Usitoe sadaka, umeshatoa

Usitoe sadaka, umeshatoa

Wajinga hawataisha tuendelee kujenga makanisa na misikiti tupate sadaka. Kule china hawaendi kanisani Wala msikitini na idadi Yao ni robo ya watu wote duniani, kwahiyo wanakamatwa na shetani?
Kule sio ndio makao ya shetani awakamate mara ngapi,wao wanaabudu shetani kupitia dragon.Unaona wachina Wana utu? Kazi ya dini ni kuishape jamii kwa huduma za kiroho na kimwili.
 
Hivi huko misikitini sadaka kumbe hamtoi

Kuna cha kujifunza hapa, mnajiendeshaje
Unajiendeshaje kufanya nn? Kila kitu kinaishia palepale kwenye ibada, kila mtu ana jukumu binafsi la kumshukuru Mungu wake. Asikudanganye mtu kwamba anaweza kukuombea wewe kwa lolote. Ili upone kula vizuri, vuta hewa vizuri, na kunywa maji vizuri kwa kiasi.

Lala vizuri, epuka mawazo, shirikiana na wenzako, nk atakuombeaje mtu ambae na yeye anaugua na kufa, anavuta hewa na kunywa maji kama wengine?
 
Uongo mtupu, wazungu wanafanikiwa kwa sababu wanazitumia akili zao vizuri kufanyia mambo ya maana.
Sadaka ina siri kubwa katika mafanikio yako,Hata hao wazungu wanatoa sana ndio maana wanafanikiwa
 
Sadaka sio pesa,kwani akitoa mda na nguvu zake uoni ni sadaka pia.
Huyo Mchungaji akabebe zege ataandaa Saa ngapi somo la kukufundisheni ninyi siku ya ibada.
Kanisa ni ofisi pia ipo wazi hata zisizo siku za ibada anahitaji kukutana na wenye shida kuwapa ushauri wa kiroho,kutoa huduma za mazishi,kufariji wagonjwa,kufungisha ndoa,bado apokee simu kuwapa faraja,au kuwaombea wahitaji.Sasa akafanye Kazi kwa Mhindi Saa ngapi huo mda ataugawa.Kazi ya Mungu na Kazi kama Kazi za kusaka kipato haziendani,ni lazima utaegemea sehemu moja.
Thus wengine uona bora kuacha Kazi. Jiulize kwann mapadre awaruhusiwi kuoa chagua moja umtumikie Mungu au uitumikie familia, hivi viwili vinahitaji mda na 24 uwepo wako.
Mkuu umejaribu kudadavua vyema,ila naona hoja yako bado haijanibamba vyema...

Wakatoliki wana kitu kinaitwa jumuia,
Unakifahamu hata kwa uchache?
Then ndio tuendelee na mada yetu.
 
Mkuu umejaribu kudadavua vyema,ila naona hoja yako bado haijanibamba vyema...

Wakatoliki wana kitu kinaitwa jumuia,
Unakifahamu hata kwa uchache?
Then ndio tuendelee na mada yetu.
Mimi ni Mwenyekiti wa jumuiya yenyewe,twende kazi
 
Naunga mkono hoja...

Hakuna kula madhabauni, hata wachungaji nao watafute kazi za kujiingizia kipato..

Siku za ibada tutakutana kumshukuru Mungu kwa tulichokipata kwa sote na sio kutoa masadaka tu...
Wako waumini wana hali ngumu za kimaisha na bado kanisa linawaimize watoe tu hadi senti ya mwisho bila huruma. Na wao wanatoa tu coz brain washed.

Sadaka ni kile unachowapa wenye uhitaji...
Walivyo wajinga mpaka wakawatungia wimbo wajinga wajikamue mpaka tone lao la mwisho kuwapa wao: "..toa ndugu toa ndugu hicho ulichonacho maana Mungu anakuona mpaka rohoni mwako...." wanamtumia Mungu kupumbaza watu watoe hata ile thumumuni ya kununulia kishikizo cha shati lako uwape wao. Yaani kama Mungu anaona mpaka rohoni mwako sembuse kwenye pochi yako, kwenye mfuko wako wa suruali? Toa ndugu.......

