Baraka Kasinge
Member
- Apr 4, 2016
- 60
- 69
Kondoo wawili walikuwa wakitokea tofauti za mto. Mmoja akitokea mashariki na mwingine magharibi.
Walipoufikia ule mto, kila mmoja kwa upande wake alihitaji kuvuka. Kwa bahati mbaya, mto ule haukuwa na daraja pana zaidi ya gogo lililokuwa limelazwa kwa kuvukia.
Basi, walipolifikia lile gogo wote walilazimisha kuvuka kwa pamoja.😳 Hakuna hata mmoja aliyekuwa tayari kusimama ili mwenzake apite kwanza.🫢 Hatimaye walipokutana katikati ya lile gogo, walilazimisha kupishana.
Kwa bahati nzuri, kama si mbaya,🤣 gogo like halikuwa na nafasi ya kutosha wao kupishana. Hivyo, walijikuta wamegongana uso kwa uso na wote kuangukia mtoni wakasombwa na maji.🤦🏽♂️
FUNZO: Tunaposhindana kukomoana, tusisahau kujiuliza kitakachotukumba ikiwa tutashindwa. Hata kama tukishinda, bado tusisahau, kukomoana huzaa uhasama, visasi na mwishowe huzua msiba.