Usiuze kwanza Subiri Mji Ukue hapo pakishachangamka patakulipa sana

Usiuze kwanza Subiri Mji Ukue hapo pakishachangamka patakulipa sana

Bueno

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2022
Posts
34,600
Reaction score
59,760
Wakuu, katika kitu kuna Mzee wangu mmoja kila tukikaa anajutia ni kuuza eneo maeneo fulani ya Dar ambapo kipindi hicho palikua ni km Chaka la Simba tu. Enzi hizo kitambo sana akapaona sio kitu akauza akahama anakwambia leo hii akirudi kupaangalia pale alipouza anajuta ni mji pameshushwa ghorofa safi na zimepigwa apartment.

Another mistake, akanunua Shamba poli huko almost Ekari 10 au 15 kwa bei ya kawaida sana, pale aliponunua palikua Chaka tena yaan ni poli hakuna makazi ya watu wala nini kutoka nyumba mpaka kuifikia nyumba ni umbali sana huduma za kijamii hakuna barabara mbovu, akachoka akafanya mpango akauza sasa yule aliemuuzia eneo lilelile akafanya uwekezaji kwanza akajenga Zahanati, Kituo cha kufundishia Watoto yaan Nursery & Primary, kisha akajenga real estate yaan nyumba za kupangisha na fremu za kutosha za maduka, sasa hivi pamechangamka sio kawaida ukienda kupaangalia unajutia kupauza, hii pia anajuta laiti km angejua angesubiri kwanza pachangamke.

Kuna mwingine hapa amepanga kuuza nyumba kwa million zaidi ya 800, mimi naona mbali nimemwambia usiuze hilo eneo ni very potential hilo eneo ni zaidi ya hio pesa hio mwaka hauishi imeisha lile eneo ni faida ya milele, anafikiri atakufa kesho ooh watakaobakia watafaidi bora niuze tu nile hela zangu nijue moja hata nikifa hela zangu nimeshakula si nilijenga mwenyewe, mentality za kijinga sana pesa zikiisha akipita palepale alipouza akakuta aliemuuzia kashusha ghorofa la apartment kadhaa kaweka watu wanaishi anaanza kujilaumu ujinga kwanini aliuza kwanini hakusubiri.

Usiuze kwanza subiri mji uchangamke hapo hapo unapopadharau leo kesho patakulipa sana.
 
Mwingine aliuza eneo usawa wa Barabara eneo alilouza hakujua kua ni eneo very potential na alimuuzia alikua na akili mingi tajiri mmoja hivi tena kamuuzia kwa bei ya hasara kabisa bonge moja la eneo, baada ya kununua akajenga Kituo cha Mafuta unaambiwa kile kituo kimeanza kupiga kazi tangu miaka ya 90 mpaka leo jamaa anaendelea kula faida, waliouza wakipita pale wanajilaumu tu kwanini waliuza eneo very potential km lile

Kujilaumu huja mwishoni huku mwanzoni hakuna kujilaumu.
 
Kwa nini wajilaumu....alikuwa na mtaji wa kufungua hicho kituo cha mafuta?
 
Nauza ichi kipo kibaha,mtaa mzuri,kimepimwa kabisa ,
Milioni Saba.
Ukubwa Mita 30 kwa 20.
Kutoka morogoro road km 1
 
Attachments

  • IMG_20250620_124540_350.jpg
    IMG_20250620_124540_350.jpg
    1.3 MB · Views: 29
  • IMG_20250620_124534_260.jpg
    IMG_20250620_124534_260.jpg
    1.2 MB · Views: 28
  • IMG_20250620_124518_022.jpg
    IMG_20250620_124518_022.jpg
    1.1 MB · Views: 32
Kuna mwingine hapa amepanga kuuza nyumba kwa million zaidi ya 800, mimi naona mbali nimemwambia usiuze hilo eneo ni very potential hilo eneo ni zaidi ya hio pesa hio mwaka hauishi imeisha lile eneo ni faida ya milele, anafikiri atakufa kesho ooh watakaobakia watafaidi bora niuze tu nile hela zangu nijue moja hata nikifa hela zangu nimeshakula si nilijenga mwenyewe, mentality za kijinga sana pesa zikiisha akipita palepale alipouza akakuta aliemuuzia kashusha ghorofa la apartment kadhaa kaweka watu wanaishi anaanza kujilaumu ujinga kwanini aliuza kwanini hakusubiri.
Unajifanya mshauri mzuri hadi unamuita Mjinga.....hilo eneo ni lako? Wewe tafuta ya kwako ndio upangie matumizi.

Hata akiliacha miaka 10 akija mtu kununua bilion moja. Si utamwambia aache kwanza huk mbele atauza bilioni 1.2?

Yeye pengine alijibana bana na kuhustle sana akapanunua milioni 20. Leo anauz mil 800 wewe unamuita Mjinga?
Watanzania Umaskini ni Mbata hadi tunaingilia mali za watu. We utakuwa mchawi ukizeeeka
 
Wateja binafsi nauza Nyumba Ya Room 3 na Kiwanja Chake HEKARI MBILI (2) Mlandizi/Vihingo

Back
Top Bottom