Wajinga hawatakwisha usizitupe pembe zako za ng'ombe kila ukichinja. Hebu fikiria kama mtoto wako anadaiwa ada ya tsh 200000 ili aruhusiwe kufanya mitihani, halafu mla kondoo anakwambia toa sadaka 20,000 kumpa "Mungu" na Mungu atakuzidishia mara 100 pale ulipopunguza. 200000 - 20,000 zinabaki 180,000. Hebu elezea namna 180,000 mungu atakavyoziongeza zifike 2000000+. Wakati wewe mwanao anakosa kufanya mitihani mla kondoo anapeleka kwanza sadaka kwa wazazi wake kuhakikisha kuwa hawana shida yoyote, zilizobaki anafanyia mambo yake na kidooogo anawalipa posho wahudumu mule kwenye nyumba ya Ibada na kulipia umeme na maji.

Tena hata huo umeme na maji inawezekana kuna mjinga mmoja pia amelipia mwaka mzima kutoka na fedha alizopata kwa nja haramu anaambiwa azisafishe.
 
Naunga mkono hoja...

Hakuna kula madhabauni, hata wachungaji nao watafute kazi za kujiingizia kipato..

Siku za ibada tutakutana kumshukuru Mungu kwa tulichokipata kwa sote na sio kutoa masadaka tu...
Wako waumini wana hali ngumu za kimaisha na bado kanisa linawaimize watoe tu hadi senti ya mwisho bila huruma. Na wao wanatoa tu coz brain washed.

Sadaka ni kile unachowapa wenye uhitaji...
Hiyo ndiyo inayotakiwa na iliyokusudiwa. Mungu Yuko kila mahali hata uvunguni mwa kitanda unaweza kumshukuru TU akakusikia, kule kanisani tunakwenda kusalimiana, kufarijiana, kuhabarishana, kuwafahamu wanaohitaji sadaka za aina mbalimbali, kuwapelekea sadaka (chakula, nguo, dawa, maji, etc) wahitaji.

Kila anaetoa sadaka malipo yake ni hapahapa duniani, tena yanafanywa na wanadamu wenzake sio Mungu, yaani ukitoa kingi utapata kingi hapahapa duniani. Maana yake ukifanya wema kwa watu wengi utalipwa wema na watu wengi pia, ukishiriki harusi za watu wengi watashiri watu wengi kwenye harusi yako pia. Kumpa pesa Mchungaji ukidhani Mungu atakulipa ni ujinga.

Mzazi ana maagizo maalumu kutoka kwa Mungu, ...mheshimu Baba na mama yako ........ . Wazazi ni chombo alichokitumia Mungu kukufikisha hapo ulipo na hivyo ulivyo Leo, hakuna mtu anaetaka gari analosafiria lipate pancha Wala kuharibika, ni lazima atalikagua kila mara kuona kama Lina mafuta maji oil na upepo, atasikiliza hata mngurumo wake njiani na hata likisimama, ataliosha na kilifanyia service hata mwisho wa safari.

Gari lako limekufikisha salama kwenye safari ndefu yenye misukosuko mingi, milima, Kona, makorongo, vibaka, njaa, mafuta ghali, nk hadi limekufikisha hapo ulipo Sasa, ni kazi yako kilifanyia service Sasa, na hayo ni maagizo ya Mungu mwenyewe, sio hiyari. Kila siku lazima uhakikishe kuwa umepata taarifa za baba na mama. Yaani unaanza na baba ndipo umalizie na mama kwa mujibu wa maagizo; "Baba na mama" na sio "mama na baba"
 
Mungu wetu alishatuumba, akawakabidhi wazazi wako wakamilishe mchakato uliobakia wa kukuzaa, kukulisha, kukuvalisha na kukutunza kwa muda fulani kabla na wewe hujaanza kujitunza na kuzaa watoto wengine. Kama ni sadaka mpe mzazi wako anaeweza kuitumia hiyo sadaka sio Mungu, kwakuwa Mungu hana matumizi ya sadaka; fedha, chakula wala mifugo yako maana vitu vyote ni vyake vinatoka kwake na anavyo vingi kuliko baba na mama yako. Wazazi wako wana matumizi, wana mwili, wana mdomo, na wana tumbo, hivyo wanajua nini cha kufanya ukiwapa pesa, nguo, chakula, mifugo. Mungu wetu anataka ushukuru tu na kumsifu kama vile unavyomsifu TOYOTA kwa kutengeneza aina ya gari lako unaloliendesha.

