Usisomeshe mtoto shule za gharama kwa matarajio kwamba atapata ajira, utaishia kuumia tu

Usisomeshe mtoto shule za gharama kwa matarajio kwamba atapata ajira, utaishia kuumia tu

Mtoto akifika darasa la7 anajua kusoma na kuandika hiyo elimu inamtosha sana, muachishe shule, peleka chuo cha ufundi veta ama college yoyote akasomee kwa vitendo, akitoka hapo tyr ana ujuzi na anauwezo wa kuanza maisha yake, mtaftie mtaji na urith mapema, then fanya kunawa mikono maana kazi yako kwake unakuwa umeimaliza kama mzaz.

or otherwise kama unajua una connection ya mwanao kwenda kufanya kaz ktk nchi za kigeni ama biashara basi msome izo english medium mpka form4 then achisha shule mpeke short coz ya ujasiliamali miez3-6 then baada ya hapo mkatie urithi wake na mtaji wa kuanzia maisha..

tusiish kwa kukalil maisha kuwa hii mifumo nikama misaafu kwamba huruhusiw kuibadiri ama kufikil nje ya box.

mim nkifanikiwa kupata mtot bas atasoma kwa bata sana, yaan hata shulen atakuwa akienda mara moja kwa wiki, eeh mara moja maana sitaki aende kusomea ajira, bal akasomee kujua kuandika na kusoma tu chazaid akachangamshe akili na watoto wenzake huko, hata mtian wa darasa la7 sitotaka aufanye, maana nikumpotezea muda.

Tuish kiuhalisia jmn maisha ni mafupi why tuteseke?
View attachment 2015279
Kumbe mtoto mwenyewe huna bado???😁😁
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Sijakataa kuwa connection ni muhimu. Ukiwa na ufundi wako, ukishuhudiwa kuwa mchapa kazi na kijitengenzezea jina kwa kazi zako, ukiishi vizuri na watu na kuwa na watu wa kuku support (mf. Family) connection zinatokea naturally. That's the mentality nataka mwanangu awe nayo. Just build yourself and be a good human being.

Kinachonipa ukakasi ni hiyo mentality kwenye huo mfano wa Mo Dewji ulioutoa. I guess it's so ingrained in you you don't see any problem with it.

Wangapi wamesoma na Mo Dewji na wangapi "wametoka" kupitia Mo Dewji kwasababu tu walikuwa class mates?

Ndo tofauti ya mwanao na mwana wa Mo Dewji. Mwana wa Mo Dewji kasoma akiwaza miradi ya baba yake. Mwanao kasoma akiwaza ana connection na mtoto wa Mo Dewji. 😄😄.

Lakini vyovyote vile Kila mtu apambane tu anavyoona yeye. Hii topic ya mambo ya pesa ni complex, we are all making many assumptions and hasty generalizations here, na me sio mtaalam wa haya mambo.

Maana pia kuna watu ambao kwenda shule ni by the way but they have the money to survive lavishly without holding a finger up for the rest of their lives to the next generation.
Maisha connection Ni lazima haikwepeki mfano ukiwa na duka la jumla connection kwenye business world lazima ukiwa na hotel watu uliosoma nao Wenye power kifedha etc wakiwa na shughuli yao waweza kuja kutumia ukumbi wako nk

Umesoma na watoto wa Bakhresa ukajenga urafiki una kituo Cha mafuta waweza pata tenda ya ku supply mafuta kwenye magari na meli zake kupitia hap ulisoma nao

Dunia nzima ziko elite schools na universities ambazo elites watoto wao husoma Bei zake sio za kitoto lakini waweza build network ya kuaga umaskini for good

Mfano umesoma na mtoto wa Mo Dewji mwanae kampa u director of marketing wewe uliyesoma naye Kama ulijenga urafiki aweza kukuteua kuwa sole agent wa kuuza bidhaa zao mkoa wako bila kununua bidhaa cash ukapewa mzigo ukauza ukaulipa sababu anakujua toka mko shule Huna connection hata biashara tu itakusumbua Sana Na sio any connection Ni connection with the right people kwa muda mrefu na muda huo sehemu nzuri ya kupata Ni shuleni mkisoma pamoja

Life is not a lonely planet you need somebody to be somebody

Mzazi utake usitake hiyo kazi na Zigo la kujua mwanao anatakiwa kuwa connected na watoto wa aina gani kwa future yake Ni lako mzazi .Sio la mtoto wewe ndie director wa maisha ya Mtoto.Na kwenye elimu ndio starting point
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Unaongelea hizo shule kudhani ni kwapa kila mtu analo!! hizo shule ni 50 Millions huko na kwa mtu anaetengeneza hizo pesa yupo busy kukagua bank statement na financial statements mda huu, sip kuperuzi jf 😂

