Jibu la swali lako linapatikana katika Mhubiri 7:15-21 kwamba:-
Mtu mwadilifu hufa ingawa ni mwadilifu, ambapo mtu mwovu huendelea kuishi maisha marefu ingawa ni mwovu.
16 Basii, usiwe mwadilifu sana, wala usiwe mwenye hekima mno! Ya nini kujiangamiza wewe mwenyewe?
17 Lakinii pia, usiwe mwovu sana wala usiwe mpumbavu! Ya nini kufa kabla ya wakati wako?
18 Inakupasa ushike la kwanza na la pili pia; maana anayemtii Mungu atajengwa kwayo.
19 Hekima humfanya mwenye busara kuwa na nguvu zaidi kuliko watawala kumi mjini.
20 Hakika, hakuna mtu mwadilifu duniani atendaye mema daima bila kutenda dhambi.
21 Usitie maanani maneno yote wasemayo wanadamu, usije ukamsikia mtumishi wako akikutukana. 22Wewe mwenyewe wajua moyoni kwamba umeapiza wengine mara nyingi.