Usitoe sadaka, umeshatoa

Usitoe sadaka, umeshatoa

Hivi huko misikitini sadaka kumbe hamtoi

Kuna cha kujifunza hapa, mnajiendeshaje


Mungu wetu alishatuumba, akawakabidhi wazazi wako wakamilishe mchakato uliobakia wa kukuzaa, kukulisha, kukuvalisha na kukutunza kwa muda fulani kabla na wewe hujaanza kujitunza na kuzaa watoto wengine. Kama ni sadaka mpe mzazi wako anaeweza kuitumia hiyo sadaka sio Mungu, kwakuwa Mungu hana matumizi ya sadaka; fedha, chakula wala mifugo yako maana vitu vyote ni vyake vinatoka kwake na anavyo vingi kuliko baba na mama yako. Wazazi wako wana matumizi, wana mwili, wana mdomo, na wana tumbo, hivyo wanajua nini cha kufanya ukiwapa pesa, nguo, chakula, mifugo. Mungu wetu anataka ushukuru tu na kumsifu kama vile unavyomsifu TOYOTA kwa kutengeneza aina ya gari lako unaloliendesha. Baada ya TOYOTA kutengeneza gari lako kazi yako ni kuisifu toyota lakini sio kutoa zawadi, malipo au kuiomba toyota ikupatie mafuta ya gari lako, ukupakie rangi gari lako wala kulifanyia matengenezo gari lako.

Kuna watu wanapoteza Muda wao mwingi kwa Kuomba Mungu badala ya Kushukuru mungu, Kuna watu wanapoteza mali zao nyingi kwa kutoa sadaka kwa Mungu badala ya kuwapa wazazi wao. Wanakosea sana na hawajui walifanyalo zaidi ya kuwatajirisha watu wanaozipokea mali (sadaka) zao. Mungu hana shida lakini wazazi wako wana shida.

Anza na wazazi wako kwanza uone mambo yako yatakavyokunyookea haraka. Kama kila mtu akihangaika na wazazi wake Mungu atasikia vilio na maombi yao haraka kwakuwa wazazi ndio bomba lako linalopitisha maombi kutoka kwako kupitia kwa wazazi, mababu, mitume, kupitia kwa Adam na Hawa hadi kumfikia Mungu, kwakuwa Adam na Eva wanamfahamu Mungu zaidi kuliko wewe, na babu yako yuko karibu na Adam, baba yako yuko karibu na babu yako, na wewe uko karibu na baba yako. Ndiyo maana kila anaewadharau wazazi na mababu zake hafiki mbali kwakuwa Mungu yuko karibu nao zaidi kuliko wewe.

kila mtu anatoa sadaka kila siku anapomsaidia mtu mwingine jambo, hata kumuonyesha mtu njia, kumpa mtu maji ya kunywa, kumbeba, kumpa chakula au soda, umeshalipa sadaka tayari, lakini mzazi wako ni wajibu sio hiari kumpa sadaka zako.

Sadaka unayotoa haifiki kwa Mungu bali inaliwa tu na wajanga wanaojifanya wanaipeleka kwa Mungu. Tafuta mayatima na wajane wape kama unataka kuwapa, lakini wajali zaidi wazazi wako, utaona mambo na miujiza wasiyoiweza "watumishi wa mungu" unaowapa hela zako kila siku. Unatapeliwa ndugu yangu, fumbua macho yako.
 
Naunga mkono hoja...

Hakuna kula madhabauni, hata wachungaji nao watafute kazi za kujiingizia kipato..

Siku za ibada tutakutana kumshukuru Mungu kwa tulichokipata kwa sote na sio kutoa masadaka tu...
Wako waumini wana hali ngumu za kimaisha na bado kanisa linawaimize watoe tu hadi senti ya mwisho bila huruma. Na wao wanatoa tu coz brain washed.

Sadaka ni kile unachowapa wenye uhitaji...
 
Kutoa kwa mayatima na wajane ile haitwi sadaka, Yale ni matendo ya huruma. Sadaka ni agizo la Mungu na sio matakwa ya wanadamu.

Ajenda kuu ya waabudu shetani wanajua Sana nguvu ya sadaka, ni propaganda agenda kuwapumbaza waumini waache kutoa Ili waache kubarikiwa, mbona kwa shetani wanatoa zaidi tena ni amri na sio hiari.
 