Happ ist tu kiwakuta watoto wa tz ni kwa manati

Dua la Kuku halimpati mwewe, pambana na hali yako
 
Sijakataa kuwa connection ni muhimu. Ukiwa na ufundi wako, ukishuhudiwa kuwa mchapa kazi na kijitengenzezea jina kwa kazi zako, ukiishi vizuri na watu na kuwa na watu wa kuku support (mf. Family) connection zinatokea naturally. That's the mentality nataka mwanangu awe nayo. Just build yourself and be a good human being.

Kinachonipa ukakasi ni hiyo mentality kwenye huo mfano wa Mo Dewji ulioutoa. I guess it's so ingrained in you you don't see any problem with it.

Wangapi wamesoma na Mo Dewji na wangapi "wametoka" kupitia Mo Dewji kwasababu tu walikuwa class mates?

Ndo tofauti ya mwanao na mwana wa Mo Dewji. Mwana wa Mo Dewji kasoma akiwaza miradi ya baba yake. Mwanao kasoma akiwaza ana connection na mtoto wa Mo Dewji. 😄😄.

Lakini vyovyote vile Kila mtu apambane tu anavyoona yeye. Hii topic ya mambo ya pesa ni complex, we are all making many assumptions and hasty generalizations here, na me sio mtaalam wa haya mambo.

Maana pia kuna watu ambao kwenda shule ni by the way but they have the money to survive lavishly without holding a finger up for the rest of their lives to the next generation.
Una hoja ila bila kukuficha Africans we are not capable of building family business or brands Asians are good na waweza sababu ya connections kubwa za wao kwa wao sio as a family but as Asians wawe waarabu au wahindi waswahili family tu kukupa connection within the family itself shida Sana hata ku consume tu products zako au services zako as their family member mtihani.Wanapenda out of family products or service s

Halafu waswahili wachuuzi tu viwanda wahindi na waarabu ndio wanavyo na ndio biggest wholesale importers hiyo family business unaijengea wapi bila connection nao?

Ni big challenge but your argument theoretically iko correct

Waswahili piga ua bila connection kutoka kugumu ndio maana biashara nyingi za waswahili hufa au kufanya Vibaya mno akifa aliyekuwa na connections .

Theoretically uko sahihi lakini practically No.
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Kifupi mzazi Kama pesa unazo somesha mtoto shule nzuri usipofanya hivyo iko siku atakuporomoshea matusi ya nguoni mchana kweupe kuwa hukumjali wakati pesa ulikuwa nazo

Watoto ambao wazazi wenu Wana pesa ongeeni kabisa mna haki Kama watoto kuwa mzazi una hela huwezi kunipeleka shule hovyo Kama hii uliyonipeleka hunitendei haki
 
Peleka private ya kawaida shule ya msingi

Kisha mkazanie sekondari asome government
Huu ndio mpango uliopo mkuu ,angalau sekondari atakua mkubwa kidogo ajipambanie
 
Elimu kwa sasa imebadilika, wakati huo vilaza ndiyo waliomba kwenda vyuo kusomea certificates ya fani watakazo - vipanga wote ilikuwa Five Six then baada ya hapo wenye III Advance Diploma na wenye I and II ni Chuo kikuu - wakati huo vyuo vikuu vilikuwa 3 tu, Mlimani, SUA na Muhimbili Medical.

Kwa sasa vyuo vikuu sawa na idadi ya shule zilizopo, na kila chuo kina mchakato wa Certificate hadi Degree, miaka hiyo ukianza certificate mwisho wako utakuwa Advance Diploma, degree hutakaa uione.

Wa advance diploma akitaka kupata Masters Degree ni lazima kwanza asome PostGraduate Diploma mwaka mmoja.

Ni kweli mambo yamebadilika, mtoto anamaliza form four na Div Four lakini baada ya miaka 6 and Degree. Certificate mwaka 1, Diploma miaka 2, na Degree miaka 3.
 
Comment ya Kimaskini sana hii kama roho yako, unamfatilia wa nini Mpaka unajua siku anayosimamishwa Ada kama sio uchawi huo
Hakuna uchawi mkuu,,kila kitu kipo wazi.

Kulikuwa na sababu gn ya kubeba family nzima kusubiri school bus.
Pia kuna sababu gn ya kumficha mtoto asipokwenda shule?
 
