Environmental Security
Senior Member
- May 21, 2020
- 181
- 262
Hii tabia ya kugoma kutoka madarakani imekita mizizi ndani ya upinzani Lipumba - CUF, Mbatia - NCCR, Mbowe - CDM, na wapinzani wengine, sababu kuu ni kutokuwaamini wengine uwezo wao wa kuongoza vyama hivyo, yaani unataka mtu awe mwanachama afanye mambo yote ya kikatiba ktk chama ila asithubutu kugusa nafasi yako hasa ya uenyekiti.
Japo hii inathibitisha kwa kiasi gani hakuna uwezo wa kuandaa wengine ili kuwarithisha imani ya chama, misingi na majukumu, na kudhihirisha ubinafsi uliopindukia, lakini pia hii ni sababu ambayo inatufanya tuwe makini kuhakikisha kuwa tusithubutu kuwaamini wapinzani, wakiingia madarakani huwa hwawatoki na hawaamini kuwa wenzao wanaweza kuongoza kwa kupokezana.
Huwezi kuamini watu wa hulka ya namna hii.
Karibuni CCM, Tujenge taifa letu kwa pamoja kwa umoja.
"Umoja ni Ushindi"
CCM imara