Mungu achukui sadaka bali sadaka utumika kufanya Kazi za MUNGU duniani kupitia watumishi wa MUNGU. Mtumishi wa Mungu sio hekima akafanye Kazi saa ngapi atahudumia watu kiroho,thus utakiwa kulishwa na waamini.

Mfano unataka huduma za kiroho unafika ofisini unaambiwa subiria Saa moja jioni mtumishi ameenda kibaruani kubeba zege au kufanya kibarua Ili apate pesa aendeshe familia.

Kuwa mtumishi wa Mungu hakuondoi uhitaji wake kama mwanadamu.Pili bill za umeme,maji,simu,nauli, internet,mafundi,malazi na chakula hotelini, mafuta ya gari atakulipia Mungu? Sadaka, zaka, michango ni sehemu ya ibada na ni maagizo ya MUNGU kwa muamini na mapato na matumizi yake uwekwa wazi kwa waumini wote kimaandiko.

Hakuna mafanikio nje ya kutoa usipotoa kwa Mungu utatoa kwa shetani. KWA Mungu unatoa 10% 90 tumia kwa shetani unatoa 60% 40 tumia.

Kati ya kwa Mungu na kwa shetani nani ufanikiwa zaidi jibu ni kwa shetani kwann sababu wafuasi wa shetani wanatoa zaidi kuliko wafuasi wa Mungu. Kwa mganga unatoa ng'ombe kwa Mungu unatoa sh 500.

Waabudu shetani kutwa kuwapotosha Wakristo waache kutoa sababu wanajua nguvu ya kutoa, wanajua kutoa ni ulinzi dhidi ya shetani,
 
Nimekosa pa kunukuu mkuu kwakuwa nukuu zote zilizopo zimeandikwa na wanufaika wa sadaka. Hapa nimetumia uncommon sense, ufunuo na kutazama viumbe wengine. Hebu niambie Mungu na hela vinaendana? atanunulia nini ukimpa fedha, je ana tumbo na mdomo? je, anategemea utakachompa?
SAsa bili za maji,umeme,simu,uinjilishaji,kulipia vipindi vya redio na tv nk utawaambia watoa huduma kachukue pesa kwa Mungu,in common way?
 
Naunga mkono hoja...

Hakuna kula madhabauni, hata wachungaji nao watafute kazi za kujiingizia kipato..

Siku za ibada tutakutana kumshukuru Mungu kwa tulichokipata kwa sote na sio kutoa masadaka tu...
Wako waumini wana hali ngumu za kimaisha na bado kanisa linawaimize watoe tu hadi senti ya mwisho bila huruma. Na wao wanatoa tu coz brain washed.

Sadaka ni kile unachowapa wenye uhitaji...
Sadaka sio pesa,kwani akitoa mda na nguvu zake uoni ni sadaka pia. Huyo Mchungaji akabebe zege ataandaa Saa ngapi somo la kukufundisheni ninyi siku ya ibada.

Kanisa ni ofisi pia ipo wazi hata zisizo siku za ibada anahitaji kukutana na wenye shida kuwapa ushauri wa kiroho, kutoa huduma za mazishi, kufariji wagonjwa, kufungisha ndoa, bado apokee simu kuwapa faraja, au kuwaombea wahitaji.

Sasa akafanye Kazi kwa Mhindi Saa ngapi huo mda ataugawa.Kazi ya Mungu na Kazi kama Kazi za kusaka kipato haziendani,ni lazima utaegemea sehemu moja.

Thus wengine uona bora kuacha Kazi. Jiulize kwann mapadre awaruhusiwi kuoa chagua moja umtumikie Mungu au uitumikie familia, hivi viwili vinahitaji mda na 24 uwepo wako.
 
Niambie wametoa shilingi ngapi. Walikuwa wanatoa wanyama na mazao na watu wote wanakula sadaka hiyo, hata wazee walikuwa wanatoa sadaka mazao na wanyama tu na kuwashirikisha mababu zao waliotangulia mbele za haki, ndio maana walikuwa wakijibiwa maombi yao haraka. Sio kutoa fedha na kuziacha madhabahuni kwenye vihenge na kuondoka zenu majumbani mkiamini kuwa zinaenda kwa mungu kumbe zinakwenda kuliwa na watu na kusomesha watoto wao. Huu ni ujinga mkubwa sana,
Zamani billi za umeme,maji,simu,magari, tv havikuwepo hivi unalipa pesa ulipi mifugo
 
Nadhani mleta mada ungebaki tu kwenye kuwajali wazazi. Hii kusema usitoe sadaka HAIKUBALIKI hata kwenye dini ya mizimu ya Yericko Nyerere. Hata kwenye mizimu wanatoa sadaka. Una hoja nzuri ila umeiharibu mwenyewe.
 
