Tumia muda wako kufanya kazi na siyo kuhangaika na mapenzi.
Unakutana na pisi kali unaomba namba unaanza kuwa busy nae we unadhani ameonekana na wangapi kabla yako na ni wangapi wanaomtaka . Punguza kupenda sana watu wana watu wao, unayempenda sana naye ana mtu wake anayempenda sana.
Cheza kwa stepu hakuna aliye singo na hakuna wa peke yako
Vp Sasa mimi nishauri kidogo kama mdogo wako hiyi ni story yangu ya mahusiano hivi sasa Kulikuwa na kijana mmoja, mnyenyekevu, mwenye moyo wa upendo na kujali. Alikutana na mwanamke ambaye alikuwa akifanya kazi Saudia. Kwa maneno mwanamke huyo alikuwa na mapenzi ya dhati kwake – alimuita majina mazuri, aliweka jina lake kwenye Facebook, akamfanya ajihisi kuwa mtu muhimu sana maishani mwake.
Lakini polepole, kijana alianza kugundua kuwa kuna mwanya mkubwa kati ya maneno na vitendo.
Walianza kuwa na mawasiliano ya kila saa – mchana na usiku. Mwanamke alikuwa hapendi kabisa asikie kijana ana shughuli nyingine. Akifanya hivyo, mwanamke anaanza kulalamika kuwa ameachwa, ametupiliwa, au kuonekana hana maana. Kijana akijaribu kuweka mipaka au kujipangia ratiba, hata kidogo, mwanamke anashtuka na kusema “unanitesa” au “sihisi vizuri bila wewe.”
Lakini wakati kijana alipokuwa na matatizo – simu imeharibika, passport imekamatwa, hata alipokuwa mgonjwa – mwanamke huyo hakutoa msaada wa maana. Aliishia tu kusema “pole”. Hakujali kwa vitendo. Kijana alibaki kushangaa, kwa nini mtu anayesema anakupenda hawezi hata kutoa msaada mdogo wakati wa shida? Kijana yuko njia panda. Moyo wake unataka upendo, lakini akili inamuonya kuwa kuna kitu hakiko sawa. Huu si uhusiano wa haki – ni kama mapenzi ya upande mmoja. Mapenzi yanahitaji usawa, msaada, heshima, na moyo wa dhati. Na kwa sasa, haoni hayo yote Siku moja, mwanamke huyo alimwambia kijana amsaidie kuchukua pesa benki. Alisema anataka kumtumia kaka yake millioni 1. Lakini akatuma millioni 3. Kijana alienda kwa uaminifu, akatoa pesa zote, akampa mtu aliyekuja kuzichukua kama alivyoelekezwa. Mwanamke huyo alimwachia kijana elfu 80 tu, pesa ndogo sana ukilinganisha na kiwango alichokipokea. Hata hakuonyesha shukrani wala kusema “chukua hii kwa matumizi yako.” Kijana alishangaa – hiyo ndiyo thawabu ya kazi kubwa aliyofanya?
Lakini cha kushangaza zaidi – alipogusia kuwa aliwahi kuuza kitu kupata pesa kwa shida, mwanamke huyo alimcheka na kusema "kumbe hali ilikuwa serious 🤣🤣". Maneno hayo yaliuma.
Mara kwa mara, mwanamke huyu ameonyesha utata – kukubali kutongozwa na akaunti bandia, kusingizia usingizi wa ghafla, kutoonyesha msaada wa kifedha wakati wa shida, lakini bado kujifanya mpenzi mwaminifu mbele za watu. Hata alipoombwa msaada wa pesa kidogo, akawa mkali au anamnyamazisha.
Kwa nje, anaweza kuonekana ni mpenzi mzuri – lakini kwa ndani, matendo yake hayaendani kabisa na maneno yake. Kijana huyu anabaki na maswali mengi moyoni:
Je, ananipenda kwa dhati au ananitumia tu kama daraja la hisia?
Je, siku nikipata matatizo makubwa zaidi, atasimama nami au atanikimbia? Vijana wenzangu naombeni ushauri 😔 nimechoka