Samson Ernest
JF-Expert Member
- Aug 28, 2014
- 557
- 858
"Hivyo wewe mwanadamu, utoapo hukumu juu yao na bado unafanya mambo yale yale, unadhani utaepuka hukumu ya Mungu?" Warumi 2:3 NEN.
Wapo watu hupenda kusema usiangalie tabia yangu bali zingatia ninachokuambia au ninachokuhubiri au ninachokufundisha.
Hatujui kuwa watu hujifunza zaidi kwa matendo yetu kuliko maneno yetu, unapomwambia mtoto asiwe na tabia fulani mbaya alafu wewe unaifanya, ujue utakuwa unapiga kelele tu.
Ninajua zipo tabia mbaya tulizonazo na hatutamani watoto wetu wawe nazo, ila nasikitika kukuambia kuwa watoto wanajifunza zaidi kwa wanachoona kuliko unachowaambia, umri ambao mzazi unapaswa kujenga msingi mzuri ndio umri ambao watoto wengi hujifunza kwa kuona.
Sio kwa watoto tu, unapowaambia watu pendaneni alafu wewe huna upendo hata kwa familia yako au watoto wako au wazazi wako, ujue hayo mahubiri yatakuwa yanakurudia tu wewe.
Inawezekana watoto wako hawajui mambo yako mabaya ya siri ila kumbuka kila upandacho utavuna, unaweza usivune leo ila uwe na uhakika yale mabaya unayowatendea wengine yatakurudia vilevile na zaidi.
"Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; kwa kuwa cho chote apandacho mtu, ndicho atakachovuna", Gal 6:7 SUV.
Mtu yeyote hapaswi kuwahukumu wengine kwa tabia zao mbaya ikiwa yeye mwenyewe anaifanya hiyo tabia au anaishi katika hayo maisha mabaya yanayomchukiza Mungu.
Kwa mujibu wa neno la Mungu, mtu yeyote hapaswi kuwaelekeza wengine kufanya lile linalostahili kulifanya wakati yeye mwenyewe anashindwa kujirekebisha tabia yake mbaya.
Baadhi ya makanisa huwa yanawashawishi wengine wasiokoka kuacha dhambi wakati wao wenyewe wamedumbukia katika dimbwi la dhambi, mambo mabaya ya dunia hasa uzinzi, uasherati, ulevi, na mambo mengine mabaya.
"Utawezaje kumwambia ndugu yako, ‘Ndugu yangu, acha nitoe kibanzi kilicho ndani ya jicho lako,’ wakati wewe mwenyewe huoni boriti iliyo ndani ya jicho lako? Ewe mnafiki, ondoa boriti ndani ya jicho lako kwanza, ndipo utaweza kuona dhahiri jinsi ya kuondoa kibanzi kilicho ndani ya jicho la ndugu yako", Luka 6:42 NEN.
Kabla hujaanza kuwaambia watu wengine wawe na maisha mazuri yanayompendeza Mungu hakikisha unayaishi hayo unayowaambia, iwapo unaenda kinyume na unayosema, ni heri ukae kimya maana wakati unaongea watakuwa wanakurudishia hayo hayo.
Kipofu hawezi kumwongoza kipofu mwenzie, ikiwa huna upendo kwa mke wako alafu unawaambia wengine wawe na upendo ujue unapaswa kulitenda hilo kabla ya kuwaambia wengine. Na ukiwa unajua huna utii kwa mume wako alafu unawataka wengine wawe na utii ujue unapaswa kutengeneza wewe kwanza.
Injili ya kweli inaanza na mtu mwenyewe, yale maisha yake matakatifu mbele za Mungu, yala matendo yake mazuri kwa Mungu na kwa watu, yanakuwa injili tosha kabla ya kutoa maneno kwenye kinywa chake.
Soma neno ukue kiroho
Liwe jua iwe mvua soma biblia
Mungu akubariki sana
Samson Ernest
+255759808081