Usithubutu kumshirikisha Ndugu kwenye Mafanikio yako, Utajuta. Yamenikuta

Miss Natafutwa

Senior Member
Joined
Dec 18, 2024
Posts
190
Reaction score
593
Imeandikwa na mdau toka Mbeya:-

Nilifungua Mini-Supermarket mahali ili kujikwamua kiuchumi.
Nikaona si mbaya kumshirikisha ndugu yangu wa kike wa damu wa kuzaliwa tumbo moja mafanikio yangu ili siku moja moja naye anaweza kuja kuniungisha kununua mahitaji hapa kwangu.

Alichokuja kunifanya huwezi amini.
Kila nikipost nimeleta bidhaa mpya katika page ya duka langu kule instagram nakutana na comment moja huwa inasema "wateja msijisumbue kwenda kwenye hiyo supermarket kwani bidhaa nyingi zilizopo humo ni expired . Nlikuwa mteja wake ila nimemuhama"

Ilikuwa kila nikipromote duka langu instagram nakutana na comment hio mara kwa mara na sikujua cha kufanya na wala sikumjua muhusika.

Mungu bwana hamfichi mja wake.

Siku hiyo nikakuta hiyo account inayonichafua iko tagged na account ingine ninayoifahamu kwenye page ingine. Ikabidi niende Dm kwenye hio page ingine ili nimuulize kama anaifahamu hiyo account inayonichafua na akasema anaifahamu kwani ni mtu anayemfahamu.

Nikaanza kujenga urafiki na hio account ili aje kuniambia huyo anayenichafua ni nani ila sikufanikiwa. Kwa kuwa account hiyo inayonichafua ilikuwa iko private ikabidi nifungue account ingine nijifanye mwanaume kisha niombe kumfollow huyo anayenichafua. Ile kunikubalia, katika kufungua picha nakuta ni yule ndugu yangu wa damu kumbe ndie aliyekuwa ana ni trush kule kwenye supermarket yangu.

Nikazama Dm kwake na kumuomba namba na baada ya kunipa sikuamini kwani sauti ni ya ndugu yangu kabisa (ilibidi niombe msaada wa rafiki yangu wa kiume ili kuongea sauti ya kiume)
Na mpaka picha aliyonitumia ni yake na amepiga nyumbani tunapoishi.

Niliishiwa nguvu na kulia sana.

Japo mpaka sasa sijamwambia lolote kuhusu yale maneno ya kuikashifu supermarket yangu kule kwenye page yangu.
Naumia kuona ndugu yangu wa damu akipambana mimi nianguke kiuchumi.
Nimeumia mno.

USIMSHIRIKISHE NDUGU KWENYE MAFANIKIO YAKO HATA SIKU MOJA. ACHA AJE AJIONEE MWENYEWE SIKU IKIFIKA.
 
Well pole sana kwa yaliyokukuta, nilikuwa kwneye viatu vyako miaka fulani, hakuna btrayal inauma if family au family member ndio wana ku betray, behind your back

It is so painful. Lakini pia ni somo, one thing najua from that experience huta feel normal about huyo ndugu, hata abadilike vipi
 
Ogopa sana Teknologia

"Habari wana Jf kwa ujumla.
Sina muda mrefu tangu nijiunge na jumuia hii chini ya kaka Max.

Ni hivi, napitia msongo mkali sana wa mawazo yaani nikisema ni mkali namaanisha.

First of all nilikuwa muajiriwa serikalini na likapita suala la vyeti feki hapo nilikuwa natumia cheti cha mtu na kazi ikawa ndio basi.

Sababu nilipoteza wazazi ikabidi ile akiba niliyojiwekea kipindi nafanya kazi niitumie kwa ajili ya kumsomesha mdogo wangu ambae niliachiwa na wazazi pamoja na kununua kiwanja tu. Hali ikazidi kuwa mbaya zaidi, ikabidi niingie kwenye kazi ya kujiuza.

Nilichokuwa nafanya ni kumuandalia mdogo wangu sare za shule na pesa ya matumizi usiku ili hata kama nitarudi asubuhi au kama sitarudi kabisa basi apate kujiandaa na kwenda shule (shule na nyumbani ni kama km 1 tu) mwenyewe.

Nilifanya hiyo kazi kwa miaka 6, nikapata pesa na kuanza ujenzi wa nyumba yangu ya kuishi pamoja na mdogo wangu.

Shida imeanza tena, nyumba haijakamilika na pesa zote nimemaliza na mdogo wangu mwaka huu anaingia kidato cha

Sitaki tena kurudi kule nilipotoka (kujiuza). Nahitaji mdogo wangu akue bila kujua nafanya nini. Pia nahitaji kumalizia nyumba

Kama kuna mtu ana uhitaji wa mtu wa kufanya kazi naomba nipewe ajira.

1. Nina diploma ya Education niliyoipata pale UDSM kabla sijatumbuliwa.

2. Nina uzoefu katika kulea watoto na pia ninajua sana upishi (nilisomea hotel management kabla sijaenda kusomea ualimu), Umri wangu ni miaka 42 na niko Morogoro"
 
Itakuwa ni family jina ila haina umoja wala upendo. Kuna family kibao ndugu wanasapotiana na kufanikiwa pamoja.
 
Mtaji wangu wa kwanza umetoka kutoka kwa support ya ndugu na wazazi
 
Rejea visa vifuatavyo ndani ya Biblia.
1. Kaini na Habili.
2. Yusufu na ndugu zake.
3. Yakobo na Esau

Kisha rejea nukuu ya Yesu Kristo aliposema, nanukuu "Adui wa mtu, ni wale wa nyumbani mwake."

Kwa mleta mada, vipi ungemfuma anakufanyia ulogi ili akushushe chini?
 
Pole sana dada kwa changamoto uliyopitia
huyo ndugu yako (tena wa kike) atakuwa na matatizo kwani sio kawaida.
Nafikiri anastaki apelekwe mirembe kwa uchunguzi wa Afya ya akili
 
Ndio hivyo ndugu yangu,wahenga wakisema kikulacho ki nguoni mwako!Wapo ndugu wazuri tumepitia kwao na wabaya wapo!Kazini kwenye Bible alimuua ndugu yake wa damu!Enzi hizo za zale hakukuwa na magari Wala bar Wala Ndege, Sasa hivi maendeleo na maisha yamekamatana,akikuona unafanikiwa,inamuuma sana.Vumilia,chukua hatua hata mtu pia usimuamini,iamini roho Yako tuu na Mungu wako,ila nenda kwa Haki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…