Mr_mkisi
Member
- Sep 24, 2024
- 15
- 47
Ugomvi kati ya wateja na wauzaji wa simu, hasa hizi used za Dubai au refurbished, ni jambo linalotokea mara nyingi. Mara nyingi, chanzo kikuu ni pale simu inapoharibika, na mteja anataka kuirejesha ili abadilishiwe. Kuna wakati muuzaji anakuwa sahihi, na kuna wakati mteja anakuwa sahihi. Je, ni katika mazingira gani hali hizi hutokea?
Naitwa Mkisi
Nauza simu na laptop hapa Kariakoo kwa muda wa miaka 7 sasa. Natoa maarifa na makala kama hizi kila siku. Pia nina group WhatsApp na Telegram kwa updates za bei za jumla za simu na laptop.Kesi za Ugomvi wa Wateja na Wauzaji wa Simu
Nina uzoefu mkubwa wa kushughulikia kesi kama hizi, hasa kwenye simu kuliko laptop. Kesi hizi hutokea pale ambapo:- Mteja amenunua simu, kisha ikaharibika kwa bahati mbaya au makusudi, na anataka kuirejesha dukani ili abadilishiwe nyingine.
Mazingira Ambayo Muuzaji Anaweza Kukusaidia
- Simu yako ikiharibika kwa tatizo la software, kama vile:
- Haishiki mtandao
- Ime-corrupt
- Inastack
- Haipandishi mtandao
- Simu iliyo zima yenyewe tu bila sababu. Hii ni baada ya fundi kuthibitisha kuwa simu imezima bila sababu ya msingi.
Mazingira Ambayo Muuzaji Hataweza Kukusaidia
- Ukiharibu simu kwa kuidumbukiza kwenye maji.
- Simu ikiharibika kwa kupiga shoti kwenye motherboard.
- Simu ikiharibika kioo, iwe kwa bahati mbaya au makusudi (imeanguka, kugongwa, n.k.).
- Ukiamua kubandua sticker inayounganisha kioo na body ya simu, ambayo huonyesha kama simu imefunguliwa au la.
Shida Haswa Huwa Wapi?
Tatizo kubwa ni kwamba:- Wateja wengi hawasomi terms & conditions zilizowekwa kwenye warranty card.
- Kuna dhana potofu kwamba wauzaji wote wa simu, hasa mtandaoni, ni matapeli au wanauza simu mbovu.
Mfano wa Terms & Conditions za Warranty
Kama mteja, unatakiwa kuelewa kwamba warranty haitaweza kusaidia katika hali zifuatazo:- Ukiharibu kioo cha simu kwa bahati mbaya au makusudi.
- Ukiingiza simu kwenye maji.
- Simu ikiwa na tatizo lingine lakini ukairudisha ikiwa na crack kwenye kioo.
- Simu ikipiga shoti.
Ushauri Wangu
- Ili kuepusha ugomvi, ukiona ni ngumu au hatarishi, bora usinunue bidhaa hiyo, tafuta mbadala.
- Tafuta store nzuri ya simu ambayo inauza bidhaa zenye ubora wa hali ya juu.