Steven Joel Ntamusano
JF-Expert Member
- Jun 17, 2023
- 5,203
- 3,913
Kwenye masuala ya uongozi kuna kanuni moja muhimu sana isemayo ' usitake kumfunika boss wako'.
Kwa kingereza wanasema 'never outshine your master', anayekuapisha daima ni mkubwa wako wa kazi hata kama nafsi yako inakuambia kwamba wewe unamzidi maarifa na kila kitu. Siku zote jifanye mjinga kwa mtu anayekupa mshahara na kukufanya ukaonekana na kuthaminika.
Hiyo kanuni imekuwa ngumu kwa Mheshimiwa January Makamba, ni mtu mwenye kujitutumua kila anapopata nafasi kiasi cha kusahau matendo yake yanaonekana vipi kwa wakubwa waliomuapisha pale ikulu.
Kuna lile suala la kutokuelewena kati ya mamlaka ya anga ya Tanzania TCAA na mamlaka ya Anga ya Kenya. Na mkurugenzi wa mamlaka ya Tanzania akawaandikia wale wa Kenya kuhusu umuhimu wa kufungua anga lao kwa biashara zetu kwa mujibu wa taratibu za anga za kimataifa.
Ni suala ambalo kwa namna yoyote ile barua iliyotoka upande wa Tanzania ilikuwa imetosha kuwakumbusha majirani juu ya kupunguza kiburi na dharau katika sekta zao, na kwa namna yoyote ile lisingeweza kuvuka siku tatu bila ya ufumbuzi kuwa umepatikana.
Na ilikwishatokea hivyo hivyo wakati wa awamu ya tano na mawaziri wa mambo ya nje wa Kenya na Tanzania wakaliachia limalizwe katika ngazi za wakurugenzi bila ya wao kulazimika kuingilia kati.
Safari hii katika awamu ya sita Mheshimiwa Makamba akaona ni sehemu ya 'kutokea', akaona ni nafasi ya kuchukulia ujiko kwa bosi wake. Akaamua kuingilia kati akimhusisha waziri wa mambo ya nje wa Kenya. Hakujua kwamba ameikera ofisi iliyomteua na kumwapisha kiasi cha mwenye ofisi kuwapigia simu wahusika akimshangaa waziri wa mambo ya nje kwa namna alivyoingilia suala lenye kutakiwa kumalizwa katika ngazi za chini.
Kingine kilichomkera SSH ni kuona kwamba hilo ni suala la wizara ya uchukuzi na mawasiliano na hapakuwa na haja ya wizara ya mambo ya nje kutumia nguvu kubwa kwenye utatuzi.
Tatizo la mheshimiwa ni kujiweka katika haiba ya urais akidhani anasubiri tu muda ufike aapishwe pale ikulu. Anaishi na tatizo hili akilini mwake na hajijui kuwa analo.
Wazungu wanasema ' never outshine your master'.