Yn 5:14 SUV
[14] Baada ya hayo Yesu akamkuta ndani ya hekalu, akamwambia, Angalia, umekuwa mzima; usitende dhambi tena, lisije likakupata jambo lililo baya zaidi.
Matatizo mengine tunayafungulia mlango wenyewe, mlango ambao unaingiza kila tatizo la kutuumiza kiroho na kimwili.
Tunaweza kufikiri magonjwa tunayougua ni magonjwa ya kawaida kama mengine, ila mengine yanatokana na kujitenga na Mungu kwa matendo yetu maovu.
Jambo hili sio geni kwetu, tumeona watu wakipimwa na kukosekana ugonjwa wanaoumwa, au mtu anajulikana shida yake ila akipewa dawa za kutibu hilo tatizo haliponi, hata kama atabadilisha kila dawa.
Matatizo mengine hayapo kimwili tu, yapo mpaka kiroho, unaweza kuhangaika kutibu kimwili hilo tatizo likashindikana kupona.
Tunajifunza kwa mgonjwa huyu aliyeponywa na Yesu, alipewa tahadhari ya kutorudia kufanya dhambi tena.
Ikiwa angerudia kufanya dhambi, lingempata Jambo baya zaidi ya Mwanzo, hili suala halikupaswa kuchukuliwa kawaida, lilipaswa kuchukuliwa kwa uzito mkubwa kama ilivyo leo hatupaswi kulipuuza.
Tunaweza kukimbilia uponyaji wa ki-Mungu, hili tunalifanya tulio wengi, tunakimbilia miujiza ya uponyaji kuliko kuwa na uhusiano mzuri na Mungu, tukishaponywa tunarudi kwenye maisha yetu ya dhambi.
Mara nyingi hali zetu huwa mbaya zaidi ya Mwanzo, huwa tunaanza kufikiri hatukupata msaada wa Yesu, kumbe baada ya kupata uponyaji tulirudia maisha yetu ya dhambi.
Kama nilivyoanza kusema, si kila ugonjwa ni wa kawaida, magonjwa mengine yanaonekana ni ya kawaida lakini huwezi kuyatibu na dawa za hospital, isipokuwa yatapona kwa Jina la Yesu tu.
Yupo atazunguka kwa waganga wote wa kienyeji, huo ugonjwa hutokaa upone kwa sababu ya matendo yake maovu, na kwenda kwa huko ni kudhidi kujichafua zaidi.
Ukiombewa ukapona, iwe ni mapepo au ugonjwa wowote ule hakikisha hurudii maisha ya dhambi, hiyo ndio itakuwa salama yako.
Sio hivyo tu, tuepuka maisha ya dhambi, kwa sababu ni mlango wa magonjwa/matatizo mengi katika maisha yetu.
Soma neno ukue kiroho
Liwe jua iwe mvua soma biblia na kutafakari
Mungu akubariki sana