Siyo kweli kwa herufi kubwa.
Mkuu fuatilia hili,,mm nimeshajiridhisha kwa hilo.

Now elimu imekuwa ni biashara,,wapo wamiliki wa shule wanatumia juhudi binafsi kuhakikisha shule yake inapata ufaulu mzr ili iendelee kupata wanafunzi wengi na shule kupata soko zaidi...
 
Kwa hiyo pendekezo lako wazazi wapeleke shule za bwerere ambazo hazina mwenyewe kwenye ufaulu wa chini?

Mzazi yeyote atapenda kumpa mwanae kilicho Bora kuanzia nguo zake avae Bora chakula chake ale Bora na elimu yake asome shule Bora
Uwe ufaulu wa kwl sio ufaulu wa bao la mkono
 
Mkuu fuatilia hili,,mm nimeshajiridhisha kwa hilo.

Now elimu imekuwa ni biashara,,wapo wamiliki wa shule wanatumia juhudi binafsi kuhakikisha shule yake inapata ufaulu mzr ili iendelee kupata wanafunzi wengi na shule kupata soko zaidi...
Angalia vitabu vyao , angalia sylabus yao, halafu fuatilia namna wanavyosoma ndipo utagundua kuwa kazi kubwa inafanyika kumjengea mtoto uwezo darasani.

Kawaida hizi shule ylabus inaisha mapema kwasababu ya bidii ya walimu kwenye vipindi.

Baada ya hapo huanza kufanya revision kwa sehemu ambazo ziliwasumbua wanafunzi.
Halafu walimu wana close supervion kiasi karibu kila mtoto wanakuwa wanajua uwezo wake na wapi anakwama na hufanya bidii kusaidia na mzazi pia unaambiwa kuhusu hilo.

Watoto wanasoma sana ndio maana wanakuwa na uwezo mkubwa.

Huyakuti haya kayumba. Sylabus iishe isiishe hawajali.
Mtoto akiwa anakwama sehemu atajua mwenyewe ili mradi aje shule tu.

Kwa nilivyofuatilia mimi nimegundua hizi tofauti.
 
Mkuu nimejiridhisha kuna bao la mkono ktk shule za private.

Niliangalia matokeo ya darasa la 7 2021/2022 kuna shule moja ya private. wamepasi shule nzima
Kwa alama A na B ..wastani.
C wala D..hakuna

Hii aiwezekani na kwa akili ya kawaida ,,
 
Wanasomesha huko ki ufahari na ulimbukeni tu waonekane wana hela na pia watoto wao wajue english, kumbe hakuna lolote huko. Kama mtoto ana akili, ana akili tu hata akisoma shule za kawaida atafaulu
Tatizo lako Unadhan shuleni ni elimu tu... Tunaangalia na malezi... Shuke Ina darasa lenye wanafunzi 400 afu na wew una peleka mwanao huko....
Ya nin Wakati umejaliwa hela ya ada?
Nita peleka kwenye darasa la wanafunzi 50.
Hela kwangu haina maana kama nitamtesa mwanangu
 
Mkuu nimejiridhisha kuna bao la mkono ktk shule za private.

Niliangalia matokeo ya darasa la 7 2021/2022 kuna shule moja ya private. wamepasi shule nzima
Kwa alama A na B ..wastani.
C wala D..hakuna

Hii aiwezekani na kwa akili ya kawaida ,,
Kama uliielewa topiki ya probability mambo ya sample space Huwezi tikia shaka. Tena primary?

What abt f4 shule Ina dv 0ne Za singo digit tu?
 
Kumekuwa na tabia ya baadhi ya wazazi wakisomesha watoto wao shule za gharama za private toka chekechea, msingi, o level na advance mpaka chuo kwa mategemeo kwamba watakuwa na ajira zenye malipo ya juu, watoto wakimaliza chuo hawana ajira aua ajira zinakuwa za chini, kwa o yanageuka kuwa maumivu:

Nimekuwekea hapa mbinu za kumsombesha mtoto wako kwa gharama nafuu na kupata elimu sawa na wale wanaoenda private

SHULE YA MSINGI - Hapa lengo kuu la kupeleka watoto shule za private huwa ni mtoto ajifunze kiingreza, piga ua galagaza somesha mtoto wako shule za mitaala ya kiingereza kwa sababu akifika sekondari na chuo atatumia lugha ya kiingereza, kuna shule za english medium zinakidhi kila kitu kutekeleza hili, hakuna aja ya kulipia mamilioni kwenye shule za private, Mwanangu kamaliza darasa la tatu saizi anaweza kusoma / kusikia / kuongea / kuandika kiingereza kwa level nzuri tu, anaimba miziki ya kiingereza, anaweza kuelewa movies bila tafsiri, n.k. Hata nikimletea mitihani ya kiingereza ya shule kama st mary anabutua vizuri kabisa.