Shida ni hawa mitume na manabii wanaoishi kifahari magari majumba ya kifahari miradi mikubwa walinzi kwann wasiwaendeleze waumini wao masikini mfano kuwajengea uwezo wa kiuchumi jibu ni kwamba wengi wao Wana maagano na kuzimu pesa zao hazitakiwi kusaidia watu.

Wana pesa za mikataba,
 
Kila mtu ni lazima amtegemee Mungu kwa kila jambo, Na Mungu amekwishampa kila mtu kila kitu anachohitaji yeye kwenye dunia hii, anachotikiwa yeye ni kuvitumia vitu hivyo kikamilifu kama alivyoopewa, usigeuko tena nyuma na kumuomba tena akusaidie zaidi ya kumshukuru tu kila wakati kwa uumbaji huu mahiri. Sasa ni kazi yako wewe kuvuta hewa, kunywa maji, kula chakula, kutafuta chakula, kulala usingizi, kujitunza, kuzaa watoto, kuwanyonyesha, kwenda kujisaidia haja kubwa na ndogo, kucheka, kulia, nk Sio kazi ya Mungu tena hiyo yeye ameshakupa kila kitu. Kama akitokea binadamu mwenzako akakusaidia kitu chochote atakuwa amekupa sadaka. Yaani pamoja na wewe kutakiwa na Mungu ujifanyie mambo yako yote baada ya kupewa kila kitu unachohitaji mimi nimekupa msaada (sadaka) kukupa chakula, maji, malazi, au hata kukusindikiza safari yako. Hiyo ndiyo sadaka ya kweli iliyokusudiwa, na sadaka hizi tunazopeana hazina malipo kwa Mungu kwakuwa kila mtu unapokea misaada (sadaka) kutoka kwa wengine, Hivyo hakuna mtu hata mmoja asiyehitaji sadaka kutoka kwa wengine. yaani viumbe vyote vinategemeana, vinapokea na kutoa sadaka zao.

Mfano, ili ulime na kupata mazao lazima mchwa ukusaidie kuozesha manyasi kugeuka mbolea, je, wewe unaulipa nini mchwa? unamlipa nini nyuki? unamlipa nini aliyekupa maji ya kuoga?

Malizo ya mzazi ni makubwa kwakua hangaika kitandani kutoa mbegu zake, aliyekuzaa, kukubeba tumboni, kukulea, nk? sadaka yake ni kubwa kuliko sadaka za watu wooooote hapa duniani kwakuwa wao hawalipwi kwa kazi hii, Vitu vyoote binadamu analipwa na wenzake lakini kuzaa halipwi, ndio maana mtoto lazima umlipe mwenyewe mzazi wako.
Mtoto amlipi mzazi bali utoa shukrani na ni ibada pia kumtunza mzazi karma Ili nawe kesho utatunzwa sababu ulipanda mbegu.Huwezi mlipa mzazi gharama alizokulea
 
Mungu anapokea dhamira na nia sio vitu na matendo yako. Unaonekana unaswali kumbe ni mchawi tu. Usikubali kumpa mtu sadaka, ni chukizo mbele ya Mungu, hahitaji chochote kutoka kwetu zaidi ya kumsifu, kumtangaza na Kumshukuru yeye baasi. Na Mungu hajibu maombi ya mtu mmoja mmoja na wewe huna hadhi ya kuongea na Mungu wala kuoona uso wa Mungu, huna uwezo na dhamani hiyo, wewe utaishia kumuomba mzazi wako tu na yeye atayapeleka maombi yako kwa baba yake na baba yake atayapeleka kwa baba yake ambae siku ya siku yatamfikia Adam na hawa ambao wao ndio wenye hadhi na sifa ya kuyawasilisha kwa Mungu, yaani protocol lazima izingatiwe. Ndiyo maana kama wewe huna mahusiano mazuri na wazazi wako unaowafahamu kwa sura usijihangaike kabisa na maswala ya Mungu ambae hujawahi kumuona.
Hapa umechanganya,Mungu ana nafasi yake na mzazi ana nafasi yake pia.Na KILA mmoja anautaratibu wake wa kupewa.Je wale wazazi wao awapo duniani wakawafate wapi.
 
