Usiruhusu mwanaume kuhamia kwenye nyumba yako uliyojenga kwa jasho lako

Usiruhusu mwanaume kuhamia kwenye nyumba yako uliyojenga kwa jasho lako

mwanaume unamshauri afanyaje aruhusu kumuingiza kwenye nyumba aliyoijenga au sio?
Baada ya kuoa muingize kwenye nyumba yako uliyojenga kwa jasho lako, ni mkeo huyo na wewe ni kichwa cha familia.

Ikiwa hujajenga mpeleke kwa nyumba ya kupanga mkaanze maisha ya pamoja kwako.
 
Kwa hiyo,umeona una akili sanaaaa! Hao wanawake wenye hizo nyumba,wanapowapeleka hao wanaume unaowalalamikia kwao,unapungukiwa nini? Hawana akili mpaka uwakumbushe? Wewe ulijiona wa maana,mshikaji kakuchezea sana,umeona leo mzigo uje uutwishe JF! Komaa
 
Kwa hiyo,umeona una akili sanaaaa! Hao wanawake wenye hizo nyumba,wanapowapeleka hao wanaume unaowalalamikia kwao,unapungukiwa nini? Hawana akili mpaka uwakumbushe? Wewe ulijiona wa maana,mshikaji kakuchezea sana,umeona leo mzigo uje uutwishe JF! Komaa
Huu uzi ni special Kwake Ke, povu la nini bwashee ?
 
Mwanamke Usiruhusu Mwanaume Kuhamia Nyumbani Kwako...

Ukiamua kuolewa usimruhusu ahamie kwako, hata kama unamiliki jumba la kifahari katika soko la juu halafu huyo jamaa anaishi katika nyumba ndogo ya kupanga, ni heri ujishushe daraja na utoke kwa jumba lako la kifahari na uhamie katika kijumba chake hicho muishi hapo hadi mnunue au mjenge nyumba yenu pamoja.

Kuna sababu tatu za kutomruhusu ahamie kwako …

1. Mwanamume anayehamia kwenye nyumba ya mwanamke hukimbia wajibu.

Kwa kawaida mwanaume anayejua wajibu wake huchukua hatua kabla ya kuoa.

Hutayarisha makao ya bibi-arusi wake kabla ya kumpata huyo bibi-arusi.

2. Ikiwa unaweza kumudu kumiliki nyumba halafu mwanaume unayeishi naye hawezi kumudu kumiliki nyumba basi yeye sio saizi yako.

Akihamia kwenye nyumba yako ipo siku mtaingia katika ligi ya kupigana juu ya nani anayedhibiti nyumba.

Hivyo achana naye mwache aende akapate mwanamke wa saizi yake.

3. Ikiwa mwanamume atahamia nyumbani kwako, matarajio yake makuu ni kulelewa na wewe, atakufanya uwe mtoaji wake kwa kila kitu. Muda si muda, hutamheshimu tena, yeye pia hata kupenda tena.

Katika dunia ya sasa wanawake hawawezi kujisalimisha kwa wanaume ambao hawatoi.

NB: ujumbe huu ni kwa wanawake wote ambao hawajaingia ktk ndoa, ila kwa wale waliopo ktk ndoa na wanaishi na hao wanaume majumbani kwao huu ujumbe hauwahusu, wakomae tu na waume zao wazembe.
Wanataka usawa hebu tufafanulie kwanza tuelewe
 
Back
Top Bottom