Baada ya TOYOTA kutengeneza gari lako kazi yako ni kuisifu toyota lakini sio kutoa zawadi, malipo au kuiomba toyota ikupatie mafuta ya gari lako, ukupakie rangi gari lako wala kulifanyia matengenezo gari lako.

Kuna watu wanapoteza Muda wao mwingi kwa Kuomba Mungu badala ya Kushukuru mungu, Kuna watu wanapoteza mali zao nyingi kwa kutoa sadaka kwa Mungu badala ya kuwapa wazazi wao. Wanakosea sana na hawajui walifanyalo zaidi ya kuwatajirisha watu wanaozipokea mali (sadaka) zao. Mungu hana shida lakini wazazi wako wana shida.

Anza na wazazi wako kwanza uone mambo yako yatakavyokunyookea haraka. Kama kila mtu akihangaika na wazazi wake Mungu atasikia vilio na maombi yao haraka kwakuwa wazazi ndio bomba lako linalopitisha maombi kutoka kwako kupitia kwa wazazi, mababu, mitume, kupitia kwa Adam na Hawa hadi kumfikia Mungu, kwakuwa Adam na Eva wanamfahamu Mungu zaidi kuliko wewe, na babu yako yuko karibu na Adam, baba yako yuko karibu na babu yako, na wewe uko karibu na baba yako. Ndiyo maana kila anaewadharau wazazi na mababu zake hafiki mbali kwakuwa Mungu yuko karibu nao zaidi kuliko wewe.

kila mtu anatoa sadaka kila siku anapomsaidia mtu mwingine jambo, hata kumuonyesha mtu njia, kumpa mtu maji ya kunywa, kumbeba, kumpa chakula au soda, umeshalipa sadaka tayari, lakini mzazi wako ni wajibu sio hiari kumpa sadaka zako.

Sadaka unayotoa haifiki kwa Mungu bali inaliwa tu na wajanga wanaojifanya wanaipeleka kwa Mungu. Tafuta mayatima na wajane wape kama unataka kuwapa, lakini wajali zaidi wazazi wako, utaona mambo na miujiza wasiyoiweza "watumishi wa mungu" unaowapa hela zako kila siku. Unatapeliwa ndugu yangu, fumbua macho yako.

Usidanganye watu.
Wewe ni mzazi?
Kutoa huduma kwa wazazi na ndugu wengine ni wajibu wala siyo sadaka kwa mujibu wa maandiko.sikiliza ukitoa kitu ukapewa asante hiyo inatosha unaombewa. baraka.
Sadaka ni sadaka na huduma ni huduma.

Ngoja tu-expand kidogo hapa:
Sadaka huambatana na Ibada. Hebu tuanze na upande wa gizani; Mganga akikuambia leta kuku mweupe au mbuzi(Hizi ni sadaka) ili akufanyie matibabu(akuombee).Ukiifikisha pale ataichinja ili kupata ile damu kwa ajili ya miungu yake na ataongea na vimaneno uchwara hivi.akishamaliza ile ibada ile nyama inayobaki huwa hawatupi wanakulaga. sasa anachokula pale ni nyama ya mnyama iliyetolewa sadaka.

Vivyo hivyo watumishi wa Mungu(Hapa tunazungumza watumishi wa kweli wa Mungu aliye wa Kweli) baada ya kuzibariki zile sadaka ulizotoa(Kutoa kwa Imani na kwa moyo wa kumpenda Mungu).Kiimani Mungu anakuwa ameshazipokea.Mungu akishazipokea,baada ya hapo zinakuwa fedha za kawaida za matumizi mengine(Kama vile wale makuhani wa giza(Waganga) anapoanza kutumia zile nyama kutoka kwa mnyama aliyekwishatolewa sadaka.

