Usitoe sadaka, umeshatoa

Usitoe sadaka, umeshatoa

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Mungu wetu alishatuumba, akawakabidhi wazazi wako wakamilishe mchakato uliobakia wa kukuzaa, kukulisha, kukuvalisha na kukutunza kwa muda fulani kabla na wewe hujaanza kujitunza na kuzaa watoto wengine. Kama ni sadaka mpe mzazi wako anaeweza kuitumia hiyo sadaka sio Mungu, kwakuwa Mungu hana matumizi ya sadaka; fedha, chakula wala mifugo yako maana vitu vyote ni vyake vinatoka kwake na anavyo vingi kuliko baba na mama yako.

Wazazi wako wana matumizi, wana mwili, wana mdomo, na wana tumbo, hivyo wanajua nini cha kufanya ukiwapa pesa, nguo, chakula, mifugo. Mungu wetu anataka ushukuru tu na kumsifu kama vile unavyomsifu TOYOTA kwa kutengeneza aina ya gari lako unaloliendesha. Baada ya TOYOTA kutengeneza gari lako kazi yako ni kuisifu toyota lakini sio kutoa zawadi, malipo au kuiomba toyota ikupatie mafuta ya gari lako, ukupakie rangi gari lako wala kulifanyia matengenezo gari lako.

Kuna watu wanapoteza Muda wao mwingi kwa Kuomba Mungu badala ya Kushukuru mungu, Kuna watu wanapoteza mali zao nyingi kwa kutoa sadaka kwa Mungu badala ya kuwapa wazazi wao. Wanakosea sana na hawajui walifanyalo zaidi ya kuwatajirisha watu wanaozipokea mali (sadaka) zao. Mungu hana shida lakini wazazi wako wana shida.

Anza na wazazi wako kwanza uone mambo yako yatakavyokunyookea haraka. Kama kila mtu akihangaika na wazazi wake Mungu atasikia vilio na maombi yao haraka kwakuwa wazazi ndio bomba lako linalopitisha maombi kutoka kwako kupitia kwa wazazi, mababu, mitume, kupitia kwa Adam na Hawa hadi kumfikia Mungu, kwakuwa Adam na Eva wanamfahamu Mungu zaidi kuliko wewe, na babu yako yuko karibu na Adam, baba yako yuko karibu na babu yako, na wewe uko karibu na baba yako. Ndiyo maana kila anaewadharau wazazi na mababu zake hafiki mbali kwakuwa Mungu yuko karibu nao zaidi kuliko wewe.

kila mtu anatoa sadaka kila siku anapomsaidia mtu mwingine jambo, hata kumuonyesha mtu njia, kumpa mtu maji ya kunywa, kumbeba, kumpa chakula au soda, umeshalipa sadaka tayari, lakini mzazi wako ni wajibu sio hiari kumpa sadaka zako.

Sadaka unayotoa haifiki kwa Mungu bali inaliwa tu na wajanga wanaojifanya wanaipeleka kwa Mungu. Tafuta mayatima na wajane wape kama unataka kuwapa, lakini wajali zaidi wazazi wako, utaona mambo na miujiza wasiyoiweza "watumishi wa mungu" unaowapa hela zako kila siku. Unatapeliwa ndugu yangu, fumbua macho yako.
 
Umenukuu andiko gani mkuu kujenga hiyo hoja yako?
Nimekosa pa kunukuu mkuu kwakuwa nukuu zote zilizopo zimeandikwa na wanufaika wa sadaka. Hapa nimetumia uncommon sense, ufunuo na kutazama viumbe wengine.

Hebu niambie Mungu na hela vinaendana? atanunulia nini ukimpa fedha, je ana tumbo na mdomo? je, anategemea utakachompa?
 
Mbona kama umeandika taka taka tu hapa
unaona ni takataka kwakuwa wewe ni mnufaika wa sadaka hizi, mnawafanya watu wajinga kwa kutumia jina la Mungu. Fedha hizi za sarafu na makaratasi sio za Mungu na hazitoki kwa Mungu, unapopokea noti 3 za sh, 10,000 halafu unaniambia ngoja tuziombee ili Mungu akuongezee pale ulipotoa ni mbinu za kipuuzi kabisa.

