Bushmamy
JF-Expert Member
- Aug 18, 2019
- 9,140
- 15,963
Uhuru wa kupata Habari ni chakula muhimu ambacho kila mtu huiitaji kushiba, awamu iliyopita usomaji wa magazeti redioni katika kurasa za ndani ulifungiwa bila maelezo ya msingi.
Kufungiwa habari za ndani za magazeti kupitia redio wengi wa walioathirika ni wananchi wa vijijini ambao ni ngumu kupata nakala ya gazeti kutokana na kuwa magazeti mengi huuzwa mjini na sio vijijini. Hivyo kusomewa tu vichwa vya habari pekee redioni humwacha njia panda.
Wakati huo huo magazeti hayo hayo husambazwa mitandaoni ambao mtumiaji wa mtandaoni huwa na uwezo wa kusoma habari zote za gazeti husika, lakini kwa Wasikilizaji wa redio na watazamaji wa television ambao idadi yao ni kubwa hukosa kabisa haki ya kupata habari za kila siku kupitia magazeti.