usoni, hakuwa na mzaha.
 
Kuna mkeka tangu Dec umetiki lakini jamaa wa Betting wameuzuia Hadi Leo tatz sijui ni nn.
 
Kama ni kweli basi anangojewa apone tu kisha wanakula kichwa. Mama ni muungwana hawezi kumtumbua mgonjwa.

Ingekuwa enzi za mzalendo Ngosha basi unaliwa kichwa ukiwa na mabandeji yako usoni, hakuwa na mzaha.
Shujaa hakuwa na Muda wa kupoteza!
 
Back
Top Bottom