Binadamu katengeneza likaratasi lake halafu akaliita hela yeye mwenyewe halamu anamhusisha Mungu na likaratasi hilo ni wizi tu sawa na wizi mwingine.
 
Mleta mada yupo sawa, Mungu anatakiwa kushukuriwa tu, na kumshukuru kuna njia nyingi tu
Mungu anapokea dhamira na nia sio vitu na matendo yako. Unaonekana unaswali kumbe ni mchawi tu. Usikubali kumpa mtu sadaka, ni chukizo mbele ya Mungu, hahitaji chochote kutoka kwetu zaidi ya kumsifu, kumtangaza na Kumshukuru yeye baasi.

Na Mungu hajibu maombi ya mtu mmoja mmoja na wewe huna hadhi ya kuongea na Mungu wala kuoona uso wa Mungu, huna uwezo na dhamani hiyo, wewe utaishia kumuomba mzazi wako tu na yeye atayapeleka maombi yako kwa baba yake na baba yake atayapeleka kwa baba yake ambae siku ya siku yatamfikia Adam na hawa ambao wao ndio wenye hadhi na sifa ya kuyawasilisha kwa Mungu, yaani protocol lazima izingatiwe.

Ndiyo maana kama wewe huna mahusiano mazuri na wazazi wako unaowafahamu kwa sura usijihangaike kabisa na maswala ya Mungu ambae hujawahi kumuona.
 
Nimekosa pa kunukuu mkuu kwakuwa nukuu zote zilizopo zimeandikwa na wanufaika wa sadaka. Hapa nimetumia uncommon sense, ufunuo na kutazama viumbe wengine. Hebu niambie Mungu na hela vinaendana? atanunulia nini ukimpa fedha, je ana tumbo na mdomo? je, anategemea utakachompa?
Kama umekosa pa kunukuu ni heri ungeanzisha uzi wa kupinga kuhongana maana hapo waweza tumia common sense kujenga hoja yako.

Kuhusu kupinga sadaka hapo bila ya andiko (hata la kutoka kwa shetani) huwezi kujenga hoja, jipange ndugu.
 
Kila mtu ni lazima amtegemee Mungu kwa kila jambo, Na Mungu amekwishampa kila mtu kila kitu anachohitaji yeye kwenye dunia hii, anachotikiwa yeye ni kuvitumia vitu hivyo kikamilifu kama alivyoopewa, usigeuko tena nyuma na kumuomba tena akusaidie zaidi ya kumshukuru tu kila wakati kwa uumbaji huu mahiri.

Sasa ni kazi yako wewe kuvuta hewa, kunywa maji, kula chakula, kutafuta chakula, kulala usingizi, kujitunza, kuzaa watoto, kuwanyonyesha, kwenda kujisaidia haja kubwa na ndogo, kucheka, kulia, nk Sio kazi ya Mungu tena hiyo yeye ameshakupa kila kitu. Kama akitokea binadamu mwenzako akakusaidia kitu chochote atakuwa amekupa sadaka.

Yaani pamoja na wewe kutakiwa na Mungu ujifanyie mambo yako yote baada ya kupewa kila kitu unachohitaji mimi nimekupa msaada (sadaka) kukupa chakula, maji, malazi, au hata kukusindikiza safari yako. Hiyo ndiyo sadaka ya kweli iliyokusudiwa, na sadaka hizi tunazopeana hazina malipo kwa Mungu kwakuwa kila mtu unapokea misaada (sadaka) kutoka kwa wengine, Hivyo hakuna mtu hata mmoja asiyehitaji sadaka kutoka kwa wengine. yaani viumbe vyote vinategemeana, vinapokea na kutoa sadaka zao.

Mfano, ili ulime na kupata mazao lazima mchwa ukusaidie kuozesha manyasi kugeuka mbolea, je, wewe unaulipa nini mchwa? unamlipa nini nyuki? unamlipa nini aliyekupa maji ya kuoga?