Kwa Kifupi ni Hivi,ukipeleka fedha au mnyama madhabahuni(Madhabahu yoyote ile,ya giza au ya Mungu wa kweli).Inapoenda pale inapofika pale inakuwa sadaka,ila ikishatolewa pale inakuwa kile kitu ulichopeleka(fedha au mnyama)

Angalizo;Usijidangaye, kufanya matendo ya huruma tu (Msaada kwa wahahitaji).Haitoshi kumesabia haki mtoaji,yaani hayo pekee yake hayatakupeleka Mbingu.Usipoamini na kujifunga Nira kwa Kristo Yesu.

Nitarudi baadaye,ngoja kwanza nikatafute tiketi ya basi la mkoani
 
Kuna watu ni wapumbavu, wana pesa za kununua mafuta sijui ya upako ila hawana pesa za kukatia wazazi BIMA ya afya.

Kila siku za ibada mabilioni ya sadaka yanatolewa na kila siku kwenye mahospitali wanakufa watu waliokosa fedha za matibabu.

Kuna Mahospitali hata ya makanisa watu wanakosa pesa za matibabu mpaka wanakufa lakini hilo kanisa linakusanya mamilioni ya sadaka. Tunapokusanyika kumwabudu MUNGU tunamwabudu MUNGU wa aina gani? Ni huyu huyu aliyeagiza amri kuu iwe upendo?
 
Shambulizi kubwa kwa kanisa lilikuwa kumtundika Yesu msalabani, baada ya lile yote yalishindwa palelale msalabani, mtu anasema Mungu hali sadaka, hilo kanisa alijenga Bibi yako? kiti unachokalia kanisani umetoa nyumbani kwako, watumishi wanaokuhudumia wanalipwa na serikali?

Hio biblia unayonukuu kuhusu kuwaheshimu wazazi ilidondoshwa na radi?
 
Angalizo;Usijidangaye, kufanya matendo ya huruma tu (Msaada kwa wahahitaji).Haitoshi kumesabia haki mtoaji,yaani hayo pekee yake hayatakupeleka Mbingu
Acha uongo.
Yaani mtu anayelisha walio na njaa, anayesomesha wasio na ada, anayelipia matibabu ya wasio na fedha za matibabu isitoshe kumpatia haki? Umesahau amri ya Upendo?

Endeleeni kudanganya ila yule anayetoa alichonacho na kugawana na asiyenacho ana haki kuliko yule anayepeleka sadaka kwa mchungaji.
 
Shambulizi kubwa kwa kanisa lilikuwa kumtundika Yesu msalabani, baada ya lile yote yalishindwa palelale msalabani, mtu anasema Mungu hali sadaka, hilo kanisa alijenga Bibi yako? kiti unachokalia kanisani umetoa nyumbani kwako, watumishi wanaokuhudumia wanalipwa na serikali? Hio biblia unayonukuu kuhusu kuwaheshimu wazazi ilidondoshwa na radi?
Makanisa yanajengwa na hayataacha kujengwa sababu fedha za ujenzi wa makanisa hutolewa na waumini. Tena makanisa mengine yanatoa maelekezo kabisa, "MCHANGO WA UJENZI WA KANISA"

Hapa suala ni sadaka kila siku za ibada huwa zinafanya kazi gani huko kwa MUNGU ambaye ulimwengu na vyote ni vyake? Kwanini anazihitaji sadaka kuliko wagonjwa, wenye njaa na masikini? Aliposema leteni zaka kamili ghalani alitoa maelekezo kuwa baada ya kukaa ghalani zitafanyiwa nn? Au kuhoji hilo ni kukufuru?
 
Wazo lako zuri, wakifanyia kazi ambao ndio watoa sadaka wakubwa, akili ya kutafakari hawana. Mafanikio ya akina Mwamposa ni uwepo wa watu hao tena kwa wingi. Mafanikio ya wajanja wachache ni matokeo ya uwepo wa wajinga wengi. Na wajanja wanaitumia fursa vilivyo kwa kuitumia falsafa ya usimwamshe mjinga.
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Naunga mkono hoja...

Hakuna kula madhabauni, hata wachungaji nao watafute kazi za kujiingizia kipato..

Siku za ibada tutakutana kumshukuru Mungu kwa tulichokipata kwa sote na sio kutoa masadaka tu...
Wako waumini wana hali ngumu za kimaisha na bado kanisa linawaimize watoe tu hadi senti ya mwisho bila huruma. Na wao wanatoa tu coz brain washed.

