Usirudie Dhambi Lisije Likakupata Jambo Baya Zaidi

Samson Ernest

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2014
Posts
1,237
Reaction score
1,744
Yn 5:14 SUV
[14] Baada ya hayo Yesu akamkuta ndani ya hekalu, akamwambia, Angalia, umekuwa mzima; usitende dhambi tena, lisije likakupata jambo lililo baya zaidi.

Matatizo mengine tunayafungulia mlango wenyewe, mlango ambao unaingiza kila tatizo la kutuumiza kiroho na kimwili.

Tunaweza kufikiri magonjwa tunayougua ni magonjwa ya kawaida kama mengine, ila mengine yanatokana na kujitenga na Mungu kwa matendo yetu maovu.

Jambo hili sio geni kwetu, tumeona watu wakipimwa na kukosekana ugonjwa wanaoumwa, au mtu anajulikana shida yake ila akipewa dawa za kutibu hilo tatizo haliponi, hata kama atabadilisha kila dawa.

Matatizo mengine hayapo kimwili tu, yapo mpaka kiroho, unaweza kuhangaika kutibu kimwili hilo tatizo likashindikana kupona.

Tunajifunza kwa mgonjwa huyu aliyeponywa na Yesu, alipewa tahadhari ya kutorudia kufanya dhambi tena.

Ikiwa angerudia kufanya dhambi, lingempata Jambo baya zaidi ya Mwanzo, hili suala halikupaswa kuchukuliwa kawaida, lilipaswa kuchukuliwa kwa uzito mkubwa kama ilivyo leo hatupaswi kulipuuza.

Tunaweza kukimbilia uponyaji wa ki-Mungu, hili tunalifanya tulio wengi, tunakimbilia miujiza ya uponyaji kuliko kuwa na uhusiano mzuri na Mungu, tukishaponywa tunarudi kwenye maisha yetu ya dhambi.

Mara nyingi hali zetu huwa mbaya zaidi ya Mwanzo, huwa tunaanza kufikiri hatukupata msaada wa Yesu, kumbe baada ya kupata uponyaji tulirudia maisha yetu ya dhambi.

Kama nilivyoanza kusema, si kila ugonjwa ni wa kawaida, magonjwa mengine yanaonekana ni ya kawaida lakini huwezi kuyatibu na dawa za hospital, isipokuwa yatapona kwa Jina la Yesu tu.

Yupo atazunguka kwa waganga wote wa kienyeji, huo ugonjwa hutokaa upone kwa sababu ya matendo yake maovu, na kwenda kwa huko ni kudhidi kujichafua zaidi.

Ukiombewa ukapona, iwe ni mapepo au ugonjwa wowote ule hakikisha hurudii maisha ya dhambi, hiyo ndio itakuwa salama yako.

Sio hivyo tu, tuepuka maisha ya dhambi, kwa sababu ni mlango wa magonjwa/matatizo mengi katika maisha yetu.

Soma neno ukue kiroho
Liwe jua iwe mvua soma biblia na kutafakari
Mungu akubariki sana
 
Ahsante Sana mtumishi
 
Asante mkuu!
Question
Hivi
Petro alipomkana YESU mara 3 alitenda dhambi tena au ilikuwaje maana alikuwa amesha ambiwa yajayo yatakayotokea ila akapinga!
 
Alitenda dhambi, ila alipokumbuka alilia sana kwa kutubu;

Mathayo 26:75 – "Ndipo Petro akalikumbuka lile neno alilosema Yesu, ya kwamba, Kabla jogoo hajawika, utanikana mara tatu. Akatoka nje, akalia kwa uchungu."
 
Sin is an imaginary disease invented by religions to sell imaginary cure.

It's like creating virus in order to sell Anti-virus.

Ili uweze ku control na kuwapiga watu hela ni lazima uwaambie wao ni wadhaifu na wadhambi, wanahitaji kutakaswa kwa maombi, maungamo na sala ambazo zinasindikizwa kwa SADAKA.

Sadaka ambazo ni Hela za kunafaisha wachungaji, manabii, mapadri na viongozi wa kidini.

HAKUNA DHAMBI.

DHAMBI NI KICHAKA CHA MANABII WANACHOTUMIA KUJIFICHIA KUIBA NA KUPIGA PESA ZA WAUMINI MABOYA.

HASA WAAFRIKA WAFIA DINI MANYUMBU YASIO SIKIA.
 
Una hitaji maombi mkuu
 
Tumeambiwa tusirudie dhambini sijui mleta mada amesahau kuwa kuna addiction ambayo huwezi kuitoa kwa utashi wa kibinadamu mpaka nguvu ya roho mtakatifu
Ni kweli mkuu mimi kuna dhambi iliniwia vigumu kuacha tuporngraph yani ni kama nilikuwa na pumzika tu then narudi mzgoni ila namshukuru MUNGU amenisaidia, so hatutakiwi kurudia dhambi maana mlango wa rehema unaweza ukafungwa!
 
Hata mi pia hii dhambi ilinitesa sana mpaka walipofungia ikawa ponapona yangu
 
Kwa kizazi hiki kama kuna kijana hajacheki hizi issue APEWE MAUA YAKE! kwani wewe ulianzaje mkuu na ukashinda vq
Simu simu simu madhara ya kushika simu katika umri mdogo tena wa balehe kuacha ni kujikeep buzy na usiwe addicted na simu jitahidi usiwe online hata mwezi mzima nunua bando kama kuna ulazima tu
 
Back
Top Bottom