Usitoe sadaka, umeshatoa

Hivi huko misikitini sadaka kumbe hamtoi

Kuna cha kujifunza hapa, mnajiendeshaje


 
Naunga mkono hoja...

Hakuna kula madhabauni, hata wachungaji nao watafute kazi za kujiingizia kipato..

Siku za ibada tutakutana kumshukuru Mungu kwa tulichokipata kwa sote na sio kutoa masadaka tu...
Wako waumini wana hali ngumu za kimaisha na bado kanisa linawaimize watoe tu hadi senti ya mwisho bila huruma. Na wao wanatoa tu coz brain washed.

Sadaka ni kile unachowapa wenye uhitaji...
 
Kutoa kwa mayatima na wajane ile haitwi sadaka, Yale ni matendo ya huruma. Sadaka ni agizo la Mungu na sio matakwa ya wanadamu.

Ajenda kuu ya waabudu shetani wanajua Sana nguvu ya sadaka, ni propaganda agenda kuwapumbaza waumini waache kutoa Ili waache kubarikiwa, mbona kwa shetani wanatoa zaidi tena ni amri na sio hiari.
 
Mungu achukui sadaka bali sadaka utumika kufanya Kazi za MUNGU duniani kupitia watumishi wa MUNGU. Mtumishi wa Mungu sio hekima akafanye Kazi saa ngapi atahudumia watu kiroho,thus utakiwa kulishwa na waamini.

Mfano unataka huduma za kiroho unafika ofisini unaambiwa subiria Saa moja jioni mtumishi ameenda kibaruani kubeba zege au kufanya kibarua Ili apate pesa aendeshe familia.

Kuwa mtumishi wa Mungu hakuondoi uhitaji wake kama mwanadamu.Pili bill za umeme,maji,simu,nauli, internet,mafundi,malazi na chakula hotelini, mafuta ya gari atakulipia Mungu? Sadaka, zaka, michango ni sehemu ya ibada na ni maagizo ya MUNGU kwa muamini na mapato na matumizi yake uwekwa wazi kwa waumini wote kimaandiko.

Hakuna mafanikio nje ya kutoa usipotoa kwa Mungu utatoa kwa shetani. KWA Mungu unatoa 10% 90 tumia kwa shetani unatoa 60% 40 tumia.

Kati ya kwa Mungu na kwa shetani nani ufanikiwa zaidi jibu ni kwa shetani kwann sababu wafuasi wa shetani wanatoa zaidi kuliko wafuasi wa Mungu. Kwa mganga unatoa ng'ombe kwa Mungu unatoa sh 500.

Waabudu shetani kutwa kuwapotosha Wakristo waache kutoa sababu wanajua nguvu ya kutoa, wanajua kutoa ni ulinzi dhidi ya shetani,
 
SAsa bili za maji,umeme,simu,uinjilishaji,kulipia vipindi vya redio na tv nk utawaambia watoa huduma kachukue pesa kwa Mungu,in common way?
 
Sadaka sio pesa,kwani akitoa mda na nguvu zake uoni ni sadaka pia. Huyo Mchungaji akabebe zege ataandaa Saa ngapi somo la kukufundisheni ninyi siku ya ibada.

Kanisa ni ofisi pia ipo wazi hata zisizo siku za ibada anahitaji kukutana na wenye shida kuwapa ushauri wa kiroho, kutoa huduma za mazishi, kufariji wagonjwa, kufungisha ndoa, bado apokee simu kuwapa faraja, au kuwaombea wahitaji.

Sasa akafanye Kazi kwa Mhindi Saa ngapi huo mda ataugawa.Kazi ya Mungu na Kazi kama Kazi za kusaka kipato haziendani,ni lazima utaegemea sehemu moja.

Thus wengine uona bora kuacha Kazi. Jiulize kwann mapadre awaruhusiwi kuoa chagua moja umtumikie Mungu au uitumikie familia, hivi viwili vinahitaji mda na 24 uwepo wako.
 
