Usitafute Sifa Ukweni. Wanakusanifu

Usitafute Sifa Ukweni. Wanakusanifu

Wakwe na ukweni sio mahali pa kupazoea ovyo. Nenda huko kwa sababu muhimu na maalumu, wasiliana nao kwa sababu muhimu, sio kila siku unanyanyua simu kumpigia mama mkwe, kila holiday wewe ni kwa wakwe tu...

..halafu mkwe hakopeshwi, aliomba kiaina, hukujua ukatoa mkopo, pole sana!
 
Uliyeoa "Mgombani" usijidai kutaka point 3 ukweni eti unasaidia shemeji sijui wakwe, utaumbuka mapema asubuhi. Jiimarishe kwenu! Mgombani hawanaga shukrani.

NB: Yamemkuta rafiki yangu kaoa Palestina, kachangia ujenzi wa nyumba na Kuna kipindi Mama mkwe aliomba akopeshwe 7m eti akipata pensheni atamrudishia mpaka leo hamna kitu. Jamaa kwao Dodoma (Bahi) bado wazazi wake wanalala nyumba ya Tembe!
*Jamaa Ndoa imevunjika anadai Chake (Deni 7m) wamemtoa nduki.

**USISEME HUKUTAHADHARISHWA MAPEMA.
NOTE: Inasemekana ANTENNA adimu Sana huko.
Ukweni sio nishaapa hakuna ndugu wa mke atakuja na shida mm nitoe pesa yangu mfukoni kumpa kuna shemeji yangu dada wa wife alinionba nimkopeshe laki 1 atanirudishia baada kama ya siku 3 mbele ebwanaaeee nkaingia kingi nkampa ndo mpaka leo mwaka wa pili huu tena kajikausha kama hakijatokea kitu nkasema anhaaaa ook kumbe hivyo tu jambo dogo sanaaa tangu siku hiyo ndugu zake wife wote atakaeomba msaada wa kipesa basi anaambulia ushauri
 
Back
Top Bottom