Sadaka ni kile unachowapa wenye uhitaji...
Mchungaji akipata kazi sawa, ila vipi awe anachukua mshahara wake ananunua umeme, ulinzi, usafi, ujenzi, usafiri nk?
 
Hiyo ndiyo inayotakiwa na iliyokusudiwa. Mungu Yuko kila mahali hata uvunguni mwa kitanda unaweza kumshukuru TU akakusikia, kule kanisani tunakwenda kusalimiana, kufarijiana, kuhabarishana, kuwafahamu wanaohitaji sadaka za aina mbalimbali, kuwapelekea sadaka (chakula, nguo, dawa, maji, etc) wahitaji. Kila anaetoa sadaka malipo yake ni hapahapa duniani, tena yanafanywa na wanadamu wenzake sio Mungu, yaani ukitoa kingi utapata kingi hapahapa duniani. Maana yake ukifanya wema kwa watu wengi utalipwa wema na watu wengi pia, ukishiriki harusi za watu wengi watashiri watu wengi kwenye harusi yako pia. Kumpa pesa Mchungaji ukidhani Mungu atakulipa ni ujinga.

Mzazi ana maagizo maalumu kutoka kwa Mungu, ...mheshimu Baba na mama yako ........ . Wazazi ni chombo alichokitumia Mungu kukufikisha hapo ulipo na hivyo ulivyo Leo, hakuna mtu anaetaka gari analosafiria lipate pancha Wala kuharibika, ni lazima atalikagua kila mara kuona kama Lina mafuta maji oil na upepo, atasikiliza hata mngurumo wake njiani na hata likisimama, ataliosha na kilifanyia service hata mwisho wa safari.

Gari lako limekufikisha salama kwenye safari ndefu yenye misukosuko mingi, milima, Kona, makorongo, vibaka, njaa, mafuta ghali, nk hadi limekufikisha hapo ulipo Sasa, ni kazi yako kilifanyia service Sasa, na hayo ni maagizo ya Mungu mwenyewe, sio hiyari. Kila siku lazima uhakikishe kuwa umepata taarifa za baba na mama. Yaani unaanza na baba ndipo umalizie na mama kwa mujibu wa maagizo; "Baba na mama" na sio "mama na baba"
Kuna wababa wana watoto kila kona na hawawaudumii mama ndo anateseka nao, kwann wale watoto waanze na baba na sio mama?

Dini zisitufunge fikira zetu na kufata maagizo yake bila kutumia ubongo. Halafu sio kila andiko lililopo kwenye biblia limekulenga ww msomaji, Mfano: Elia aliua mabaali baada ya kusadiki je na sisi tuue watu baada ya kusadiki?
 
Hakika, tatizo binadamu wa siku hizi ni wabishi sana...
 
Usidanganye watu.
Wewe ni mzazi?
Kutoa huduma kwa wazazi na ndugu wengine ni wajibu wala siyo sadaka kwa mujibu wa maandiko.sikiliza ukitoa kitu ukapewa asante hiyo inatosha unaombewa. baraka.
Sadaka ni sadaka na huduma ni huduma.

Ngoja tu-expand kidogo hapa:
Sadaka huambatana na Ibada. Hebu tuanze na upande wa gizani; Mganga akikuambia leta kuku mweupe au mbuzi(Hizi ni sadaka) ili akufanyie matibabu(akuombee).Ukiifikisha pale ataichinja ili kupata ile damu kwa ajili ya miungu yake na ataongea na vimaneno uchwara hivi.akishamaliza ile ibada ile nyama inayobaki huwa hawatupi wanakulaga. sasa anachokula pale ni nyama ya mnyama iliyetolewa sadaka. Vivyo hivyo watumishi wa Mungu(Hapa tunazungumza watumishi wa kweli wa Mungu aliye wa Kweli) baada ya kuzibariki zile sadaka ulizotoa(Kutoa kwa Imani na kwa moyo wa kumpenda Mungu).Kiimani Mungu anakuwa ameshazipokea.Mungu akishazipokea,baada ya hapo zinakuwa fedha za kawaida za matumizi mengine(Kama vile wale makuhani wa giza(Waganga) anapoanza kutumia zile nyama kutoka kwa mnyama aliyekwishatolewa sadaka.