Zamani billi za umeme,maji,simu,magari, tv havikuwepo hivi unalipa pesa ulipi mifugo
 
Nadhani mleta mada ungebaki tu kwenye kuwajali wazazi. Hii kusema usitoe sadaka HAIKUBALIKI hata kwenye dini ya mizimu ya Yericko Nyerere. Hata kwenye mizimu wanatoa sadaka. Una hoja nzuri ila umeiharibu mwenyewe.
 
Shida ni hawa mitume na manabii wanaoishi kifahari magari majumba ya kifahari miradi mikubwa walinzi kwann wasiwaendeleze waumini wao masikini mfano kuwajengea uwezo wa kiuchumi jibu ni kwamba wengi wao Wana maagano na kuzimu pesa zao hazitakiwi kusaidia watu.

Wana pesa za mikataba,
 
Mtoto amlipi mzazi bali utoa shukrani na ni ibada pia kumtunza mzazi karma Ili nawe kesho utatunzwa sababu ulipanda mbegu.Huwezi mlipa mzazi gharama alizokulea
 
Hapa umechanganya,Mungu ana nafasi yake na mzazi ana nafasi yake pia.Na KILA mmoja anautaratibu wake wa kupewa.Je wale wazazi wao awapo duniani wakawafate wapi.
 
Mkuu hawa manabii feki ni suala lingine kabisa ambalo ni janga la kitaifa. Pia baadhi ya mafundisho ya kikristo kuhusu sadaka yanachanganya sana. Mfano SDA wanaambiwa 10% ya mapato ni zaka na 10% ni sadaka. Jumla 20% ya mapato yako. Lakini tukumbuka mapato na faida ni vitu viwili tofauti.

Lakini viongozi wanang'ang'ania ukipata 10m utoe 1m bila kujali pale capital & expenses inaweza kuwa labda 9m hivyo 1m ndo unaweza kuitumia. Ukiwaelekeza wanakutolea maneno ya vitisho. Mimi nadhani sadaka zitolewe kwa jinsi mtu anavyoguswa na sio lazima kumpelekea nabii /mtume /mchungaji.

Sadaka kwenye haya mambo ya kiimani haizuliki. Imani zote hadi wale freemason wana sadaka zao.
 
Waabudu shetani awataki Wakristo watoe, Ili wasibarikiwe na kuwekewa ulinzi kusudu waweze kuwateka. Unaweza ukasoma agenda za shetani kwa mwaka 2022 zilizotimia dhidi ya mwanadamu.

Naingia chimbo taweka mkakati wa shetani kwa mwaka 2023 dhidi ya dunia.Ishu kama corona,ushoga nk hizi ni on going agenda. Corona ilikuwa ni ajenda ya 2020
 
Hakuna mafanikio yeyeto iwe kwa shetani au kwa Mungu au kwa nature bila kutoa, Hakuna mganga anaetibu bure ni kinyume na miiko atakula adhabu kali Sana ikiwemo kifo.
 
Kila Mtu na life style yake, na kizuri zaidi maisha hayanaga kanuni unaweza usitoe na ukawa msindikizaji tu wa mafanikio ya wengine miaka nenda rudi [emoji124][emoji1]

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
Nijuavyo Mimi ukitoa unapunguza, lakini jamaa wanakwambia ukitoa unaongezewa, kwanini hasemi ukipokea unapunguziwa?

Kwanini wanapokea zaidi kila siku lakini waumini wanakitoa wanaongezewa. Yaani zinaongezeka kivipi? 20 -5 = 15. Kweli wajinga hawaishi tuendelee kutengeneza vibuyu vyetu.
 
Na mie naongezea "atawaacha baba yake na mama yake......."

Guess will happen
Hapo maana yake ataacha kuendelea kutunzwa na kulindwa na baba na mama yake.... Lakini heshima kwa baba na mama itabaki palepale,
 
Wajinga hawataisha tuendelee kujenga makanisa na misikiti tupate sadaka. Kule china hawaendi kanisani Wala msikitini na idadi Yao ni robo ya watu wote duniani, kwahiyo wanakamatwa na shetani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…