Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 33,679
- 49,841
Fanya uhusiano na mtu anayekupa mawazo ya kusonga mbele kiutafutaji; sio unatengeneza mahusiano na mtu muda wote ni kukupiga mizinga tu; mara hela ya kodi imeisha, mafuta ya gari, mtaji n.k . Siku utakaposhindwa kumuhudumia kwa hayo mahitaji yake, ndio utakuwa mwisho wako wa kuwa naye, kwa sababu amekufanya wewe kama kikoba kisichokuwa na marejesho.
Nilishajiwekea mipaka binafsi, kama mtu ninayetaka kuingia naye kwenye mahusiano anapenda sana kupiga mizinga; huwa nampiga chini mapema kabla hayajanifika shingoni. Kwa sababu anakuwa hana mawazo mbadala ya kukuwezesha wewe kusonga mbele, zaidi ya kukudidimiza.
Sasa ukimuuliza swali, zaidi ya tendo unafaida gani kwangu? Anaweza akashindwa kukujibu kwa kuliona swali kuwa gumu.
Ni wewe tu uchague; uendelee kupigwa mizinga mpaka uchanganyikiwe au ujihadhari mapema kabla ya kupauka kutokana na mizinga iliyokomaa na kuwa makombora.