Kanungila Karim
JF-Expert Member
- Apr 29, 2016
- 20,743
- 25,564
WABENA ni kabila la kibantu linalopatikana katika eneo la Nyanda za Juu Kusini mwa Tanzania wilaya ya Njombe mkoa wa Iringa. Lugha yao inaitwa Kibena na makao yao makuu yanaitwa Ubena.
Makao makuu ya Wabena ni Iringa katika eneo maarufu la Ubena, idadi kubwa ya Wabena inapatikana pia katika wilaya jirani ikiwa ni pamoja na Ulanga mkoani Morogoro, maeneo makuu ya Wabena yamegawanyika katika sehemu tano ndani ya wilaya ya Njombe ambayo ni Ivanging’ombe, Usovi, Ikilavugi, Nyikolwe na Mfirika.
Kibena ni lugha pana yenye utajiri wa maneno na lahaja kuu tano ambazo ni Ki-Kilavwugi inayotumiwa na wakazi wa eneo ya Ilembula; Kisovi inayotumiwa na Wabena wa eneo la Lusisi hadi Makambako.
Lahaja nyingine ni Kimaswamu inayotumiwa na wakazi wa Imalinyi, Njombe mjini na sehemu ya kata ya Mdandu, Ki-Lupembe inayotumiwa na wakazi wa Lupembe na Kimavemba ambacho kutumiwa na Wabena wa Uwemba na sehemu ya tarafa ya Igominyi.
Lugha yao ni moja tu ila tofauti ni ndogondogo, zinazotokana na matamshi. Mfano kukaza “dz”, kwa lahaja zote isipokuwa Kikilavwugi ambacho ingawa inaandikwa “dzi” inatamkwa kama “dji” kama vile ‘umuhudji’. Watumiaji wa lahaja ya Kilupembe inaandikwa “dzi” lakini wanatamka kama “chi” umuhuchi, achile - amekuja, wakati “adjile” (Kikilawugi)... Wengine wote wanakaza adzile, umuhudzi. Tofauti nyingine ni ya kutumia herufi K na H.
Mfano katika maneno Kamwene wengine husema Hamwene, Kangi na hangi pia ukukulima na uhulima. Ingawa historia ya Wabena haitoi jibu sahihi huu ya jina la kabila, watafiti mbalimbali wanahisi kuwa limetokana na ama kazi ya kuvuna ulezi yaani kubena au kutengeneza chumvi kwa kuwa majina ya eneo yalitokana na majina ya watu maarufu au kazi muhimu yenye kuwaingizia wananchi wengi kipato.
Kutokana na tofauti za kijiografia, shughuli za Wabena hutofautiana kutoka eneo moja hadi jingine. Hata hivyo, kwa ujumla Wabena wote ambao hivi sasa hupatikana wilaya za Njombe, Mufindi, Kilombero na Songea ni wakulima hodari. Wabena wanaoshi sehemu zenye mito na mabonde hujishughulisha pia na uvuvi, wakati wale wa ukanda wa juu wanajishughulisha na kilimo na ufugaji.
Wabena wana historia nzuri ya kudumisha ujamaa na ushirikiano kutokana na mfumo wao wa wakibadilishana mazao na mali mbalimbali. Wabena, kabila linalosifika kwa ukaribu pia lina sifa ya kipekee katika historia ya hatua za maendeleo ya binadamu kwa kuwa lilikuwa hodari wa kufua chuma.
Kwa mujibu wa utafiti wa akiololojia uliofawanya na Profesa Paul Msemwa mwaka 2001 katika na maeneo yanayozunguka mji wa Njombe walikuwepo wakulima ambao walifua chuma kuanzia kipindi cha kame ya tano au hata kabla ya hapo, jambo linalodhihirisha kuwa Wabena walikuwa wakifua chuma.
Utafiti huo wa kisayansi umefanyika kwa kuchimbua ardhi kwa lengo la kutafuta masalia ya zana mbalimbali zilizotumiwa na watu wa kale umeweza kuibua masalia ya vipande vya vyungu na masalia ya viwanda vya chuma katika eneo linalokaliwa na Wabena ikiwamno Mgala Isitu, tarafa ya Igominyi.