SHULE YA SEKONDARI - Hapa mtaji wa kujua lugha ya kiingereza unahitajika sanaili kumpiga jeki asome kwa urahisi, Hapa nasihi sana asome shule ya day, aidha iwe ni shule yenye walimu wa kutosha na inafanya vizuri mitihani ya taifa iwe ni shule ya serikali aliyochaguliwa au hizi shule za umoja wa wazazi ambazo mara nyingi hazizidi laki 4.

Binafsi enzi zangu wazazi wangu walinipeleka shule za boarding za gharama kwa sababu wazazi wenzao wengi walifanya hivyo (mkumbo) pia wakiamini kwamba ndio ntajifunza maisha na kuepukana na vishawishi, Mimi muhusika nilieenda huko nlikutana na hali tofauti kabisa, ukiwa mlegevu utaonewa, ukiwa mtu wa makundi utavuta bangi, kulikuwa na mashoga, n.k. watoto wa ma rpc, majaji, wabunge, wakurugenzi wa taasisi, n.k walikuwepo. Kuna ile dhana ya kwamba mtoto aende huku kwa lengo la kupata marafiki wazito, hii nayo siwezi kuipa uzito maana kuna watoto wa vigogo walikuwa wakikuona unawalamba lamba wananyanyasa sana wenzao na kuwafanya kuwa watumwa.

Kiufupi mambo ya boaring hayana sana umuhimu kwa sasa, baki na moto wako nyumbani, Siku hizi kuna vitabu vya maswali na majibu vya kumuandaa mwanafunzi kujua kuyajibu kwenye chumba cha mtihani, Tuition zipo kibao nyingi sana, mtoto anafeli vipi???

FORM 5 NI TAKATAKA PELEKA CHUO - Kuliko kujiminya kumsomesha mtoto shule ya milioni 2 ni heri umpeleke chuoni kwa milioni 1 aanze kujifunza taaluma yake mapema, hata serikali yenyewe huwa inatoa selection chache sana mithiri ya bahati nasibu kuwafadhili wanafunzi kwenda kusoma vyuoni, hii ni sababu tosha kwamba chuoni ndio kuna elimu bora kuzidi form 5.

Nakumbuka hata nilivyomaliza form 6 na kuingia chuo, wale watu waliosomea certificate na diploma badala ya kwenda form 5, kwao karibu kila kitu kilikuwa ni marudio, maisha ya uhuru wa chuoni walikuwa wameshayazoea, walikuwa tayari wameanza taaluma zao mapema huku sisi tunasomea kombi, walikuwa wameshafanya mazoezi ya kazi kwa vitendo huko maoofisini kuvimbishia cv huku sisi ni weupe, vyeti vyao vilikuwa vina hadhi ya kuajiriwa serikalini wakati sisi na vyeti vyetu vya form 6 hata kiwe na division 1 hupati ajira, n.k. Pia nao wanapata mikopo kama waliomaliza form 6.

VITABU - Hakikisha mtoto wako anasoma vitabu kwajili ya elimu binafsi, kuna vitabu kama rich dad poor dad, How to make friends and influence people, n.k hakikisha anasoma hivi, Mwanangu napanga aanze kusoma hicho cha how to influence people mwakani. vitabu ni resource muhimu zaidi, ajabu ni kwamba kuna wahitimu wengi wa vyuoni hawajawahi hata kujisomea kitabu kimoja

Kwa mtinfdo huu utaweza kupunguza gharama
Umepotoka
. 1. Hatusomeshi mtoto ili apate ajira.
2. Shuleni ni zaidi ya elimu.. Si kama unavodhani
3. Sampling yako umefanya utafiti kwa mwanao tu then Unataka ugeneralize
4. Kesho njoo na hoja Za hosptal binafs watu wasiende kutibiwa huko kwa kuwa ni gharama
 
Mkuu nimejiridhisha kuna bao la mkono ktk shule za private.

Niliangalia matokeo ya darasa la 7 2021/2022 kuna shule moja ya private. wamepasi shule nzima
Kwa alama A na B ..wastani.
C wala D..hakuna

Hii aiwezekani na kwa akili ya kawaida ,,
Upo sahihi
 
Back
Top Bottom