.......uso kwa uso na mwana JF mwenzangu

Kwi kwi kwi kwi kwi lol!!!! Hahahaha mie mwenyewe karibu nibambwe mara mbili mara ya kwanza jamaa zangu wakanialika kwao. Nikakaa huko for four days kila mara wakati niko kwao nikawa naingia JF kutumia PC yao basi kuna wakati wakaja wote kwenye nilipokuwa mimi nikifuatilia majadiliano ya hapa ikabidi nicheze kama pele ili wasiione ID yangu. Baada ya miezi michache wakaja kwangu nikawa niko humu nao wanaangalia TV basi nikawajoin wote tukawa tunaangalia TV mmoja akadai nionyeshe PC ilipo nataka kutumia nilikuwa sijalog off JF ikabidi nicheze kama pele tena ili ID yangu isijulikane. Baadaye katika mazungumzo mmoja kaanza kuisagia JF kwamba siku hizi wazushi wamekuwa wengi sana haingii sana kama zamani na hata akiingia ni kuchungulia mara moja tu haandiki chochote.

Juzi juzi nikawa kwenye mnuso mmoja watu wakawa wanaongelea ile case ya uforoo wengine wakadai hawaijui lolote kuhusu hiyo kesi. Mdada mmoja akawauliza nyie mnapata wapi habari zenu? Mmoja akajibu magazetini mdada akajibu ukitaka latest habari nenda JF. Mie kimya, mdada akaendelea sasa hivi hapa niko JF (mkononi yuko busy na simu yake) na mkaka mwingine naye hata mimi nasoma yanayojiri kule JF (naye busy na simu yake mkononi) mie natamani nikae upande wao lol!!! Ili nizijue ID zao maana tulikuwa tunaangaliana.

Mwiko kutumia pc za watu kuingia JF simu yangu inatosha kabisa na kama nina wageni simu pia itatumika kuingia huku lol!! Mpaka wageni waondoke.
 

please dont use H.O.E coz it rhymes with W.H.O.R.E.....
 
natamani namie nimjue huyo uliyekutana nae. lol. hebu ajitaje basi tupate uhondo kamili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…