Malizo ya mzazi ni makubwa kwakua hangaika kitandani kutoa mbegu zake, aliyekuzaa, kukubeba tumboni, kukulea, nk? sadaka yake ni kubwa kuliko sadaka za watu wooooote hapa duniani kwakuwa wao hawalipwi kwa kazi hii, Vitu vyoote binadamu analipwa na wenzake lakini kuzaa halipwi, ndio maana mtoto lazima umlipe mwenyewe mzazi wako.
 
Kama umekosa pa kunukuu ni heri ungeanzisha uzi wa kupinga kuhongana maana hapo waweza tumia common sense kujenga hoja yako.

Kuhusu kupinga sadaka hapo bila ya andiko (hata la kutoka kwa shetani) huwezi kujenga hoja, jipange ndugu.
Ibrahim alitoa sadaka kwa mungu. Wana wa Israel walitoa sadaka kwa mungu, daudi na Suleiman pia. Halafu anakuja hapa kutwambia tusitoe sadaka[emoji706][emoji706][emoji706]
 
unaona ni takataka kwakuwa wewe ni mnufaika wa sadaka hizi, mnawafanya watu wajinga kwa kutumia jina la Mungu. Fedha hizi za sarafu na makaratasi sio za Mungu na hazitoki kwa Mungu, unapopokea noti 3 za sh, 10,000 halafu unaniambia ngoja tuziombee ili Mungu akuongezee pale ulipotoa ni mbinu za kipuuzi kabisa. Binadamu katengeneza likaratasi lake halafu akaliita hela yeye mwenyewe halamu anamhusisha Mungu na likaratasi hilo ni wizi tu sawa na wizi mwingine.
Ibrahim alitoa sadaka kwa mungu. Wana wa Israel walitoa sadaka kwa mungu, daudi na Suleiman pia. Halafu unakuja hapa kutwambia tusitoe sadaka[emoji706][emoji706]
 
Mleta mada yupo sawa, Mungu anatakiwa kushukuriwa tu, na kumshukuru kuna njia nyingi tu
Kaleta hoja kuhusu mambo ya Mungu, halafu hana reference kutoka andiko lolote, hatuwezi kusema yupo sahihi Ila tutasema ana roho ya korosho ama mkono wa birika.
 
Wingi wa hizi mada ina maana sio bahati mbaya lazima kuna kikundi kinawatumia. Hicho kikundi ni vyema kikawaelekeza kutumia akili.
Sadaka iko kwenye maandiko matakativu,leo muhuni anakuja na blah blah tu akiwaambia watu wasitoe sadaka bila kunukuu maandiko. Jitu hili hata likienda kwa shetani kuchanjwa chale za makalio linatoa sadaka.

Tumeelekezwa tukusanyike madhabauni kumwabudu Mungu. Kwa akili ya kawaida tu, hiyo nyumba ya Mungu itajengwa vipi, inatunzwa vipi, itajiendesha vipi. Wewe uko na mkeo asubuhi mnaelekea vibaruani. Mchungaji yeye anaenda kanisani kuandaa ibada na mafundisho. Atakula kwa baba yako bila sadaka?

Halafu wahuni hawa wanakuja na mikelele humu kuhusu sadaka. Mbona simple tu nenda kwa paroko/shehe wako kamwambie mimi siwezi kutoa sadaka. Kama hausali hizo sadaka zinakuuma nini?
 
Ibrahim alitoa sadaka kwa mungu. Wana wa Israel walitoa sadaka kwa mungu, daudi na Suleiman pia. Halafu anakuja hapa kutwambia tusitoe sadaka[emoji706][emoji706][emoji706]
Niambie wametoa shilingi ngapi. Walikuwa wanatoa wanyama na mazao na watu wote wanakula sadaka hiyo, hata wazee walikuwa wanatoa sadaka mazao na wanyama tu na kuwashirikisha mababu zao waliotangulia mbele za haki, ndio maana walikuwa wakijibiwa maombi yao haraka.

Sio kutoa fedha na kuziacha madhabahuni kwenye vihenge na kuondoka zenu majumbani mkiamini kuwa zinaenda kwa mungu kumbe zinakwenda kuliwa na watu na kusomesha watoto wao. Huu ni ujinga mkubwa sana,
 
Back
Top Bottom