Ogopa sana Teknologia
"Habari wana Jf kwa ujumla.
Sina muda mrefu tangu nijiunge na jumuia hii chini ya kaka Max.
Ni hivi, napitia msongo mkali sana wa mawazo yaani nikisema ni mkali namaanisha.
First of all nilikuwa muajiriwa serikalini na likapita suala la vyeti feki hapo nilikuwa natumia cheti cha mtu na kazi ikawa ndio basi.
Sababu nilipoteza wazazi ikabidi ile akiba niliyojiwekea kipindi nafanya kazi niitumie kwa ajili ya kumsomesha mdogo wangu ambae niliachiwa na wazazi pamoja na kununua kiwanja tu. Hali ikazidi kuwa mbaya zaidi, ikabidi niingie kwenye kazi ya kujiuza.
Nilichokuwa nafanya ni kumuandalia mdogo wangu sare za shule na pesa ya matumizi usiku ili hata kama nitarudi asubuhi au kama sitarudi kabisa basi apate kujiandaa na kwenda shule (shule na nyumbani ni kama km 1 tu) mwenyewe.
Nilifanya hiyo kazi kwa miaka 6, nikapata pesa na kuanza ujenzi wa nyumba yangu ya kuishi pamoja na mdogo wangu.
Shida imeanza tena, nyumba haijakamilika na pesa zote nimemaliza na mdogo wangu mwaka huu anaingia kidato cha
Sitaki tena kurudi kule nilipotoka (kujiuza). Nahitaji mdogo wangu akue bila kujua nafanya nini. Pia nahitaji kumalizia nyumba
Kama kuna mtu ana uhitaji wa mtu wa kufanya kazi naomba nipewe ajira.
1. Nina diploma ya Education niliyoipata pale UDSM kabla sijatumbuliwa.
2. Nina uzoefu katika kulea watoto na pia ninajua sana upishi (nilisomea hotel management kabla sijaenda kusomea ualimu), Umri wangu ni miaka 42 na niko Morogoro"