Shida ni hawa mitume na manabii wanaoishi kifahari magari majumba ya kifahari miradi mikubwa walinzi kwann wasiwaendeleze waumini wao masikini mfano kuwajengea uwezo wa kiuchumi jibu ni kwamba wengi wao Wana maagano na kuzimu pesa zao hazitakiwi kusaidia watu. Wana pesa za mikataba,
Mkuu hawa manabii feki ni suala lingine kabisa ambalo ni janga la kitaifa. Pia baadhi ya mafundisho ya kikristo kuhusu sadaka yanachanganya sana. Mfano SDA wanaambiwa 10% ya mapato ni zaka na 10% ni sadaka. Jumla 20% ya mapato yako. Lakini tukumbuka mapato na faida ni vitu viwili tofauti.

Lakini viongozi wanang'ang'ania ukipata 10m utoe 1m bila kujali pale capital & expenses inaweza kuwa labda 9m hivyo 1m ndo unaweza kuitumia. Ukiwaelekeza wanakutolea maneno ya vitisho. Mimi nadhani sadaka zitolewe kwa jinsi mtu anavyoguswa na sio lazima kumpelekea nabii /mtume /mchungaji.

Sadaka kwenye haya mambo ya kiimani haizuliki. Imani zote hadi wale freemason wana sadaka zao.
 
Waabudu shetani awataki Wakristo watoe, Ili wasibarikiwe na kuwekewa ulinzi kusudu waweze kuwateka. Unaweza ukasoma agenda za shetani kwa mwaka 2022 zilizotimia dhidi ya mwanadamu.

Naingia chimbo taweka mkakati wa shetani kwa mwaka 2023 dhidi ya dunia.Ishu kama corona,ushoga nk hizi ni on going agenda. Corona ilikuwa ni ajenda ya 2020
 
Mkuu hawa manabii feki ni suala lingine kabisa ambalo ni janga la kitaifa. Pia baadhi ya mafundisho ya kikristo kuhusu sadaka yanachanganya sana. Mfano SDA wanaambiwa 10% ya mapato ni zaka na 10% ni sadaka. Jumla 20% ya mapato yako. Lakini tukumbuka mapato na faida ni vitu viwili tofauti. Lakini viongozi wanang'ang'ania ukipata 10m utoe 1m bila kujali pale capital & expenses inaweza kuwa labda 9m hivyo 1m ndo unaweza kuitumia. Ukiwaelekeza wanakutolea maneno ya vitisho. Mimi nadhani sadaka zitolewe kwa jinsi mtu anavyoguswa na sio lazima kumpelekea nabii/mtume/mchungaji. Sadaka kwenye haya mambo ya kiimani haizuliki. Imani zote hadi wale freemason wana sadaka zao.
Hakuna mafanikio yeyeto iwe kwa shetani au kwa Mungu au kwa nature bila kutoa, Hakuna mganga anaetibu bure ni kinyume na miiko atakula adhabu kali Sana ikiwemo kifo.
 
Kila Mtu na life style yake, na kizuri zaidi maisha hayanaga kanuni unaweza usitoe na ukawa msindikizaji tu wa mafanikio ya wengine miaka nenda rudi [emoji124][emoji1]

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
Nijuavyo Mimi ukitoa unapunguza, lakini jamaa wanakwambia ukitoa unaongezewa, kwanini hasemi ukipokea unapunguziwa?

Kwanini wanapokea zaidi kila siku lakini waumini wanakitoa wanaongezewa. Yaani zinaongezeka kivipi? 20 -5 = 15. Kweli wajinga hawaishi tuendelee kutengeneza vibuyu vyetu.
 
Na mie naongezea "atawaacha baba yake na mama yake......."

Guess will happen
Hapo maana yake ataacha kuendelea kutunzwa na kulindwa na baba na mama yake.... Lakini heshima kwa baba na mama itabaki palepale,
 
Waabudu shetani awataki Wakristo watoe, Ili wasibarikiwe na kuwekewa ulinzi kusudu waweze kuwateka. Unaweza ukasoma agenda za shetani kwa mwaka 2022 zilizotimia dhidi ya mwanadamu.
Naingia chimbo taweka mkakati wa shetani kwa mwaka 2023 dhidi ya dunia.Ishu kama corona,ushoga nk hizi ni on going agenda.Corona ilikuwa ni ajenda ya 2020
Wajinga hawataisha tuendelee kujenga makanisa na misikiti tupate sadaka. Kule china hawaendi kanisani Wala msikitini na idadi Yao ni robo ya watu wote duniani, kwahiyo wanakamatwa na shetani?
 
Back
Top Bottom