Kwa Kifupi ni Hivi,ukipeleka fedha au mnyama madhabahuni(Madhabahu yoyote ile,ya giza au ya Mungu wa kweli).Inapoenda pale inapofika pale inakuwa sadaka,ila ikishatolewa pale inakuwa kile kitu ulichopeleka(fedha au mnyama)

Angalizo;Usijidangaye, kufanya matendo ya huruma tu (Msaada kwa wahahitaji).Haitoshi kumesabia haki mtoaji,yaani hayo pekee yake hayatakupeleka Mbingu.Usipoamini na kujifunga Nira kwa Kristo Yesu.

Nitarudi baadaye,ngoja kwanza nikatafute tiketi ya basi la mkoani
Vitu ni vya Mungu, ni vyake, katengenneza yeye na kakupa yeye halafu wewe unatoa mbuzi (sadaka) kumpa Mchungaji halafu unasema Mungu anaipokea na kukubariki na kukupa zaidi!!! Kweli wajinga hawaishi, tusivitupe vibuyu vyetu watakuja TU.

Yaani Toyota katengenneza gari, akaliuza, likakufikia wewe, yaani wewe tena unataka Toyota akupe brake pads mpya baada ya wewe kumpa fundi magari vitumbua na shock ups zilizotumika ukiamini kuwa fundi atavifukisha vitumbua na shock ups zako Toyota.

Mganga wa kienyeji nae anatumia ujinga wa wateja wake kupata Kuku, nazi, ng'ombe, nguo na nk. Kitakachokuponya kwa Mganga, kwa Mchungaji na sheikh anaekuombea ni imani yako wewe mwenyewe. Yaani wao wanaofanyakazi ya phycologists, counsellors, phychoanalysts. Njia pekee ya kupata ziada ni kutoa kwa watu wengine, kushiriana na watu wengine, kuchanganya na watu wengine, yaani ni "scratch my back, I will scratch yours."

Mungu kashakupa wewe kila kitu alichotaka wewe ukipate, ni wewe TU kutumia pua, ulimi, mdomo, macho, masikio, ubongo, mikono, miguu, na viungo vyote kuvipata,, baada ya kuvipata kazi yako kubwa na muhimu ni kumshukuru Mungu, kuheshimu wazazi, kuzaa na kulea watoto, mengine madogomadogo utayapata kwa wenzio kwa njia ya sadaka (,misaada).

Kumbuka kuwa sadaka ni msaada wa kile ambacho unakihitaji Sasa hivi lakini hunacho. Kama una njaa na mwenzio akakupa chakula hiyo ni sadaka, kama yatima Hana chakula, nguo wewe ukampa chakula au nguo hapo umetoa sadaka.

Na mtu uliyemsaidia kumpa Benz lako kumpeleka mkewe hospital hawezi kukunyima baiskeli yake uwende ukabebee Kuni zako shambani.
 
Kuna watu ni wapumbavu, wana pesa za kununua mafuta sijui ya upako ila hawana pesa za kukatia wazazi BIMA ya afya.

Kila siku za ibada mabilioni ya sadaka yanatolewa na kila siku kwenye mahospitali wanakufa watu waliokosa fedha za matibabu.

Kuna Mahospitali hata ya makanisa watu wanakosa pesa za matibabu mpaka wanakufa lakini hilo kanisa linakusanya mamilioni ya sadaka. Tunapokusanyika kumwabudu MUNGU tunamwabudu MUNGU wa aina gani? Ni huyu huyu aliyeagiza amri kuu iwe upendo?
Usipotoa sadaka wazazi wako na kuwaheshi dalili mbaya za kwanza kwanza utakazoziona ni hitilafu kwenye tamaa (Mali, mke, mume, watoto, mifugo, mazao na kazi/biashara) zako. Kuna kasoro nyingi utaziona upende usipende kwa mkeo, mumeo, watoto, mifugo na mazao yako.

Hizi ndizo Mali ambazo Mungu anazitambua sio fedha, mahali Wala majumba. Huwezi kufilisika hata kidogo kwa kuwatunza wazee na kuwapa sadaka.
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Back
Top Bottom